Pinacoladee
JF-Expert Member
- May 22, 2023
- 543
- 596
Hahaha ha,hakuna jipya sana yaleyale tuHeri yako wewe unavyenzo za kusikilizia, huku tukuyu ndanindani tuna hali mbaya.
Anyways utatu-update.
1. Wameongelea swala la aptitude test/online test utafanyik kwenye vituo vyao vya kila mkoa hivyo watu waupdate current location kweny account zao,na ikitokea haupo kwenye kituo ulichopangiwa basi nenda kituo kilichopo karibu nawe lakini unaweza kuchelewa kuhudumiwa
2. Wamesisitiza tu tusome tangazo na kanuni za ajira, tuzingatie tangazo la kazi linataka nini,na zile general conditions muhimu mno
3.Wamegusia interview haitok nje ya majukumu. Hivyo kwenye tangazo la kazi tusome majukum ya kazi na tuelewe vizuri. Kuna keywords mule tutapata kitu au direction tusome wapi zaidi.
4.Kwa mujibu wa katibu placement zinachelewa sababu kuu ni vibali
5.Pia unaweza kufanya interview zaid ya 1 kwa siku ikitokea zimepangwa siku 1 watatenganisha tu muda
6.Pia wamesema kutakua wanatufanyia psychometric test,kutupima haiba,akili au jinsi tunavyojitambua ili kujua sisi ni watu wa aina gani na wanampelekea mwajiri mtu wa aina gani🤣
7.Matokea ya aptitude test ni ya haraka mno unarud home ushajua mbivu na mbichi mapema tu🤣..nadhan awa waliofanya hivi karibuni watakua na experience zaidi.