Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,689
- 3,268
Habari. Nasikia zamani Dar watu binafsi hawakuruhusiwa kumiliki daladala za abiria. Usafiri ilikuwa shida sana. Baadaye serikali ikaja kuruhusu na ahueni ya usafiri ikapatikana. Serikali kuruhusu watu binafsi kuzalisha na kuuza umeme. Huku miundombinu ya umeme iwe kama barabara zinavyotumika na daladala inaweza saidia kupunguza shida ya umeme?
Na uzalishaji si mpaka uwe mkubwa. Kuna nchi mtu ukiweka umeme wa sola unaunganishwa kwenye gridi. Kama unazalisha wa kukutosha na ziada, basi ile ziada inaenda kwenye gridi na unalipwa. Kama unazalisha kidogo basi utachukua kwenye gridi ili kufidia na utalipia hicho kiasi ulichochukua.
Maana hii shida ni too much. Wamekata hapa mpaka jioni. Dola zitapatikanaje kwa mtindo huu.