SoC04 Tuuvune na kuuhifadhi umeme kwa matumizi ya baadae ili kupunguza tatizo la mgao na kukatika kwa umeme katika nchi yetu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mabula marko

Member
Jul 18, 2022
44
38
TUUVUNE NA KUUHIFADHI UMEME KWA MATUMIZI YA BAADAE ILI KUPUNGUZA TATIZO LA MGAO NA KUKATIKA KWA UMEME KATIKA NCHI YETU
1715178392985.png


Utangulizi

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazojitegemea katika swala ya miundo mbinu ya nishati ikiwa inategemea vyanzo mbali mbali kufua na kuzalisha umeme ikiwemo maji, upepo na mashine zinazotumia mafuta bila kusahau gesi pia.

Pamoja na jitihada mbali mbali ambazo kama taifa limekuwa likifanya kuhakikisha tunakuwa na nishati ya umeme ya kutosha tumeshuhudia uhaba mkubwa wa umeme hasa kipindi ambacho kuna upungufu wa maji katika vyanzo vya kufua umeme hali ambayo imekuwa ikisababisha kutokuwa na uhakika wa nishati ya umeme katika viwanda ,majumbani na kwa mtu mmoja mmoja katika kazi zao, hivo kusababisha hasara za kiuchumi kwa viwanda na mtu mmoja mmoja katika shughuli za kila siku, kuungua kwa majengo na hasara zinginezo ambazo zinatokana na kukosekana kwa umeme lakini pia kukatika kwa umeme .

Hivo basi kuna haja kubwa ya kuvuna nishati hii ya umeme kutoka katika vyanzo vyetu pindi inapopatikana kwa wingi na kuuhifadhi kwa matumizi ya hapo baadae kutakapo kuwa na upungufu, kwani mara kadhaa tumepata taarifa kuwa umeme umezalisha Zaidi ya mahitaji na hata kuzima mashine baadhi kumbe badala ya kuzima tungeendelea kuzalisha kisha tukavuna na kuuhifadhi kwa ajili ya kutumia hapo baadae tutakapokuja kupatwa na changamoto ya upungufu wa umeme kama taifa ili kuepuka tatizo la kukatika umeme mara kwa mara au mgao wa umeme ulio pitiliza.

Namna ya kuvuna na kuhifadhi nishati ya umeme

Kumekuwa na njia mbali mbali ambazo dunia imekuwa ikizibuni ambazo hata kwetu Tanzania tumekuwa tukizitumia kama kuchimba mabwaya ya kuhifadhi maji kwa ajili ya kuhifadhi maji hayo na kuyatumia kuzalisha umeme pindi maji hayo yatakapo pungua katika vyanzo vingine.

Sambamba na hayo yote kuna njia ambayo kama taifa kupitia shirika letu la umeme na wadau wa nishati tunaweza itumia kuuvuna umeme katika vyanzo vyetu vyote upepo, maji na mashine na kuuhifadhi ili tuutumie wakati kukiwa na ukosefu ama upungufu wa umeme.

Kuvuna na kuhifadhi nishati kwa njia ya joto katika tanki maalumu (mtambo). Njia hii hutegemea kupasha joto kitu kwa kutumia nishati ya umeme iliyopo kwa wakati huo,kitu ambacho huwa kama daraja(medium), kinaweza kuwa maji au jiwe au chumvi, hivo pindi maji au jiwe au chumvi itakapo pashwa joto mara kadhaa huweza kuhifadhiwa na joto hilo la umeme kwa muda fulani kisha kutumika pindi umeme utakapohitajika, daraja (medium) inaweza hifadhiwa katika mtambo au mfumo maalumu (tanki)

Picha ikionesha muonekano wa eneo la kuhifadhi umeme kwa nje picha na medaAcademy.com.
thermal1.jpg


Njia hii ya uhifadhi umeme inaweza fanyika katika njia mbili kuu ambazo

  • Njia ya kutumia maji au jiwe na chumvi kuhifadhi umeme na kuwezesha kutumika pindi utakapohitajika tena , hapa umeme huruhusiwa kuyachemsha maji au jiwe katika kiwango Fulani cha joto katika chumba au tanki (mtambo) maalumu kisha kuhifadhiwa kwa muda ambao mtumiaji ata hitaji kutumia kwa kuunganisha katika mkongo wa taifa au eneo husika (sensible thermal)
  • .Njia hii huwa haitegemei mabadiliko ya joto badala yake mabadiliko ya kiumuundo kwa daraja (medium) iliyotumika wakati wa ujazaji wa umeme katika mtambo au mtanki hilo la kuhifadhi umeme kama ulivyo undwa mfano kama ni maji kubadilika kuwa balafu na kadhalika.(Latent heat)
Muundo wa tanki au mtambo kwa ndani picha na medaAcademy.com
HP333.jpg

Picha ikionesha namna ya uvunaji na uhifadhi wa umeme picha na mtandao
HPO444.jpg

Picha ikionesha namna ya kutoa umeme katika mtambo wa kuhifadhia umeme picha na mtandao
HPO555.jpg


Umuhimu au Faida za kuhifadhi nishati ya umeme

Kuhifadhi nishati ya umeme ni muhimu kwa sababu inatoa fursa za kuboresha ufanisi, kuimarisha usalama wa gridi ya umeme, kusaidia kusambaza umeme wakati wa mahitaji au upungufu wa uzalishaji. Hapa kuna maelezo zaidi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi nishati ya umeme:
  • Kupunguza Mahitaji ya Kupandishwa kwa Nguvu (Peak Demand):
Kuhifadhi nishati ya umeme inaruhusu matumizi ya umeme uliohifadhiwa wakati wa kipindi cha uzalishaji mkubwa na kutumika wakati kukiwa na upungufu wa nishati hii hivo
Hii inapunguza hitaji la kupandisha kasi ya uzalishaji wa umeme wakati wa uhitaji mkubwa au upungufu wa nishati hii, ambapo kwa kawaida hufanyika kwa kutumia vyanzo vya nishati ya ziada ambavyo vinaweza kuwa vya gharama kubwa au vina athari kubwa kwa mazingira.
  • Kuimarisha Usalama wa Gridi ya Umeme:
Kuhifadhi nishati ya umeme husaidia kudumisha usawa katika gridi ya umeme na kusaidia kuzuia kukatika kwa umeme na matatizo mengine ya usambazaji.
Gridi zenye uwezo wa kuhifadhi nishati hupunguza hatari ya matukio yasiyotarajiwa kama vile upotezaji wa umeme na vurugu za kusambaza umeme.
  • Kupunguza Utegemezi kwa Mafuta ya Petroli na Makaa ya Mawe:
Kuhifadhi nishati ya umeme kunawezesha matumizi zaidi ya vyanzo vya nishati safi na endelevu kama vile nishati ya jua, upepo, na umeme wa maji.
Hii inachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na kuboresha afya ya mazingira kwa kupunguza matumizi ya mafuta ya petroli na makaa ya mawe.

  • Kuwezesha Maendeleo ya Uchumi:
Kuhifadhi nishati ya umeme inawezesha na inasidia Zaidi kuwa na uhakika wa umeme katika maeneo ya uzalishaji yaani viwanda na mashamba na katika maeneo ya biashara na shughuli za wananchi
Hii inachochea ukuaji wa uchumi endelevu na kukuza ajira kwa wanchi.

  • Kupunguza lawama kwa serikali na wadau wa nishati kwani kuhifadhi umeme kunatoa nafasi ya uhakika wa umeme wakati wote

Hitimisho

Nikihitimisha juu ya wazo au ubunifu huu ningependa kuwaomba wadau na watalamu wetu katika mambo ya nishati ya umeme waweze kuulifanyia utafiti Zaidi wazo hili au ubunifu na kujaribu kuitumia ili tuweze kuvuna na kuhifadhi nishati ya umeme ya kutosha hasa wakati ambapo uzalishaji wake unapokuwa mwingi ili kuwa na umeme wa kutosha wakati ambao kuna upungufu na uhitaji mkubwa wa nishati hii hali ambayo itatusaidia kupunguza shida ya kukatika mara kwa mara kwa umeme na pia uwepo wa mgao wa umeme katika nchi yetu hasa katika kipindi hii cha dhima ya Tanzania ya viwanda ambavyo huhitaji Zaidi nishati ya umeme katika shughuli za uzalishaji na pia watu wanahitaji sana nishati hii katika matumizi na shughuli zao za kila siku hakika Tanzania ya kesho bila tatizo la kukatika kwa umeme inawezekana

“Tunayanganza maisha yako”

Asante
 

Attachments

  • HP333.jpg
    HP333.jpg
    38.1 KB · Views: 1
Nikihitimisha juu ya wazo au ubunifu huu ningependa kuwaomba wadau na watalamu wetu katika mambo ya nishati ya umeme waweze kuulifanyia utafiti Zaidi wazo hili au ubunifu na kujaribu kuitumia ili tuweze kuvuna na kuhifadhi nishati ya umeme ya kutosha hasa wakati ambapo uzalishaji wake unapokuwa mwingi ili kuwa na umeme wa kutosha wakati ambao kuna upungufu na uhitaji mkubwa wa nishati
Wazo zuri kaka,

Na kila siku teknolojia ya kuhifadhi umeme zinazidi kuvumbuliwa na kuboreshwa. Sand battery, gravity battery, na kuna nyingine wanapooza hewa badala ya kupasha joto lisilohifadhika kirahisi. Namaanisha nini?

Teknolojia tayari zipo huko duniani, ni kufanyia tu utafiti kujua kipi ambacho kitatufaa kwetu Tanzania. Na kama kawaida mimi huwa ninaanza na mwananchi mmoja mmoja kabla ya taifa.

Itatusaidia kama kila mmoja hapo kwake nyumbani ataangalia namna ya kuwa na mfumo wa kuhifadhi umeme kwa mabetri(au kuwa na nishati mbadala( jua au upepo)kwa ajili ya dharula binafsi.

Ahsante sana kaka
 
ingawa joto nalo linahifadhika , cha msingi tafiti zifanyike tuangalie njia ipi nzuri ikizingatia muda wa kuhifadhi pia
 
Back
Top Bottom