KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,161
- 33,028
Kabla ya WhatsApp nilikuwa na line za nchi mbalimbali. Ililazimu Kila nchi uliyofika ununue line. Mwisho nikajikuta na line zaidi ya 100. Nikijua naenda Italy nachukua SIM, Naenda Switzerland nachukua MOBISTAR, n.k. Kwa sasa natumia Togocel na Moov. Hii ni mitandao ya Togo. Togocel ni shirika la umma na Moov ni kampuni binafsi.
Kwa hiyo nina uzoefu mkubwa wa mitandao.
Huko kote mteja habughudhiwi. Kampuni haiwatumii wateja meseji hovyohovyo. Na wakitaka kukutumia wanakuuliza kwanza kama unaruhusu kupokea meseji zao? Ukijibu "non" wanakuacha.
Hapa Tanzanie kuna kitu hakiko sawa. Kutwa unapokea meseji "unsolicited" zaidi ya 10! Mara uulizwe kati ya Alikiba na Diamond nani zaidi?!! Mara uambiwe "chaguo wimbo"?!? Mara uonywe kuhusu matapeli mtandaoni kana kwamba hujui Kuna matapeli mtandaoni! Mara tabiri nani atashinda Kariakoo Derby!! Kama mchezo wangu ni gololi au miereka au kulamba asali? Kwa Voda Wana provision kama eti unataka kuendelea kupokea meseji zao, Cha ajabu hata uki click hapana ndio zinaongezeka! Pourqoi? Why? Kwa Nini? Ni kini icho avae?
Sasa jana nikapokea simu toka Vodacom. Kibinti kikaanza *habari Yako mteja mpendwa, naongea na nani"??? Nikamjibu unaongea na uliyempigia" Kakajibu "nataka tu kuthibitisha ninaongea na nani" Nikajibu "kwani wewe umempigia nani? Kassim Majaliwa? Kakaona ujinga wake kakaniambia "natumaini naongea na Mlamba Asali"? Nikakajibu "kumbe unajua"?
Basi kakaomba samahani. Kakaanza "napenda nikupe taarifa ya huduma yetu ya VODA BIMA, tuna bima aina tatu ..... ". Kakaeleza weeee mwishoni kakaniuliza "unataka kujiunga nikuunganishe sasa hivi mlamba asali". Nikakaambia "yaani nijiunge na bima Kwa simu tu? Kakajibu * ndio utaratibu wetu". Mimi nikakaambia siwezi kujiunga na bima kihivyo. Kakaniuliza "kwani hujaelewa Nini hapo" nijakajibi "sijaelewa VODA BIMA". Kwa hasira kakata simu.
Yaani sijui wamewaona wateja ni mbuzi? Yaani kweli mtu ajiunge na mfuko wa bima Kwa kupigiwa simu? Ni bima ya kivipi sampuli hii? Na hivi nani karuhusu Hawa kufungua mifuko ya bima? Yaani wanafanya biashara zote? Mawasiliano na bima? Wakifungua DECI?
Bwana Mdogo NAPE vipiiiiii? Hebu tizama hili suala . Wakataze kusumbua wateja Kwa meseji zao. Halafu piga marufuku huu utapeli wa BIMA za kampuni za simu. Nimesikiliza mafao na malipo unayotakiwa ulipe ni utapeli mtupu. Bima waachie kampuni za bima wao waboreshe mawasiliano.
La mwisho bwana Nape: gharama za wifi hapa nchini ni kubwa mno. Pale Lome Mimi nalipia wifi XOF 15000 sawa 12000 TZS Kwa mwenzio. Bundle hiyo hiyo hapa Dar nalipia 75000/= !!! Why? Na Togo ziko kampuni 2 tu zinatoka huduma ya wifi (Canal + na Togotelecom). Canal + ni private Togotelecom ni shirika la umma. Athari za wifi kuwa gharama ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi. Hebu na huko patazame. Msiache waumuze walaji. Tanzanie ni tajiri mara elfu kwa Togo.
Imeandaliwa na
Yahya Msangi