aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,636
3,620
2C99D1E7-C117-4DE0-BAD3-0C595548DB4C.jpeg

Nikupongeze kwa hatua hii ya kuzindua gari uliyoitengeneza wewe mwenyewe kama ulivyotuaminisha ila naomba basi utusaidie yafuatayo ili utuvutie zaidi kuweza kununua gari yako

1. Je, ukichaji gari ikajaa unaweza kutembea kwa umbali wa kilomita ngapi?
2. Je, vipuri vya gari vikiharibika vinapatikana?
3. TBS imethibitisha ubora wake?
4. Je kuna aina nyingine tofauti na iliyozinduliwa?
5. Speed ya gari ni ngapi maximum?
 
Kwa miaka minne au mitano ijayo, huyu jamaa anaanza kutegeneza self driving. Vijana inabidi waanze kusoma IA, ML, DL. Image & video processing, sensors etc. Japo ni changamoto bado self driving nchi nyingi za africa kwa sababu ya miundombinu.

Jana niliona presentation, hakutolea ufafanuzi mambo mengi ya msingi kuhusu hili gari

Lkn jamaa hongera zake. Kuna kipindi nilipishana na pikipiki ya umeme kama mara mbili sijajua kama ni kampuni ya kibongo au wame import
 
1. Ukichaji kwa masaa sita linakuwa kimekula units ngapi za umeme?
2. Kinauwezo wa kusukuma Tani ngapi if not kilos?
3. Kikiharibika kinaenda garage au kwa fundi simu/ radio?
4. Kina shelf life ya miaka mingapi kwa engine take na max load capacity
 
Back
Top Bottom