Changamoto gani umewahi kutana nayo sehemu umejitolea kufanya kazi?

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
88
105
Wakuu habari,

Embu tujadili hili swala hapa. Mimi baada ya kumaliza form 6 niliamua kujitolea kwenye shule fulani hivi ya sekondari nikisubiri kujiunga na chuo kikuu.

Sasa bwana pale kuna changamoto nilikutana nayo kwamba kuna supervisor wangu alinielewa. Mimi nikamkatia bwana kwa sababu siwezi kuwa na mahusiano na mtu ambae niko nae kwenye mazingira ya kikazi maana najua lazima kuna namna moja au nyingine itaathiri utendaji wa kazi.

Yule msela alinisumbua bwana yaani sehemu ya kazi ikageuka a living hell hadi akitolea remarks mbovu hadi nikafukuzwa na headmaster wa pale. Hilo tukio sitakaa nilisahau kwa kweli lakini nilijifunza vitu vingi sana.

Na nyie mmeshawahi kukutana aua unakumbana na situation kama hii au changamoto yoyote umewahi kukutana nayo sehemu ya kazi kama mfanyakazi, intern au volunteer?
 
Mimi nilizinguana na mwalimu mkuu, niliajiriwa tempo kama ticha wa math, nikawa napiga vipindi vyangu nikimaliza nasepa, naingia mtaani kufundisha tuition, ticha mkuu akawa analazimisha nibaki mpaka jioni, nikamwambia madam ukweli halisi vipindi vya math vinaisha asubuhi kabla ya lunch, madaftari na sahihisha, mazoezi natoa, mwanafunzi akihitaji msaada wa ziada napatikana so kwa nini niendelee kukaa mpaka jioni??!! Madam akawa haelewi kabisa.

Ukifika mwisho wa mwezi mshahara hadi muanze kuulizana tena, nikaona huyu madam hanijui vizuri, nilipopokea mshahara wangu wa mwezi wa pili tu, sikurudi tena ile shule. Niliondoka bila kuaga na kuendelea na mishe zangu mtaani, madama alipiga simu sana bila mafanikio.

Hapo ndio ilikua experience yangu ya kwanza kukutana na watu toxic mahala pa kazi
 
Wakuu habari,

Embu tujadili hili swala hapa. Mimi baada ya kumaliza form 6 niliamua kujitolea kwenye shule fulani hivi ya sekondari nikisubiri kujiunga na chuo kikuu.

Sasa bwana pale kuna changamoto nilikutana nayo kwamba kuna supervisor wangu alinielewa. Mimi nikamkatia bwana kwa sababu siwezi kuwa na mahusiano na mtu ambae niko nae kwenye mazingira ya kikazi maana najua lazima kuna namna moja au nyingine itaathiri utendaji wa kazi.

Yule msela alinisumbua bwana yaani sehemu ya kazi ikageuka a living hell hadi akitolea remarks mbovu hadi nikafukuzwa na headmaster wa pale. Hilo tukio sitakaa nilisahau kwa kweli lakini nilijifunza vitu vingi sana.

Na nyie mmeshawahi kukutana aua unakumbana na situation kama hii au changamoto yoyote umewahi kukutana nayo sehemu ya kazi kama mfanyakazi, intern au volunteer?
Kulikuwa na mradi wa ujenzi nikapewa kitengo Cha uratibu wa manunuzi ya vifaa na matumizi yake pale site. Hii nafasi nilitamani niiteme maana nilikutana na majaribu ambayo hata ayubu asingeweza kupona
 
Wakuu habari,

Embu tujadili hili swala hapa. Mimi baada ya kumaliza form 6 niliamua kujitolea kwenye shule fulani hivi ya sekondari nikisubiri kujiunga na chuo kikuu.

Sasa bwana pale kuna changamoto nilikutana nayo kwamba kuna supervisor wangu alinielewa. Mimi nikamkatia bwana kwa sababu siwezi kuwa na mahusiano na mtu ambae niko nae kwenye mazingira ya kikazi maana najua lazima kuna namna moja au nyingine itaathiri utendaji wa kazi.

Yule msela alinisumbua bwana yaani sehemu ya kazi ikageuka a living hell hadi akitolea remarks mbovu hadi nikafukuzwa na headmaster wa pale. Hilo tukio sitakaa nilisahau kwa kweli lakini nilijifunza vitu vingi sana.

Na nyie mmeshawahi kukutana aua unakumbana na situation kama hii au changamoto yoyote umewahi kukutana nayo sehemu ya kazi kama mfanyakazi, intern au volunteer?
nilionekana tishio kwenye ajira na nafasi za watu pale ofisini, kwa ile bidii ya kazi, confidence, appearance, ability na ile voice of authority nilichukiwa sana na wakuu wa idara flan flani hadi nikawa naitwa mnoko 🤣

hakuna kazi ya team ama binafsi ili lala eti kwasababu ya uvivu au tamaa za watu fulani. mathalani tumeenda kufanya kazi mkoani kwa malipo na posho, halafu ile kazi tumeifanya kwa siku2 imeisha na kukamilika, halafu ati mtu anakuja kushauri tuendelee kukaa mkoani kwa malipo, kwa kurefusha siku2 zaid kwasababu ya tamaa ya pesa, wakati kazi hakuna imeisha 🐒

au ati kitu ikae vibaya ofisini nisiweke ikae vizuri, no ilikua Lazima niweke vizuri mahali sahihi. In short I was smart to date before wananchi 🐒
 
Back
Top Bottom