Search results

  1. aise

    Buguruni kunalemaza sana wakuu, hebu angalia nguvu ya 500!

    Hii ni Supu ya shilingi 500 hapa Buguruni, hivi kwa hali hii unaweza ukapata akili ya kuwa na vitu vikubwa? Buguruni hii kuna mpaka Chips za 500. Wali ule unaouzwa 2,000 maeneo mengine hapa tunauziwa 1000, kuna mpaka kipimo cha 500 kama ukiomba unapata wali na maharage! Nataka nihame hapa...
  2. aise

    Niko polisi imepigwa filimbi ya kushusha bendera watu wote wakasimama! Hii maana yake nini?

    Habari za jioni wakuu! Niko polisi hapa kituo ambacho kipo karibu na soko! Imepigwa filimbi na watu wote wamesimama mpaka jamaa kamaliza kushusha bendera akapiga tena filimbi ndiyo watu wakaendelea na mishe! Hivi huu si utumwa? Maana yake nini kwa kizazi cha leo? Mimi yote hayo yakiendelea...
  3. aise

    Analia mke wake kutumiwa ujumbe usiku na mwanaume mwingine, ametudhalilisha wanaume

    Huyu jamaa kwakweli naona hana haiba ya kiume! Asubuhi yote hii kwenye gari amepiga simu kwa mwanaume mwenzie analia kuwa kwanini anachati na mke wake usiku. Yaani watu wamebaki wanamcheka na kusikitika tu hapa. Kwa mujibu wa maelezo yake mkewe anafanya kazi kiwandani, na kazi za viwandani...
  4. aise

    Tigo rekebisheni mtandao wenu, tangu jana mpaka sasa ni shida sana kuupata

    Eneo nilipo watu wote wenye laini za Tigo mtandao hausomi! Kwenu hali ikoje? ======
  5. aise

    Una maoni gani kwa matokeo haya ya kidato cha pili Shule ya Diplomasia inayopatikana Dar?

    Kwa matokeo haya una maoni gani? Shule ipo Jijini Dar es Salam na siyo Nachingwea.
  6. aise

    Watoa huduma na wafanyabiashara badilikeni katika hili

    Kuna hii kasumba sijui tuseme ulimbukeni limeenea sana kwa wafanya biashara na watoa huduma. Mfano unaenda dukani kununua shati, muuzaji anakwambia bei ya shati ni 40,000. Wakati shati kama hilo kwa kawaida huwa bei yake ni 15,000, Sasa unamuuliza mbona bei sana? Anajibu "ulikuwa na sh ngapi?"...
  7. aise

    Kuna tofauti gani kati ya Lecture na Teacher?

    Wakubwa naomba kupewa maana na tofauti kati ya Lecture na Teacher.
  8. aise

    Hawa city wanapita kusumbua wafanyabiashara mpaka saa 5 usiku?

    Wakuu niko Buguruni hapa, hawa city wanapita mpaka muda huu kusumbua wafanyabiashara. Kwa hali niliyoiona, ipo siku yatatokea madhara makubwa sana. Watakuja kuuana hawa wachuuzi na migambo. Saa tano usiku wanatafuta nini?
  9. aise

    Nahitaji Biashara au Shughuli ya kuingiza faida ya Tsh 70/= ndani ya dakika moja kwa masaa 14

    Wachumi habari! Mimi nakuja kwenu nahitaji muongozo wa biashara au shughuli yoyote ile inayoweza kuingiza faida ya Shilingi 70 za Tanzania kwa kila dakika, kwa masaa 14, siku 7 za wiki. Ni shughuli au biashara gani inaweza kunipatia faida ya shilingi 70 kwa dakika, ndani ya masaa 14, siku 7...
  10. aise

    Nilicho jifunza kipindi nafanya kazi kwenye mashamba ya mkonge!

    Kuna kipindi nilienda kufanya kazi kwenye mashamba ya mkonge, wakati nafika nilipokelewa vizuri na nikapewa chumba, kuna vijumba vya wafanyakazi vimejengwa, ukifika unapewa kijumba chako. Kwakuwa nilikuwa nimesota kweli kweli, nikapewa ofa ya kula kwa wiki mbili bure {kuna wafanyakazi fulani...
  11. aise

    Wimbo wa Diamond Zuwena ni wa kawaida sana

    Huu wimbo ni wa kawaida sana, ni vile tu umeimbwa na Diamond. Diamond anajua, ila kwa huu wimbo hapana.
  12. aise

    Biashara bwana!

    Mara nyingi huwa napita pale Feri , ni saa moja asubuhi lakini kuna jamaa wanauza juisi baridi ya miwa. Watu wamejazana sana mara zote utadhani ni mchana wa saa saba! Nilidhani ile biashara inauzika mchana, ila pale kuanzia saa moja kasoro asubuhi jamaa wameshajaza watu.
  13. aise

    Nahitaji godoro 5 kwa 6

    Wakuu nahitaji godoro used 5×6, nchi kuanzia 8. Niko kigamboni. Liwe katika hali nzuri
  14. aise

    Hivi ni kweli kuna wanyama ukiwagonga hupati kesi?

    Habari wakuu, kuna jambo nimelisikia mara kadhaa watu wakisema, kuwa kuna baadhi ya wanyama au ndege ukiwagonga wapo ambao unashitakiwa na wapo ambao hakuna kesi ila kibinadamu unamalizana tu na mmiliki. Kwa mfano ukigonga bata au kondoo, hapo kesi ipo na itafika mbali. Ila kama utamgonga...
  15. aise

    Wimbo wa Marioo na Barnaba classic, 'Marry me' ni mzuri

    Habari wakuu, mimi ni mpenzi wa nyimbo zote nzuri. Mwezi Septemba Barnaba na Marioo walitoa wimbo wao unaitwa "Marry Me". Kwakweli ni wimbo mzuri sana. Unaweza kuusikiliza ukiwa sehemu yoyote na watu wa aina yoyote bila shaka. Nimekaa nausikiliza peke yangu, nikaona siyo mbaya kushirikisha na...
  16. aise

    Kuna tofauti gani kati ya 4WD na AWD?

    Habari wakuu, kwa mwenye uelewa. 4WD ni nini? na AWD ni nini Ni ipi tofauti kati ya 4WD na AWD?
  17. aise

    Wazo simple la kujipatia kipato

    Hili ni wazo simple, kwa mtu simple. Kuna wale watu ambao tayari mjini wanatafuta hela ya kula tu na kulipa kodi, basi hili ni wazo poa kwa ajili yako. Kwakuwa ndiyo unaanza, Nunua maharage 1kg, mchele 3kg na walau robo ya nyama. Nenda asubuhi sana stendi, pika chakula chako, mpaka saa...
  18. aise

    Maisha haya aisee, jana ilikuwa harusi leo imekuwa msiba

    Wakuu, hapa mtaani kwangu kuna ndugu yetu nyumbani kwake kulikuwa na harusi(mtoto wake alikuwa anaoa). Ndoa imefungwa vizuri kabisa, watu tumekula ubwabwa mpaka basi, na wanywaji wamekula bia mpaka basi. Cha kusikitisha leo asubuhi mzee wa watu kaenda Kibaoni kununua pumba za kuku wake...
  19. aise

    Hivi Uchagani watu wanafundishwa nini kuhusu Pesa?

    Jamani kwa wale ambao mmewahi kuishi uchagani, watu wa huko wanafundishwa nini kuhusu pesa? Watu karibia wote wanaotoka uchagani ni wafuatiliaji wazuri sana wa pesa. Jamii zote zinapenda pesa, ila hii jamii ya watu wa kaskazini ni kama vile ina kitu cha ziada kwenye kupenda pesa. Hii...
  20. aise

    Nataka nianze biashara ya kuuza Ugali na Kitimoto Rost

    Wakuu, kuna sehemu imechangamka sana. Pilikapilika za watu ni karibia 24 hours. Eneo hili kuna vilabu vya pombe vingi sana. Kwa ufupi hapa ni uswahilini. Sasa nataka niwawekee kitimoto rost na ugali. Changamoto ninayoiona hata kabla sijaingia kwenye hii biashara ni watu wa eneo hili...
Back
Top Bottom