Habari za jumapili!
Ni wivu katika jamii au ni jambo gani?
Ña hii tabia ipo kwenye jamii maskini hasa huku Afrika,
Ni kwànini mdada akiwa mzuri wale ambao hawakujaliwa uzuri humpa maneno mabaya na kumhusisha na umalaya, udangaji, ukahaba n.k?
Wakati ûkienda site unakuta hali ni tofauti...
RIWAYA YA CONNECTION
Mtunzi: Robert Heriel
Mwaka 2024
Riwaya; CONNECTION
Kazi hii itarushwa katika mitandao kwa akaunti hizi:
Facebook: Robert Heriel Tz
Jamii Forum: Robert Heriel Mtibeli
WhatsApp +255693322300
Maandishi ya Robert Heriel Kwa Lugha ya Kiswahili. Hairuhusiwi kunakili na...
Kwema Wakuu!
Nipo kwenye kumi la tatu. Lakini Watu wengi wanapokutana na mimi hushindwa kukadiria umri wangu na wengi huniona nina umri mdogo. Yaani huniona kama nipo chuo hivi au nimezaliwa miaka ya 2000 jambo ambalo sio kweli.
Nimeandika hivi kwa wale ambao wanataka miili yao isichoke...
Habari za jumapili!
Zile porojo za Watu waongo kuwa mzazi ni mzazi zinaenda kufutika. Kila siku nawaambia hapa, mahusiano ya Watu yanatokana zaidi na ukaribu wao jinsi wanavyoishi na kutendeana.
Kuzaa sio sababu ya mtu kukupenda.
Upendo unasababu kuu zifuatazo;
1. Hisia za ndani.
Hii mara...
FAMILIA ZENYE LAANA, TAIFA LENYE LAANA,
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Familia zenye laana huzalisha taifa lililolaanika.
Làana ni malipo ya uovu ulioufanya wewe mwenyewe au uliofanywa na Watangulizi wako.
Baraka ni malipo ya Wema kwa uliyoyafanya mwenyewe au yaliyofanywà na Watangulizi...
MUNGU WA WAYAHUDI "YEHOVA" hawezi HATAMBUI MWANAMKE KAMA MCHUNGAJI, NABII AU MTUME. WANAWAKE WANAOJIITA WACHUNGAJI au MANABII WANA mungu MWINGINE
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
YEHOVA kama Mungu wa wayahudi hatambui cheo cha mwanamke kuwa mchungaji, Nabii, au Mtume.
Unapozungumzia...
Kwema Wakuu!
Juzi kuna dada mmoja alinicheki na kuniomba ushauri kuwa afanyeje ili amkomeshe kijana mmoja ambaye kwa madai yake anasema amemkatili.
Sisi wanaume wengi wetu hatukomolewi wala kuumizwa na Matusi yenu.
Sisi wanaume wengi wetu hatuumizwi wala kukomolewa na maringo au kejeli au...
Wakuu kwema!
Kuna jambo huwaga najiuliza kila siku kwenye hivi vita vinavyoendelea huko Mashariki ya kati baina ya Israel na Hamas.
Wakati wanawake na watoto wanapouliwa huko Gaza, Wanaume zao wanakuwa wapo wapi?
Je, wanakuwa wanapigana?
Je, wamekimbia na kuacha familia yao?
Je, wanawatumia...
MTU AKIFA ANATAKIWA AZIKWE WAPI? MIGOGORO YA KUZIKA MAITI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Mwezi Aprili nilifiwa na Bibi yangu kipenzi ambaye ndiye aliyenilea, kwangu alikuwa kama Mama. Nilijifunza mengi kupitia yeye, madhaifu na ubora wake. Mazuri na mabaya yake.
Maziko ya Bibi yangu...
Kwema Wakuu!
Watanzania waliowengi ni Conservative(Watu ambao ni wagumu kubadilika au wanachukia au kuogopa mabadiliko)…
Sio ajabu mtu ni muislam au mkristo kwa sababu alizaliwa na kukulia kwenye Ukristo. Sio ajabu mtu ni Simba au Yanga kwa sababu alipokulia ni Washabiki wa Simba na Yanga...
ANAYOFANYA CHRISTINA SHUSHO NI MATOKEO YA WANAUME WENGI KUOA WANAWAKE WATUMWA "WASIOHURU. SIKU WAKIPATA UHURU WAO HAYO NDIO HUTOKEAGA.
Anaandika Robert Heriel
Mtibeli
Huwezi mfanya Mwanamke mtumwa alafu ukamuita Mkeo.
Unajua Watu wengi wamechukua wanawake na kuwageuza watumwa wa kingono na...
VIJANA WA KIUME LAZIMA MUELEWE KUWA KUNA WANAWAKE WANAOWAZIDI KWA MBALI KIUWEZO IWE WA AKILI, UCHUMI NA MAONO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
NI kweli wewe ni mwanaume lakini elewa wapo wanawake wanauwezo zaidi yako. Hilo ukubali au ukatae lakini ndio ukweli huo.
Wanaume wengi hujikuta...
MZAZI JUKUMU LAKO NI KUNIFUNDISHA JINSI YA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NA SIO UNIFANYIE MAAMUZI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Wewe ni wewe. Mimi ni Mimi. NI kweli wewe ni mzazi na mimi ni mtoto. Lakini hiyo haimaanishi kuwa wewe ni Mimi. Utabaki kuwa mzazi lakini hautakuwa mimi na mimi sitakuja...
MAMBO MENGI NI YAKAWAIDA ILA WAMEYA- OVERRATED NA KUWAFANYA WATU DHAIFU KUYAOGOPA ISIVYOSTAHILI. USIWE DHAIFU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Kama ni msomaji wa makala zangu utagundua kuwa moja ya mambo ninayoyarudia ni pamoja na suala hili la uongo wa makusudi unaovumishwa ili kuathiri...
Kwema Wakuu!
Bado nafanya utafiti nipate uhakika wa moja kwa moja lakini mpaka sasa majibu yangu yanamuelekeo wa asilimia kubwa inayozidi 80% ya wanawake wembamba kuwa na tabia ya gubu, mdomo na roho mbaya.
Hii ni tofauti na wanawake Wanene. Ni nadra sana kumkuta Mwanamke mnene kuwa na gubu...
Habari za Sabato Wakuu!
Wiki nzima hii nilikuwa huku Mbweni, ninakijiplot changu. Sasa kwa hali niliyoikuta nimejikuta ninakata tamaa.
Aiseeh! Hawa majirani zangu sio Pouwa. Hii mijengo walioidondosha na wanaoidondosha sio Pouwa! Unaweza ukadhani upo kwenye filamu za kinaijeria.
Hapa...
Kwema Wakuu!
Kauli zinazotolewa na viongozi mbalimbali wakijitamba kuwa wao ni watoto wa mjini, wengine wakisema wamezaliwa Kariakoo, wengine, Ocean road, wengine mnazi mmoja, wengine Kinondoni basi ilimradi kila mmoja ajitutumue. Ndio ukweli huo. Kauli hiyo inamaana kubwa sana. Watoto wa...
Habari Wakuu!
Watibeli ni bora tufe lakini kamwe hatuwezi kuwafuata waganga au wachawi. Ushirikina na uchawi kwetu ni kama kosa la mauaji, au kosa la usaliti.
Binafsi siwezi ishi na mtu ambaye anapenda mambo ya kishirikina, anaenda kwa waganga, au anadalili za uchawi uchawi.
Mke akijihusisha...
Kwema Wakuu!
Nimekua nikisikia hizi kauli kwenye majukwaa ya kisiasa. Lakini moja ya viongozi wa juu niliowahi kuwasikia wakisema kauli hiyo ni pamoja na Spika mstaafu Mzee wetu Job Ndugai.
Sasa kila nikisikia au kusoma ujumbe wenye maana ya nchi kuuzwa ninajikuta ninamaswali.
Miongoni mwa...
Habari za Sikukuu ya Pasaka!
Moja ya dalili kubwa kuwa taifa fulani halina rasilimali Watu ni kwa kuangalia safu ya viongozi na watawala.
Ukiona Watu wanaoteuliwa ni walewale yanaitwa miaka nenda rudi Watu ni walewale basi sababu kubwa ya jambo hilo ni kuwa nchi Hiyo haina Rasilimali Watu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.