Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa lengo la kuwapatia Vitambulisho vya Taifa Manispaa ya Moshi.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)
TANGAZO KWA WANANCHI WOTE WAKAZI WA MANISPAA YA MOSHI
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, tunapenda kuwatangazia wananchi wote kuanza kwa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa lengo la kuwapatia vitambulisho vya Taifa
Zoezi hili linahusu wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ambao bado hawajasajiliwa
Kwa tangazo hili unaombwa kuwasiliana na Afisa Mtendaji wako wa KATA (WEO) au Mtendaji wako wa Mtaa (MEO) kwa maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa. Ratiba nzima ya namna zoezi hili litakavyoendeshwa inapatikana kwenye Mtaa wako
Ili kusajiliwa lazima kuwasilisha vielelezo vyenye kuthibitisha umri wako, makazi na urai. Vielelezo hivyo ni :-
1. Cheti cha Kuzaliwa
2. Hati ya kusafiria ya Tanzania (Passport)
3. Vyeti vya Elimu ya Msingi na Sekondari
4. Kadi ya kupiga kura
5. Leseni ya Udereva
6. Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN)
7. Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi
8. Kadi ya Bima ya Afya
9. Kadi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF, PPF, PSPF, GEPF N.K)
Kuwa na viambatanisho vingi zaidi ni kutambulika kwa haraka zaidi. Toa nakala(photocopy) ya viambata tajwa hapo juu na kuwasilisha wakati wa kusajiliwa
Kumbuka kuwa zoezi hili ni bure kwa Raia isipokuwa gharama za kutoa nakala (photocopy) ya viambatanisho vyako
Zipo faida nyingi za kuwa na Kitambulisho cha taifa, ni Kitambulisho pekee kitakachokutambua na kukutambulisha kama raia halali wa Tanzania, kukopesheka kirahisi katika mabenki na mifuko ya Fedha, kupata huduma mbalimbali kirahisi na kwa haraka zaidi, pamoja na faida nyingine nyingi. Jitokeze mapema usajiliwe na kupata kitambulisho chako.
Imetolewa na;-
Afisa Usajili Wilaya ya Moshi,
Ofisi - Mtaa Wa KDC, Mkabala Na Halmashauri Ya Wilaya Ya Moshi
S.L.P 580, Moshi-Kilimamnjaro
Simu 0766 600678