Zoezi la kufungia Simu ni kama lishafeli kabla halijaanza

Leo nilikua naangalia ITV asubuhi, cha kushangaza yule mmama wa TCRA alikuwa anasema ikiwa simu yako itafungiwa kwa bahati mbaya, basi nenda kwa subscriber wa mtandao wako, nao watakufungulia.

Nilijiuliza sana hili swala, hivi kweli subscriber ndio awe na mamlaka ya kufungia au kufunga simu feki, apa tutapona kweli?
Hawa subscriber si ndio wanauza simu pia?

Kwanini TCRA wasiwe na mtambo wao?

UFAFANUZI,
Kauli hiyo inahusu simu genuine zitakayofungiwa kwa bahati mbaya NA sio simu feki.
In fact, uzimaji wa simu feki uko pale pale!
 
Wanabodi bado saa chache simu zitafungwa ooohhh haya mambo ya kusikiliza maneno ya kufurahishana kwenye mitandao yatakugharimu hata kama si pesa lakini usumbufu. Mi nawaasa wanabodi wenzangu tuache ubishi. Nakumbuka tulianza na simu analog tulipoambiwa zinabadilishwa tukaponda sanaaaaa.... na kuona kuwa ni upuuzina usumbufu hivi leo nani ana simu ya analog! tunacho sahau teknologi inabadilika sana day in day out. Nakumbuka tulipo tangaziwa wenye vituo vya tv wazime mitambo ya analog kuja digitali ikawa issue kweli kweli!! mitambo imezimwa kila mtu na king'amuzi hutaki kalaga baho. Jamani tusiwalaumu TCRA teknologi inabadilika kwa sababu mbali mbali moja wapo mambo yapo kibiashara zaidi twendeni na wakati other wise tutakuwa kama bushman this is a e-world
Simu zitazimwa wewe hutakuwa na mawasiliano and watch out with advace world they can trace you!
 
Aka ka mchezo hakakuwahi kuniingiaa akilini,, ata sikuwah kujisumbuaa kuakiki,, mi na Sony yangu Lt 28h #at&t naenjoy
 
Kuna Sehem Nilisoma Kuwa Eti Watafunga Kwa Kuangalia Imei Ya Simu Yako Lakini Simu Za Android Zilizokuwa Rooted Unaweza Kubadilisha Make Ya Simu,model,,,na Wait For It,,,,,IMEI Ndio Unaweza Kubadili IMEI Ya Simu Yako Ya Android Najua Cz Katka Kuchokora Kwangu Htc One M8 Yangu Fake Nilibadili
Kama ulibadiri IMEI wanakula kichwa
 
Nyie msioamini kwamba zinafungwa endeleeni kujipa moyo kesho simu yako ikianza kusearch network bila mafanikio ndio utawapa shikamoo Tcra
 
Back
Top Bottom