LGE2024 Zitto: Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikishaonja madaraka ya kisiasa watakaofata kushughulikiwa ni CCM wenyewe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,384
3,876
Your browser is not able to display this video.

Akiwa kwenye mkutano na wananchi Kigoma, leo Novemba 29, 2024 Zitto ameongea mengi:

- Amewaonya CCM kuwa wanachofanya kwa sasa kitawageuka kama inavyotokea nchi nyingine.

- Ametolea mfano yanayoendelea Angola na Msumbiji kuwa Vyama tawala vilitegemea Vyombo vya Dola kubaki madarakani

- Ameonya kuruhusu Taifa kuendeshwa na Vyombo vya Dola badala ya Demokrasia iliyowekwa kikatiba

- Asema Chama cha Siasa ambacho kinashindwa kushawishi wananchi na kuishia kuegemea Dola, siku kinaondoka madarakani hakitajua. Na kudondoka kwake kutakuwa kwa mshindo mkubwa sana

- Ameongeza kuwa Vyombo viwili vya Dola vimeshaingizwa kwenye siasa (Polisi na Idara ya Usalama)

Namnukuu:

Nataka nimwambie mwenyekiti wa CCM Rais Samia, kama kuna kosa ambalo CCM wanafanya ni kusurrender siasa kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Vyombo vya Usalama vikishaonja madaraka ya kisiasa kama hivyo unavyofanya watakaofata kushughulikiwa ni CCM wenyewe, hivyo vyombo vitawaondoa CCM Madarakani.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Tunayoyaona ayantokea Angola, Mozambiki ni makosa ya FLELIMO na MPLA kusarenda kisiasa kwa vyombo vya dola ndio maana muda wote wangu wote nilivyokuwa mbunge katika jambo nililokuwa nalipigania kwa nguvu zangu zote ni kuiondoa Idara ya Usalama wa Taifa katika makucha ya CCM, nikawapigania mageuzi ya TISS kwasababu ni kosa kubwa sana kuiondoa nchi kwenye democracy na kuipeleka kwenye nchi inayoongozwa na vyombo vya dola.
 
Tumefika hapa tulipo kwasababu ya tunao wapa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data, tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo

Yaani taifa la chawa? Kwa zama hizi?, nisawa na kulazimishwa kufikiri wanavyotaka wao duuu

Jamii ya kanyaga twende jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi ambayo inasafishwa ubongo

A society that can be brainwashed

Baba na mwana wanaimba na kucheza, (seya tutoke wote)

Natamani kusoma kuhusu akili mnemba wapi naweza pata elimu hii
 
Hii Iko sahihi. Kuna kipindi hawa polisi wa vyeo vya chini na walimu wanasimamia uchaguzi huu watakuja kuwageuka CCM hasta watakapobaini kuwa wanatumika kama toilet paper. Na Iko wazi kuwa watumishi wa umma hawawapendi hawa CCM sema wanawaogopa tu.
 
Zitto mzee wa kuuma na kupuliza. Hakuna mwanasiasa ambaye simwelewi kama huyu. Huwezi kujua kama yuko upande wa serikali, huwezi kujua kama ni mpinzani, yaani ni kama popo. Anasemaje haya wakati yeye na Samia ni wamoja?
Hana tofauti na Mbowe
 
Zitto kabwe ameshiba kunde na maharage na kuna dalili kavimbiwa!
 
Mbowe angekuwa kama Zitto asingekaa rumande kwa miezi kadhaa kwa sababu za kusingiziwa. Umeshawahi kuona Zitto amekamatwa na kukaa ndani?
Na Tuzo akampa Samia mwanaCCM na ticket ya kuwania Urais akampa mwanaCCM Lowassa, na baada ya kutoka mahabusu moja kwa moja ikulu, na maridhiano akaya nga'ang'ania hapa kamzidi mpaka Zitto.
 
Zitto mzee wa kuuma na kupuliza. Hakuna mwanasiasa ambaye simwelewi kama huyu. Huwezi kujua kama yuko upande wa serikali, huwezi kujua kama ni mpinzani, yaani ni kama popo. Anasemaje haya wakati yeye na Samia ni wamoja?
Hunizidi mimi..
Kesho utasikia nimeongea na mh rais katuhakikishia uchaguzi huru na wa haki..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…