Zitto: Mbowe ni Kiongozi wangu, Tusameheane

Hapa patamu kuna watu walikuwa wanafuata upepo leo sijui wataficha wapi nyuso zao
 
  • Thanks
Reactions: nao
Zitto amuangukia mbowe akili nikiongozi wake mda wote, akiri alikosea.
 
Attachments

  • Screenshot_2016-02-03-16-52-18-1.png
    Screenshot_2016-02-03-16-52-18-1.png
    62.2 KB · Views: 23
Akileta zake tunamzingua tena kama kawa, sisi ndio CDM, tunaijua siasa vizuri sana. Hakuna mwanasiasa aliyefanya siasa kwa mafanikio makubwa katika nchi hii kama Mbowe. Jamaa ni genius. Zitto anajifanya mjanja lakini kwa Freeman amechemka. Kupatana kwao sio bure, lazima kuna kitu Mbowe anakitafuta, maana hafanyi siasa kihasara. Tuendelee kusubiri!!

Mbowe ashabadili gia angani...Lowasa sio plan yake tena 2020...Zito atarudi CHADEMA....Watch this kwa makini
 
"Mbowe siku zote amekuwa kiongozi wangu na siwezi kubeza nafasi yake ktk kujenga demokrasia nchini. Tulipishana. Tulikoseana. Tusamehane"....Zitto Zuberi Kabwe

Hayo ni maneno ya ZZK katika Account yake ya facebook
Ninahis kwa mwendo huu 2020 itabadilishwa gia angani na si ajab zzk akasimamishwa kukipiga na magu na kama sio 2020 bas 2025
 
Tatizo lilikua ni kikwete aliwalaghai sana wanasiasa wa upinzani kwa kuwapandikizia maugomvi yasiyokua na kichwa wala miguu, ili mradi tu ccm iendelee kutawala. Haya mapatano kama ni kweli na kila mtu anajua nini maana ya upinzani Dr slaa na lipumba nao waunganishe nguvu ikiwa bado asubuhi ili upinzani uongeze nguvu.
 
Ndipo akili yangu inanituma hapa zitto ndio mgombea wa chadema 2020

Na ndiye Mwenyekiti wa Chama ajaye...waligombanishwa tu hawa...hata zito aliwahi kusema wanagombanishwa...hope slaa pia atarudi kundini...Mtu mzima hua anakubali makosa...ndio uanaume huo...heko mbowe...heko Zitto
 
Wamuombe msamaha na Lowasa walivyokua wakimchafua over the years, kua ni FISADI kumbe mzee wa watu hana hata doa.
 
Soon na Dr Slaa naye atapatana na Mbowe, waliokuwa wakimwita kila aina ya majina mabaya sijui nao watapatana naye,yaelekea kuna watu huwa wanachukia watu wengine kwa kufuata mkumbo tu,lakini hata wao wenyewe hawajui kwanini wanamchukia mtu huyo,ni kwasababu wamemsikia mtu flani wanayemuabudu akimchukia mtu huyo.In the same way watarudisha upendo tena kiurahisi mno kwa huyo mtu bila hata wao wenyewe kujijua.They're simply acting like programmed robots.
Hiyo ni human nature mbona ,wewe ukisikia kuna jamaa anamzengea mkeo utampenda ???
 
Mbowe ashabadili gia angani...Lowasa sio plan yake tena 2020...Zito atarudi CHADEMA....Watch this kwa makini
kumbe ndio maana, siku za hivi karibuni ukimtazama Zito akiwa kwenye mazungumzo body language yake inatoa viashiria kwamba kuna tukio flani kubwa linakuja hata mavazi yake amebadili na namna anavyonyoa nywele anatengeneza personality flani hivi, kwanza ameanza kuvaa zile nguo kama alizokua akivaa nyerere za Chou en lai, kaunda suti yenye colar iliyokatwa round, na pia tazama anavyonyoa, he aims at something bigger, kama kawaida ya CCM naye ataambulia Vumbi, muda wake wa kuvuma bahati mbaya umeshapita, analazimisha naye ataingia kwenye historia ya kushindwa dhidi ya CCM, watch this space...
 
"Mbowe siku zote amekuwa kiongozi wangu na siwezi kubeza nafasi yake ktk kujenga demokrasia nchini. Tulipishana. Tulikoseana. Tusamehane"....Zitto Zuberi Kabwe

Hayo ni maneno ya ZZK katika Account yake ya facebook

Kama kauli yake hiyo ni dhati ya moyo wake nasema huo ndio uanamme na kukua ki-busara na hekima. Unafahamu ni kweli hawa watu wawili wamezaliwa kiuongozi na naweza kusema tu ni wapambe zaidi waliowavuruga hawa viongozi hadi kufikia hatua waliyokuwa wamefikia. Naweza kusema hawa wote wana uwezo mkubwa sana katika siasa za nchi hii. Mbowe una uvumilivu wa hali ya juu na kilichobaki ni kupeana mikono na kushirikiana kuikwamua hii nchi.Zitto nae nampongeza kwa uvumilivu pia kwani sikuwahi kuwasikia hawa viongozi wakirushiana matusi. Pia dr Slaa nae ana uwezo na ni kiongozi visionary ila mchumba wake kamkalia kooni mno kiasi hata shughuli na maamuzi mazito na ya siri kazini kwa Slaa mchumba nae anataka awe na maamuzi.
 
kumbe ndio maana, siku za hivi karibuni ukimtazama Zito akiwa kwenye mazungumzo body language yake inatoa viashiria kwamba kuna tukio flani kubwa linakuja hata mavazi yake amebadili na namna anavyonyoa nywele anatengeneza personality flani hivi, kwanza ameanza kuvaa zile nguo kama alizokua akivaa nyerere za Chou en lai, kaunda suti yenye colar iliyokatwa round, na pia tazama anavyonyoa, he aims at something bigger, kama kawaida ya CCM naye ataambulia Vumbi, muda wake wa kuvuma bahati mbaya umeshapita, analazimisha naye ataingia kwenye historia ya kushindwa dhidi ya CCM, watch this space...

My friend....with Combined effort.....Plus makosa mengi mtakayofanya ....Kumbuka Kuna kina Lowasa ,slaa and others who will come to join efforts......Miaka 10 ijayo lazima muachie

Kuna effort kubwa zinaenda kufanywa kuhusu katiba...na huo ndio mzizi wa fitna

So far...Ili kuitoa CCM tunahitaji mchango wa kila mtu..Haina haja ya Uadui usio na msingi...Hongera Mbowe
 
Back
Top Bottom