Zitto: Magazeti mawili yakaliwa kooni kuvujisha siri ya uhusika wa Muhongo kupandisha umeme

Kumbe ndio maana ndio maana sijawai kumwamini Muhongo .....

Wakala wa mafisadi tu yupo pale kama pazia.....

Fumueni hiyo Tanesco...

Time will tell ........
 
Ha ha ha ngoja tuone kama jamaa Muongo aa Muhongo kama atatumbuliwa.......ila kwa asili yake wala sishangai Majungu,fitina na unafiki kwa wenzake kutumbuliwa!!
 
Kuna sinema ilikuwa inachezwa ili kumngo'a Mramba. Sasa kwa vile lengo limitimia basi Muhungo ahakikishe bei ya umeme haipandi hadi baada ya uchaguzi ujao. Kinyume chake ni kuendeleza sinema. Mramba karibu kwenye ujasiriamali, wako wengi walifukuzwa wameishia kuwa wafanya biashara wakubwa hapa nchini. Watani zangu nawavulia kofia kwa kuchakarika.
 
Kichwa cha Waziri Muhongo kinatafutwa na baadhi ya wanasiasa kwa udi na uvumba.

Wizara ya Nishati na Madini na pia Wizara ya Fedha ni roho ya nchi lakini pia ni mawindo muhimu kwa mafisadi na wawekezaji uchwara.

Rais Magufuli akitetereka tu kwenye maamuzi atajikuta hata ndoto ya nchi ya viwanda inakuwa ndoto ya mchana.

Filimbi za wanasiasa zimekuwa ni nyingi lakini ukizichunguza utakuta chimbuko lake ni unafiki na ubinafsi.

Rais Kikwete alijaribu kuzisikiliza filimbi za wanasiasa na matokeo yake alibadilisha Mawaziri katika wizara hizi kitu ambacho kilizifanya kutokuwa stable.

Kwa sababu Wizara ni roho ya nchi, Afya ya nchi haiwezi kuwa nzuri kama kila mara Rais anabadilisha Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini.

Kwenye nchi za wenzetu walioendelea, wizara ambazo ni roho ya nchi, viongozi wake wakuu hawabadilishwi badilishwi kama inavyofanyika Tanzania. Kubadilisha badilisha viongozi wakuu kunaifanya wizara kutokuwa stable.

Muhongo ana mapungufu yake lakini vile vile ni muhimu kuangalia faida na umuhimu anaoleta kwa taifa kama Waziri wa Nishati na Madini.
 
Muhongo sijawahi kumuamini, toka enzi za escrow, akaja sakata la ufungwaji mita za mafuta kule bandari, mpaka kumsababishia maumivu yasiyoisha mama wa watu mbele ya majaliwa, leo Mramba kajaa kwenye 18 zake. Hakika nimtega mitego mzuri anaeweza kufaidika pande zote yani kama mtego ukitick atafaidika nao, na kama mtego ukibuma atafaidika nao pia.
 
Mkwere hii zambi utakuhukumu, kwa nini usiwache wanachama wakachagua
 
Sasa kama huwa mnajua kuna siri zinakuwepo.... Mnataka nini kujua kilichopo zaidi ya kumwamini prof apige kazi.... Anajaribu kuwaelesha bado hamuishi sababu... Wivu tu
 
Kichwa cha Waziri Muhongo kinatafutwa na baadhi ya wanasiasa kwa udi na uvumba.

Wizara ya Nishati na Madini ni roho ya nchi lakini pia ni mawindo muhimu kwa mafisadi na wawekezaji uchwara.

Rais Magufuli akitetereka tu kwenye maamuzi atajikuta hata ndoto ya nchi ya viwanda inakuwa ndoto ya mchana.

Filimbi za wanasiasa zimekuwa ni nyingi lakini ukizichunguza utakuta chimbuko lake ni unafiki na ubinafsi.
Mkuu, umeongea kweli tupu. Ila hoja hapa iliyoibuliwa ni kuwa Wizara haikua na taarifa ya mchakato, na hapo ndipo akili za watu makini ambao Taifa liligharimikia kuwasomesha na wakaelimika wanajaribu kutafakari kwamba ule mchakato ambao ulirushwa kwenye Tv tena kwa uwazi kweli haikuwa inajulikana level ya Wizara?
Maswali hayo ndiyo nadhan hizo media zimeingia chimbo na kuleta hayo machapisho.
 
Huyu Zito naye nadhani kavurugwa haelewi dili zake kama zitaendelea. Muhongo wamwache achape kazi:
Mzee wangu kijijini alinishangaza, Tanesco wanambembeleza alipe Tsh 27,000 aunganishwe umeme japo hakutaka, anatumia solar, nikampa amelipa kesho yake wakamfungia umeme.
Hapa Dsm kuna jamaa hapo Kitunda analipa tariff (sikumbuki inaitwaje) mwezi mzima analipa 17,000 (akitumia friji, tv, taa na pasi).
Muhongo tumsifie badala ya kumuudhi.
Umeme sasa ukikatika una uhakika utarudi shortly, mgawo ni historia.
Pigeni siasa tuachieni mashujaa wetu
 
Toka Muhongo amechukua wizara hiyo hali ya Umeme imekuwa nzuri kuliko wakati wowote tangu tupate uhuru. Aliwahi kuwekwa Simbachawene kwa miezi michache ilikuwa balaa. Ngeleja ndio usiseme. Muhongo amefuta biashara ya Majenereta na mmi nauza Jenereta miezi mitatu sasa hakuna wateja.

Ukimpima kiongozi based on results Muhongo is the best, ila kama mnataka wanasiasa wazuri mtoeni ila Mimi ameokoa biashara yangu iliyotaka kufa kwa kukosa umeme wa uhakika wa Tanesco
Mara unauza majenereta umekosa wateja, mara amedaidia biashara yako, mbona hueleweki?
 
Mkuu, umeongea kweli tupu. Ila hoja hapa iliyoibuliwa ni kuwa Wizara haikua na taarifa ya mchakato, na hapo ndipo akili za watu makini ambao Taifa liligharimikia kuwasomesha na wakaelimika wanajaribu kutafakari kwamba ule mchakato ambao ulirushwa kwenye Tv tena kwa uwazi kweli haikuwa inajulikana level ya Wizara?
Maswali hayo ndiyo nadhan hizo media zimeingia chimbo na kuleta hayo machapisho.

Mimi bado nitaendelea kuuliza hivi:-
kuna mchakato walisema utaletwa kwa wananchi........
kwenye taarifa nikasikia bei ya umeme imepanda sio neno jioni yake tena kanisani mkuu anasema hakuna kitu kama hicho
kilichonishanga kwanini hakuzuia toka mwanzo? Anadhani akija kwenye vyomba vya habari ndio ataonekana anawaonea wanyonge huruma???

Thubutu mnyonge ana kibatari chake cha mafuta ya taa hana habari na huo mnaoita umeme khaaaa
 
Toka Muhongo amechukua wizara hiyo hali ya Umeme imekuwa nzuri kuliko wakati wowote tangu tupate uhuru. Aliwahi kuwekwa Simbachawene kwa miezi michache ilikuwa balaa. Ngeleja ndio usiseme. Muhongo amefuta biashara ya Majenereta na mmi nauza Jenereta miezi mitatu sasa hakuna wateja.

Ukimpima kiongozi based on results Muhongo is the best, ila kama mnataka wanasiasa wazuri mtoeni ila Mimi ameokoa biashara yangu iliyotaka kufa kwa kukosa umeme wa uhakika wa Tanesco
Ha ha ha! Ameokoa Biashara yako ya majenerata.
 
Unajichanganya na wewe ni muongo, sasa kama hujauza majenerator miezi mitatu ameokoaje biashara yako? ukitaka kuwa muongo uwe na kumbukumbu - Pumb....fu
Unapata faida gani baada ya kumtukana mtu ambaye ninaamini humfahamu?

Kwa nini usimjibu kwa hoja tu.

Wewe ukitukanwa utafurahi?
 
Kaka Zitto bado hajamalizana na Prof Muhongo. Hebu muache Prof wetu afanye kazi. Mimi kibanda nilichojenga kijijini kwetu kimepata umeme wa TANESCO mwezi huu. Sikulitarajia hili katika uhai wangu.
 
Back
Top Bottom