Usichangie mada kabla hujasoma. Acha uvivu wa kusoma!Nasubiri walio elewa hapa waje waseme. Sioni kama zito ameongea point tofauti na povu tu
Wabunge walitoa Hoja Binafsi kuhusu Madawa ya kulevya ( Esther Bulaya na Faustine Ndugulile ) na kufuatia hoja hiyo Serikali ikaleta Muswada bungeni na Bunge likatunga Sheria ya Kupambana na Madawa ya kulevya mwaka 2015.
Serikali mpya ikaingia madarakani mwezi Novemba 2015. February 2017 Ndio Kamishna Mkuu anateuliwa tena baada ya wabunge kuhoji na kushinikiza kupitia Kamati husika na pia mbunge Esther Bulaya aliyetoa Hoja Binafsi katika Bunge la Kumi.
Rais anasema hakuwa anajua kuwa sheria hiyo ipo. Lakini Rais anapogawa Wizara huwa anatoa instruments na Hizo instruments hutaja kila sheria kwa kila Waziri. Ilikuwaje Rais akasahau sheria hii nyeti kama alikuwa na nia ya dhati ya Kupambana na Madawa ya kulevya?
Rais anaona Bunge kikwazo kwa sababu Bunge linamwongoza afuate sheria. Lakini Kama anaona Bunge linamkera turudi kwenye uchaguzi tu, alivunje.
Kuna mtu anadhani watu watahangaika na Waziri Mkuu. Why? Anajidanganya Sana.
PM ni mbunge mwenzetu. Hatuna shida naye.
Ukitaka kula chura kula aliyenona.
Sasa MABADILIKO waliyoyataka wananchi mungu anayaleta kwa njia zake alizochagua. Njia zinazokomaza Taasisi za nchi yetu.
Heshima kubwa kwa Wabunge wa Bunge la 4 kwa mabadiliko makubwa ya Katiba ya mwaka 1984.
Hii nchi sio Gangsters Republic. Hii nchi ya Nyerere hii ina misingi ya Haki na Utu. Hii ni United Republic of Tanzania.
Kutoka:
Haya ndio yatawafanya akina MsemajiUkweli wawe wanameza hedex kila siku wakibuni utetezi dhidi ya yanayoendelea. Ni aibu kubwa-uliona watu wazima walishikwa na butwaa mkuu alipokuwa akisisitiza watu kunyongwa wakati sheria yetu haisemi hivyo! Inasikitisha lakini acha kama ni Mungu alimleta atakuwa na kusudi lake ambalo sisi kwa akili zetu na macho ya nyama pengine hatuwezi kufahamu!Mkuu hayo ndio madhara ya kuwa mkali kupita kiasi hata kwa mambo yasiyohitaji ukali. Inafikia mahali unaoshirikiana nao wanaona unajua kila kitu hivyo waanacha utekeleze. Kwa ujumla watu wanahitaji kiongozi makini na baadhi ya sehemu uwe mkali na sio mara nyingi kuongozwa na jazba. Kumbuka ukifanya kazi na watu wazima sio watoto, kufoka sana hakuwezi kukufanya kuwa bora. Udhaifu ninaouna ni mkuu kukosa subira na sheria zisizokidhi tabia yake ya jazba, hivyo kujikuta anatoa sheria za mfukoni zinazokidhi matamanio yake. Kwa namna yake ya jazba ndio tuona wapi sheria zisizo kwenye vitabu vya sheria na kusikia sheria zinazoitwa amri toka juu zinapotoka. Niliposikia anasema mtu kama amehukumiwa kunyongwa acha anyongwe, je sheria zetu zinaruhusu kunyongwa kwa madawa ya kulevya? Kuna haja gani ya kuwa na balozi ambaye hawezi kutetea wananchi wake? Hata kama mtu amefanya makosa lakini ni lazima nchi yetu itumie njia za kidiplomasia kutetea mwananchi wake na kuja kumpa adhabu zinazoendana na taifa letu na sio adhabu za utashi wa rais. Kwa hapa ndio tunaona kwanini Mh. Lema yuko ndani mpaka leo.
Nyie endeleeni kumsifia huyo mtu muda ndio utawajibu.Nchi haiongozwi na matamko uchwara ya zito kabwe!
Mkuu hayo ndio madhara ya kuwa mkali kupita kiasi hata kwa mambo yasiyohitaji ukali. Inafikia mahali unaoshirikiana nao wanaona unajua kila kitu hivyo waanacha utekeleze. Kwa ujumla watu wanahitaji kiongozi makini na baadhi ya sehemu uwe mkali na sio mara nyingi kuongozwa na jazba. Kumbuka ukifanya kazi na watu wazima sio watoto, kufoka sana hakuwezi kukufanya kuwa bora. Udhaifu ninaouna ni mkuu kukosa subira na sheria zisizokidhi tabia yake ya jazba, hivyo kujikuta anatoa sheria za mfukoni zinazokidhi matamanio yake. Kwa namna yake ya jazba ndio tuona wapi sheria zisizo kwenye vitabu vya sheria na kusikia sheria zinazoitwa amri toka juu zinapotoka. Niliposikia anasema mtu kama amehukumiwa kunyongwa acha anyongwe, je sheria zetu zinaruhusu kunyongwa kwa madawa ya kulevya? Kuna haja gani ya kuwa na balozi ambaye hawezi kutetea wananchi wake? Hata kama mtu amefanya makosa lakini ni lazima nchi yetu itumie njia za kidiplomasia kutetea mwananchi wake na kuja kumpa adhabu zinazoendana na taifa letu na sio adhabu za utashi wa rais. Kwa hapa ndio tunaona kwanini Mh. Lema yuko ndani mpaka leo.