Zitto Kabwe tena katika issue ya ndege ya Boeing

Tumeibiwa...

I doubt kampuni kubwa kama Boing wanaweza kufanya ujinga wa kutu overcharge..

Hii ni sisi wenyewe ndio tumepiga.

Negotiations zote alifanya mwenyewe na Katibu Mkuu Hazina Dotto ambae ni mtoto wa Dada yake.Hakukuwa na mtaalam yeyote wa airline.

Tumeibiwa watanzania.
Tumshukuru Mungu amefanya mwenyewe (asiyefanya makosa), vinginevyo sasa hivi tungekuwa tunazungumzia 'msiba' wa mtu kutumbuliwa.
 
nafikiri kuna jambo ZZK amelinena "between the lines"

kama kweli tumepigwa na boeing basi hii ni kashfa kubwa kwa boeing na kuna uwezekano ikachafua reputation ya boeing

ila kama kuna ufisadi umefanywa basi boeing hawatakubali kuchafuliwa kizembe, they're definitely gonna do something about it
 
acha Uongo, website ya Boeing inaonyesha hiyo ni terrible teen. Kujua kama ni terrible teen huambiwi ila unaangalia specs za manufacturer then unaiclassify... Tuache ushabiki kwenye mambo muhimu na tusiishi kwa hisia kama tulivyozoea tukaja kupata hasara..
Kuna watu huwa hawataki kuhoji they belive every government statements
Kulikuwepo na Meli inayoitwa Mv Dar es salaam ilikuwa ifanye safari zake kati ya Dar Bagamoyo lkn majuzi wamekabidhiwa jeshi maana haifai kwa matumizi ya abiria
 
Dah, Bila Mange Kimambi tusingejua Hili...
Ukweli una nguvu sana aisee na ndio maana ukiutafuta blindly utaishia kuamini kuwa Mange asiyekuwa hata na Vitz hajui lolote kumlinganisha na 'prince bashi' anayeng'ara kwenye Lexus V8 na mlingoti wa bendera juu!
Na muda ulivyo na urafiki wa karibu na ukweli sio ajabu tukaja kushuhudia Mange mwenye vihereni kama matairi na vinywele vyake anatambulika kama shujaa wa taifa na mzalendo namba moja. Ngoja tusubiri maana mjadala ndio umeanza!
 
Naomba tusiweke siasa za uchama katika hili. Naamini tutamtetea sana mkuu kwa sababu tunataka kumtetea, lakini ikithibitika maneno ya Zitto ni ya kweli, tutainamisha vichwa chini kwa aibu. Binafsi nimemuelewa sana Zitto.
Ukweli ni kuwa tumeshspigwa cha juu na mkubwa na mwanae
 
kioo cha ndege yaani dirisha. hivyo vinawekewa oda jamani. kampuni haizalishi kila kitu. ila inaunda. kwa mfano. ni gari pekee mikanda ya madereva huonyesha mwaka halisi wa gari ilitengenezwa lini. vingine ni parts tu. na bado viti vinatoka ktk viwanda vingine. mf. samsung anatengeneza simu lakini betri inatoka china.
 
Ulishaona fisadi gani aliyeweza kushindwa kesi mahakamani? Utakuwa unajisumbua tu na kupoteza muda na pesa yako kumshitaki fisadi mahakamani maana hutamshinda.
shutuma dhid yake zinakujaje???
 
Kuna watu huwa hawataki kuhoji they belive every government statements
Kulikuwepo na Meli inayoitwa Mv Dar es salaam ilikuwa ifanye safari zake kati ya Dar Bagamoyo lkn majuzi wamekabidhiwa jeshi maana haifai kwa matumizi ya abiria

Ni ujinga kuendelea kuacha kuihoji serikali wakati serikali yenyewe ndio imetufundisha tuihoji kutokana na kufanya mambo ya hovyo na kuitia nchi hasara.. Mijitu mingine nafikiri hailipi kodi ndio maana haina uchungu na inaleta mzaha kwenye mambo ya muhimu..
 
ANAANDIKA ZITTO KABWE: SERIKALI INAFICHA JAMBO KUHUSU DREAMLINER 787-8

“Serikali inaficha jambo kuhusu Dreamliner 787-8, Tunaambiwa kwamba Ndege tunayonunua Boeing 787-8 Dreamliner Ndio kwanza inaundwa. Sio Kweli. Ndege hiyo iliundwa mwaka 2009 na kinachofanyika Sasa ni kubadilisha Injini yake Kwa sababu Injini za ndege hizo zilikuwa na matatizo ya kuwaka moto ( imetokea Kwa Ethiopian na Nippon Air ya Japan ). Hivi sasa kuna ushindani mkubwa kati ya Kampuni ya GE ya Marekani na Kampuni ya Rolls Royce Uingereza kuhusu nani apate biashara ya injini hiyo.
Hata hizi Bombardier tulizonunua hazikuundwa baada ya sisi kuweka order. Ndege hizi ziliundwa mwaka 2014 na zilikuwa tayari zimenunuliwa na Kampuni ya ndege ya Kazakhstan kabla ya baadaye kuuziwa sisi. Ushahidi wa hili ni rahisi Sana, ukipanda ATCL Bombardier tafadhali soma maandishi madogo dirishani utaona S/N 0001519017-040 DATE 10/2014. Hiyo 10/2014 ni Oktoba, 2014.

Serikali inaficha jambo katika suala la ununuzi wa Ndege hii ya Dreamliner. Serikali inajua kuwa imenunua Terrible Teen Kwa bei kubwa kuliko ilivyostahili. Shirika la ndege la Boeing linajua kuwa wametupiga bei ya kuruka na kutudanganyia Kwa kubadili injini. Serikali inajua kuwa haikusimamia maslahi ya Taifa katika mazungumzo kuhusu bei. Bahati mbaya Sana mazungumzo hayo yalimhusisha Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Fedha James Doto peke yao. Hapakuwa na Government Negotiation Team Kama ilivyo kawaida ya manunuzi makubwa ya namna haya.

Shirika la Boeing wametumia uzoefu wetu mdogo kutupiga na Ni wajibu wa Watanzania wote Kwa kutumia mahusiano yetu yote duniani kuwataka Boeing wawajibike kwa udanganyifu wao kwetu. Boeing wanapaswa kurudisha sehemu ya Fedha yetu. Ni aibu Kwa Kampuni kubwa Kama Boeing kuiibia Nchi masikini Kama Tanzania. Watanzania mnakumbuka sakata la Radar? Hii ni kurushwa zaidi ya radar. Hela zetu zirudi tujenge Reli au kuongeza Ndege.

Zitto Kabwe
3/5/2017
Mzee wa tuhuma
 
kama ndege aliyonunua Magu na Mwanae dotto ni boeing 787-8 LIN 20 hiyo ni terrible teens. hata ukidhikiri uchi haitabadili ukweli
Inaonekana hujui hata kwa nini ziliitwa terrible teens, kama unaelewa hilo unatakiwa ujue pia order yoyote juu ya 19 ya hiyo model si "terrible teen", vilevile Boeing ya Tz ni 787-8, no 719, sasa 719 hadi 19 ni ndege zaidi ya 700 zimeshanuliliwa, sasa sijui unacholazimisha hapa ni nini.
 
acha Uongo, website ya Boeing inaonyesha hiyo ni terrible teen. Kujua kama ni terrible teen huambiwi ila unaangalia specs za manufacturer then unaiclassify... Tuache ushabiki kwenye mambo muhimu na tusiishi kwa hisia kama tulivyozoea tukaja kupata hasara..
Screenshot hiyo website, usipende kuchukua maneno ya kuambiwa.
 
Back
Top Bottom