Zitto Kabwe awasili Polisi Dar kuhojiwa, aachiwa Kwa dhamana

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe awasili Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kuhojiwa.

=>Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe amewasili katika kituo kikuu cha kati cha Polisi jijini Dar,tayari ameshakutana na ZCO Camilius Wambura akiwa na RCO wa Temeke pamoja na Naibu ZCO Kwa mahojiano.

=>Ameambatana na Wanasheria wake.

=>Ameitwa polisi kuhojiwa kuhusu hotuba aliyoitoa Mbagala katika Mkutano wa 'Linda Demokrasia' Uliofanywa na Chama cha ACT Wazalendo.

=>Zitto Kabwe amaliza Mahojiano, Aachiliwa kwa dhamana na kuambiwa arudi tarehe 15.

Amehojiwa kuhusu:

=>Maombi ya ACT wazalendo Polisi ya mkutano ilikuwa 'kujenga chama' lakini ACT ilizindua operesheni linda demokrasia.

=>Kumgombanisha Rais na wananchi kwa kusema yeye anajifanya Rais wa masikini na hivyo kumgombanisha na wasio masikini.

=>Kusema Rais ameropoka kuhusu sakata la sukari.

=>Kumchonganisha Rais na wananchi kuhusu suala la vilaza.

=>Kumwita Rais dikteta na kwamba anaendesha nchi kwa imla. Yote hayo chini ya kufungu 89(1)(a) cha Penal Code" kutumia maneno ya matusi yenye kuweza kuvunja Amani ( abusive language ).

Zitto Kabwe akiongea na Waandishi wa habari baada ya Mahojiano.


Masuala Muhimu....

Masuala Matano Muhimu yaliyoibuka Wakati wa Mahojiano ya Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe na Polisi, Leo Jijini Dar es salaam.

• Maombi ya Chama Cha ACT Wazalendo ya mkutano ilikuwa 'Kujenga Chama' Lakini Chama Kilizindua "Operesheni Linda Demokrasia" (Operesheni ambayo Ni Sehemu ya Ujenzi wa Chama, Maana Kama Demokrasia ikiachwa iteketezwe Na Serikali ya Rais Magufuli, bila Kulindwa, Basi hata Uwepo wa Vyama Vingi Utakuwa Mashakani).

• Kusema "Rais Ameropoka kuhusu Sakata la Sukari Nchini" (Kwa kuelezea Namna alivyoueleza Umma akiwa Babati Kuwa Kuna Sukari imefichwa Na kukamatwa Mbagala, Taarifa ambazo TRA na Takukuru walizikanusha na Kusema Sukari Husika haikuwa imefichwa).

• Kumchonganisha Rais na Wananchi kuhusu suala la kuwaita Vijana wa Kitanzania Kuwa ni "Vilaza" (Kwa Kumnukuu Rais Mwenyewe alipowakashifu Vijana hao Wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam).

•Kumgombanisha Rais na Wananchi kwa Kusema "Yeye anajifanya Rais wa Masikini (Huku akiwakashifu hao Watoto wa Masikini Kwa Kuwaita "Vilaza") na hivyo kumgombanisha na wasio Masikini" (Pamoja Na Kunukuu Kuwa Kauli ya Kuwa Yeye Ni Rais wa Masikini ameitoa Mwenyewe Rais).

• Kumwita Rais Dikteta na Kwamba anaendesha Nchi Kiimla (Pamoja Na Kutoa Mifano ya Udikteta wake Kama Kulipangia Uongozi Bunge, Serikali yake Kuondoa Bunge Live, Kuwafukuza Bungeni Wabunge wanaotimiza Wajibu wao wa Kuihoji Serikali na Kudhoofisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali Nchini, CAG Kwa Kuiondolea Kiwango Cha Bajeti iliyopangiwa kinyume Na Sheria).

Maelezo ya Jeshi la Polisi ni Kuwa yote hayo yanaangukia kwenye Kifungu Cha 89(1)(a) cha Penal Code, Yaani "Kutumia Maneno ya Matusi yenye Kuweza Kuvunja Amani" (Abusive Language).

Jeshi la Polisi limemtaka Ndugu Zitto afike Tena Kituoni Hapo Juni 15, 2016 Kwaajili ya Mahojiano zaidi.

Mwanasheria wa Ndugu Zitto ameliomba Jeshi la Polisi kupeleka Mashtaka Mahakamani Juu ya Suala Husika, Na Kwamba Ndugu Zitto atakwenda Kuthibitisha Ukweli Na Undani wa Masuala hayo Mahakamani.
 
Tunasubiri kusikia majibu maan siku hizi kumkosoa JPM ni kosa la jinai! Anataka atawale nchi kidikteta haswa hataki kukosolewa wala kushauriwa! Yote anayajua yeye! Ingawa next door hapo Kenya rafiki yake anazunguka kila siku kwenye maandamano hajifunzi hata hilo dogo tu!?
 
ITAKUWA NI HABARI HII NADHANI ALIYOMUIAIBISHA MAGUFULI
U.S. Embassy Tanzania
18 hrs ·

The Ambassador of the United States to Tanzania Mark Childress was pleased to meet yesterday with the President of the United Republic of Tanzania Dr. John Pombe Magufuli to discuss the full range of bilateral issues and the strong partnership between the two countries. They discussed plans to sign a strategic assistance agreement between the Government of Tanzania and the United States Agency for International Development (USAID). Under the agreement, which aligns both countries’ roles and responsibilities with USAID’s five-year Country Development Cooperation Strategy ( https://goo.gl/fUVlKi ), USAID will continue to invest more than $400 million annually in health, agriculture, natural resource management, education, energy, and good governance in Tanzania. This USAID program is part of the previously committed $800 million in ongoing assistance that the United States spends annually on development and other bilateral programs in Tanzania across the full range of sectors to improve health and education, promote broad-based economic growth, and advance regional security.
 
Kituo Kikuu cha Kati ... Huu uandishi sio. Neno Central kwa muktadha uliopo kwenye "Central Police Station" maana yake ni "Kikuu" na sio "cha Kati"; hakuna "Kituo cha Kati cha Polisi" bali "Kituo Kikuu cha Polisi". Maneno yasitafsiriwe kulingana na mipaka ya uelewa wetu (centre = kati) bali kwa context.

Benki Kuu ya Kenya ambayo pia hujulikana kama Central Bank of Kenya - CBK haina maana kwamba ni "Benki ya Kati Kenya"! Au haina maana kwamba Bank of Tanzania (BoT) kwa kuwa haina neno "central" au neno lingine la moja kwa moja la Kiingereza linalo maanisha "kuu" basi haipaswi kutafsiriwa kama Benki Kuu ya Tanzania!
 
...kijana alikuwa safi sana baada ya uchaguzi ila sijui kitu gani kinamsibu, maana ZZK amekuwa mlopokaji kweli kweli akidhani anavuna wanachama kumbe anaua chama, acha chama chake kife, labda atarudi CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…