Zitto Kabwe aiponda bajeti, asema Tanzania itaanguka vibaya sana kiuchumi haijawahi tokea

Mkuu mi sidhani kama tutarudia hali iliyokua 80s ila inaweza ikawa worse au vice versa., if you are wise ungetambua hata huu mfumuko wa bei hasa za bidhaa za chakula, kushuka kwa shilingi yetu kila siku, na hali halisi ya taasisi zetu za fedha kama mabenki kungekualarm., ukumbuke kua kudidimia kwa uchumi sio an overnight process .. kuna stages zake na kwa kuangalia nyanja muhimu za uchumi wetu lazima utatambua dalili sio nzuri sana, kwa hio ili kuondoa tishio hili budget ya mwaka huu ilipaswa kuja na solutions

Hujui hata unachoandika ni kitu gani. Eti unasema, inaweza kuwa worse or vice versa. Hapo tu, mbobezi wa masuala ya uchumi atang'amua kwa sababu hulipi kodi kwa kupost hapa JF, ndiyo maana umeamua kuandika huo utumbo. Umesoma vizuri bajeti iliyowasilishwa jana? umesoma financial indicators katika mabenki yetu? mfumuko wa bei upo kiasi gani sasa? single digit. Siyo? Hivi unajua nchi hii mfumuko wa bei uliwahi kufika 30% mwanzoni mwa miaka ya 90s. Leo upo chini ya aslimia 6% wewe unaandika utumbo wako hapa. Jaribu kutumia hekma na busara. Acha kuleta stori za vijiweni, kwenye migahawa na wanywa viroba.
 
Mkuu Bufa sio kupinga kila kitu.
Ni kuweka wazi madhaifu na kuonyesha njia mbadala. Tatizo ni kuwa tumepokea demokrasia ya upinzani wa kisiasa nusu nusu lakini pia hatujaukubali ustaarabu unaoambatana na hizi siasa. Wanasiasa wetu wanaigiza vituko na vioja vya
wenzao wa Kenya, UK n.k na kudhani kuwa hiyo ndiyo demokrasia.
 
we

well said mkuu, zipi hatua tulizozifanya kama serikali mapaka zinapelekea tumeshindwa kupanga uchumi wetu?

Mkuu kwanza ukweli budget bado haijibbu maswali ya msingi, tunawaondoaje masikini 12million wasiendelee kuwa masikini zaidi?

Je masikini hawa wapo wapi kama ni vijijini kwa budget hizi tunawafikia walengwa?, Je tunaimarisha majiji, manispaa na halmashauri kuwafiki? Je sera zetu zinaongeza ama zinawapunguzia machungu?

tupo obsessed zaidi ni economic growth na sio economic Development
 
Mkuu kwenye hii bajeti hakuna zuri ni madudu tu. Huu mwaka wa fedha unaokwisha ambao bajeti yake ilikuwa ni 29 trillions pesa iliyotolewa ni 34% tu. Hivyo hii bajeti ya 2017/2018 ambayo ni 31.6 trillions tayari karibu 10 trillions ni kulipia deni la Taifa na hivyo huu uhuni wa kutoa bajeti pungufu utaendelea kwa kasi ya kutisha. Nakubaliana na Zitto kwamba huu mwaka wa fedha unaokuja hali ya kiuchumi itakuwa mbaya sana kama hakutakuwa na hatua madhubuti za kuimarisha hali ya uchumi nchini. Tusishangae kabisa kusikia Serikali kuanza mchakato wa kupunguza Wafanyakazi wa Serikali kwa idadi kubwa ili kuendelea na zoezi lao la "kubana matumizi"

Kazi ya upinzani ni kupinga. Wakianza kukubali mambo ya serikali watakua wamesahau wajibu wao wa kupinga kila kitu. Upinzani inabidi wapinge lolote lile la serikali either zuri au baya ila waendelee kuwa wapinzani
 
kinya09062017.jpg
 
Hizi Bajeti huwa hazitimiliziki miaka nenda miaka rudi bajeti ya kwanza ya magu hata 40 % haijafikisha sijui hiiya pili
 
Hujui hata unachoandika ni kitu gani. Eti unasema, inaweza kuwa worse or vice versa. Hapo tu, mbobezi wa masuala ya uchumi atang'amua kwa sababu hulipi kodi kwa kupost hapa JF, ndiyo maana umeamua kuandika huo utumbo. Umesoma vizuri bajeti iliyowasilishwa jana? umesoma financial indicators katika mabenki yetu? mfumuko wa bei upo kiasi gani sasa? single digit. Siyo? Hivi unajua nchi hii mfumuko wa bei uliwahi kufika 30% mwanzoni mwa miaka ya 90s. Leo upo chini ya aslimia 6% wewe unaandika utumbo wako hapa. Jaribu kutumia hekma na busara. Acha kuleta stori za vijiweni, kwenye migahawa na wanywa viroba.
Ha ha mkuu sikujua utapanic kiasi hiko, kunywa maji kwanza utulie otherwise wewe hapa ndio kielelezo kizuri cha wanywa viroba., wala hatugombani hapa., turudi kwenye uhalisia achana na mambo ya wanasiasa hao ni watu kama wewe tu., angalia hali halisi iliyopo nchini hivi sasa hizi report za akina IMF na ndugu zake zilizosomwa jana bungeni zinaendana na hali halisi iliyopo hivi sasa? learn to be a free thinker Mkuu
 
Kama wabunge walifuraia kushikwa kwa mchanga,na kusahau kuwa dhahabu bado inasafirishwa,wataacha kufuraia kufutwa kwa kodi ya roadlicens,na kuongeza kodi kwenye mafuta kweli?

Siyo hilo tu na waliosababisha wizi ndiyo wateuliwa wenyewe
 
Hujui hata unachoandika ni kitu gani. Eti unasema, inaweza kuwa worse or vice versa. Hapo tu, mbobezi wa masuala ya uchumi atang'amua kwa sababu hulipi kodi kwa kupost hapa JF, ndiyo maana umeamua kuandika huo utumbo. Umesoma vizuri bajeti iliyowasilishwa jana? umesoma financial indicators katika mabenki yetu? mfumuko wa bei upo kiasi gani sasa? single digit. Siyo? Hivi unajua nchi hii mfumuko wa bei uliwahi kufika 30% mwanzoni mwa miaka ya 90s. Leo upo chini ya aslimia 6% wewe unaandika utumbo wako hapa. Jaribu kutumia hekma na busara. Acha kuleta stori za vijiweni, kwenye migahawa na wanywa viroba.
Preach!
 
Back
Top Bottom