Zitto: Iundwe Serikali ya mpito ya watalaamu (Technocratic Government) kama suluhu Zanzibar

Uchaguzi ukirudiwa au ukiunda serikal sijui ya wafanyakazi vyote havina maana kwa upande wa upinzani, hii ni kwasababu lengo la uchaguzi kurudiwa ni ili mgombea wa CCM atangazwe kuwa mshindi! ikiundwa serikal yoyote na rais, basi kiuhalisia CCM itakuwa bado iko madalakani!.
msimamo wa chama fulani kuona kwamba kitaongoza milele usipobadilika, iwe bara au Zanzibar tujue tutachelewa kuingia kwenye vurugu lkn vurugu iko mbele yetu. Namkubari sana Gudlack wa Nigeria kukubari kushindwa akiwa kiongozi wa nchi kwa muhula 1. surely he is a man to learn from.
Mkuu mawazo yako ni sahihi unadhani nini kifanyike ili kubadilisha mtazamo huu kwa chama kinachodhani kina haki ya kutawala milele?
 
wachaga wakiskia zitto hata awe ametoa hoja au wazo zuri kiasi gani daima atatukanwa,kumuelewa mh zitto kunahitaji mtu makini na sio mtumia viroba,kuna watu humu ndani wanatamani vita itokee zanzibar hata leo kwa akili zao finyu.
 
Zitto amefilisika kabisa kisiasa kama hayo ndo mawazo yake.
Uchaguzi uliofanyika Zanzibar ulishuhudiwa na vyombo mbali mbali na kuthibitishwa kuwa ulikuwa huru na haki,
kwanini matokeo yafutwe?Zitto bora akae kimya
 
kweli wengine wanatumia matope badala ya akili..
Suluhisho la Zanzibar sio serikali ya mpito..
tatizo la Zanzibar ni CCM kukataa kung'atuka..suluhisho ni kua waungwana wakakubali matokeo..
muafaka gani hapo unatafuta zaidi ya alieshindwa kukaa pembeni..
Kama wamekaa vikao zaidi ya 8 wamekosa mwafaka,unadhani wataupata kwa serikali ya mpito ?
na kama lengo ni kuitisha uchaguzi mwengine hapo ni kujiandaa kuwa na serikali za mpito zisizokua na kikomo kila baada ya chaguzi..
Utakua mchezo wa kitoto mtu akila mweleka anasema uchaguzi ufutwe twende kwenye mpito..
lol !
WASOMI WA MAKARATASI NAO..
 
Zitto amefilisika kabisa kisiasa kama hayo ndo mawazo yake.
Uchaguzi uliofanyika Zanzibar ulishuhudiwa na vyombo mbali mbali na kuthibitishwa kuwa ulikuwa huru na haki,
kwanini matokeo yafutwe?Zitto bora akae kimya
 
Mkuu mawazo yako ni sahihi unadhani nini kifanyike ili kubadilisha mtazamo huu kwa chama kinachodhani kina haki ya kutawala milele?
Mtu au chama kukubari kushindwa ni uzalendo usio wa kawaida! Ifikie sehem CCM wajue kwamba mambo yanabadilika. Angalia mambo yanayoendelea kwa chaguzi mbali mbali za mayor! tatizo chama fulani kinaona chenyewe ndo kinafaa kuongoza tu! Nchi kama Burundi na Rwanda kuna kabira amalo hallijisikii kuongozwa ikitokea limeongozwa na mtu wa kabira lingine inaonekana kwamba limedharirika, angalia migogoro yao! mtazamo huu ni mbaya sana. mtu au chama kijipime au kijistahilishe kwa kuweza kukidhi mahitaji na matakwa ya raia wake. vinginevyo tunausogeze mgogoro mbele lakini lazima tutaupitia.
 
hao raia mwema wamekosa kuhoji magwiji wa siasa wanakakimbilia hako kakinda kanachowaza kupata umaarufu siasa za zanzibar tuwaachie wenyewe
 
Nafikiri suluhisho la kudumu la Z'bar ni kwa Serikali ya Tanganyika hususani kile chama kinachofikiri chenyewe ndicho kilichoumbiwa kutawala kiache ubabaishaji,kukubali Nimeshindwa maisha yandelee.Mie kwa kweli kabisa sioni mgogoro Bali mgogoro ukioyengenezwa na kuasisiwa na CCM Bara.Z'bar wanatume yao ambayo kwa kiasi ni huru kuliko hii ya kwetu ambayo Magogoni ndiyo yenye remote.

CCM watawala na wanachama wao wanatakiwa kupewa shule ya uraia kwamba watanzania na wazanzibar wote ni sawa na wanahaki ya kutawala Zanzibar. Hekima na busara ya Shein ndicho tatizo maana hana Busara wala hekima.

Tatizo ni Shein kung'ang'ania madaraka.Hana tofauti na Nkuruzinza.Na hakuna mwenye moral ndani ya CCM kwenda kutatua matatizo nchi nyingine.Ni unafiki uliopitiliza
 
Huo ushauri Wa Zitto ni wa CCM.Kura zipo,zihesabiwe upya na mshindi atangazwe bila delay techniques zozote

Sioni hata sababu ya kuhesabu kura.Kila mgombea alikuwa na wakala wake.Na kila mgombea Ana majibu yake.Kwa uhakika kabisa Shein anajua ameshindwa na anajua haitakaa itokee CCM ishinde Z'bar labda kutumia polisi.Na hapo wameiba kura mpaka basina bado wakashindwa.
Jamani CCM haijawahi kushinda Z'bar hilo wanalijua.

Ila wakituambia sababu ni Uasili wa Maalim Seif tunaweza kuelewa.Maana walitutangazia Umma kwamba Machotara wakatafute pa kuishi na kutawala kwani Z'bar
 
Mh.zito unasema hiyo serekali ijae madarakani kwa miaka mitani .na kazi yake iwe ni kutafuta suluhisho la kudumu .shughuli za maendeleobya wananchi zirafanywa na nani?
Mgawanyo wa madaraka katika ngazi za chini kama Ma DC ,RC makatibu kata makatibu wakuu na viongozi wengine itakuaje?
Wanzibari wanataka maendeleo ya kiuchumi kwa haraka sana .na wala sio vikao vya muafaka hili hukulitilia maanani kabisa.
Kuhusu kuachiliaba madaraka kwa 2.5years hujueleza ni kwa post ipi ? Ni raisi tu au whole gervenment? Pia katika hiyo serekali ya mpito hukueleza kuhusu baraza la mawaziri watatoka wapi?
Lakini mwisho katika ile ya kuwachiana 2.5years atakae kuwa wa mwisho ndie atakae chagua mwenyekiti wa tume ya uchafuzi,au itakuwaje?
 
Mimi nafikiri act wamejaribu kutoa suluhisho lisiloegemea upande wowote kuwabeza ni chuki za wana cdm kwa zito
Cuf wanataka matokeo yatangazwe ccm wanataka uchaguzi urudiwe ktk mzingira kama hayo ukitaka kusuluhisha lazima kila mmoja akubali kupoteza kile anachodhani ndio maslahi yake,ili kuanza upya.

Hicho ndicho walichofanya act.
Mbona wanasiasa wetu hawataki kuwa wa wazi kwamba uchaguzi ulifutwa kisheria au ni kwa sababu tu ccm ilishindwa ?jecha hana kaki ya kufuta uchaguzi bila ya vikao halali vya tume.ivi kana ccm ingeshindabkwenyevuchaguzi ule cuf ingesikilizwa malalamiko yake .manafiji wakubwa nyinyi mnataja amani bila ya haki .
 
Hiyo serikali ya wataalam anayopendekeza huyu bwana kama itakuwa ya mpito itakaa kwa muda gani? Baada ya muda huo wa mpito what next? Serikali za mpito maana yake ni caretaker institutions ambazo zipo pale kutengeneza mazingira ya uchaguzi kufanyika ; sasa huo muda wa uchaguzi utakapofika na matokeo yakawa kama yalivyo sasa tutafanyaje? Wazanzibari wameamua kwa sanduku la kura kuwa hawaitaki ccm na wao ccm hawataki kuachia ngazi hata pale wenziwao wanaposema kuwa wataheshimu katiba yao na kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa!!! Mpaka hapo nadhani kuna umuhimu wa kuchukua uamuzi mgumu!!!!!
 
Wengi mnajibu kwa chuki juu ya zitto as individual na si hoja zake......all in all ametoa pendekezo la kutafuta muafaka wa kudumu Zanzibar kwa kuwahusisha wazanzibar wote na si wanasiasa pekee.....kuna watu wanafikiri matatizo ya Zanzibar ni uchaguzi pekee....kiukweli kuna chuki kubwa baina ya waunguja na wapemba....

Tunasubiri hoja mbadala na hii na si kusema tu mshindi atangazwe ilhal tunajua kuna kundi lingine linakata......na haya aliyosema zitto na ACT ni mapendekezo kwa mujibu wa maono na busara zao.......
 
Suluhu yoyote iliyo nje ya katiba ya Zanzibar na Sheria zake ni bad precedent. Ni ajabu sana ZZK kuacha kupigia kelele uvunjwaji wa sheria za uchaguzi wa Zanzibar na badala yake kutoa pendekezo lililokinyume cha katiba na sheria za Zanzibar.
Alichokifanya ZZK ni kuappease the oppressors, na ukifanya hivyo ni kitu gani kitakufanya usiwappease miaka 20 ijayo wakifanya mchezo huohuo?
Dawa ya Zanzibar ni HAKI na Kuzingatia Sheria za nchi.
ZZK yuko wrong katika hili
 
Suluhu yoyote iliyo nje ya katiba ya Zanzibar na Sheria zake ni bad precedent. Ni ajabu sana ZZK kuacha kupigia kelele uvunjwaji wa sheria za uchaguzi wa Zanzibar na badala yake kutoa pendekezo lililokinyume cha katiba na sheria za Zanzibar.
Alichokifanya ZZK ni kuappease the oppressors, na ukifanya hivyo ni kitu gani kitakufanya usiwappease miaka 20 ijayo wakifanya mchezo huohuo?
Dawa ya Zanzibar ni HAKI na Kuzingatia Sheria za nchi.
ZZK yuko wrong katika hili
Hiyo haki itatendekaje na utafanyaje ili pande hizo mbili ziridhiane? Maana unamshtumu tu zitto lakini hutaji ni njia gani zitumike ili hayo uyasemayo yatokee.....kumbuka ccm nao wanalalama seif alivunja katiba kwa kujitangaza mshindi wakati hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.......sasa kwa mkuktadha huu utafanikishaje wadai haki hawa wote waridhiane huku kila mmoja akisema amedhulumiwa?
 
Hiyo haki itatendekaje na utafanyaje ili pande hizo mbili ziridhiane? Maana unamshtumu tu zitto lakini hutaji ni njia gani zitumike ili hayo uyasemayo yatokee.....kumbuka ccm nao wanalalama seif alivunja katiba kwa kujitangaza mshindi wakati hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.......sasa kwa mkuktadha huu utafanikishaje wadai haki hawa wote waridhiane huku kila mmoja akisema amedhulumiwa?

Suala si kumridhisha mtu, suala ni kusimamia katiba na sheria za nchi, kama Seif alivunja sheria basi ashitakiwe.

Pia ZEC itangaze matokeo kwa sababu Jecha hana mamlaka ya kuyafuta

Kinyume na hiyo Wapinzani waendeleze harakati za Kupinga udhalimu huu kupitia non violence means
 
Nishawahi kuwambia washikaji mahali fulani kuwa Zitto Kabwe sio mpinzani wa kweli,ni mtu anayefanya siasa fulani ya kisanii ambayo ina manufaa kwake mwenyewe na ccm yake. Hivi katika hali ya kawada unaweza kuja na wazo lakuunda sijui serikali ya wataalum sijui kutoka wapi wakati jambo liko wazi kabisa kuwa cuf wameshinda lkn hawataki kuwatangaza kuwa washindi. Kwanini asiwashauri ccm wakubali kukabidhi madaraka kwa mshindi halali? Hivi kweli kama yeye ni mpizani wa kweli kwanini aguswi na uporaji wa wazi unaofanywa na ccm dhidi ya upinzani? Pia anasema kuwa tume haina uwezo wa kufuta matokro ya wawakilishi waliotazwa kisheria. Swali linazuka tena, hao wawakilishi wamepatikana kwa uchaguzi upi? Zitto amedhihirisha kuwa ni kada wa ccm ama ni kilaza kama walivyo vilaza wakawaida. Nyumbafu zake sura kama mamba
 
RAIS John Magufuli ameshauriwa kuchukua uamuzi mgumu wenye kuibua muafaka wa kudumu kwa mgogoro wa kisiasa Zanzibar, bila kujali uamuzi huo utawafurahisha wengi ama la, uamuzi utakaohusisha kusimamisha Katiba ya Zanzibar na kuunda serikali ya mpito.

Akizungumza na Raia Mwema baada ya mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kutoa maelezo ya kina kuhusu mazungumzo yanayoendelea baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar, Jumatatu wiki hii jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema suluhisho la mgogoro huo ni kuunda serikali ya mpito ya watalaamu (Technocratic Government) ambayo itafanya kazi ya kutafuta muafaka wa kijamii kwa watu wa Zanzibar na kuandaa uchaguzi.

Alisema kuwa kwa hali ilivyo sasa haoni ni kwa namna gani CCM watakubali matokeo wa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana yatangazwe na pia hawaoni CUF wakikubali kuingia katika uchaguzi wa marudio.

“Kwa maoni yangu iundwe serikali ya mpito ambayo haitahusisha wanasiasa na ifanye kazi ya kuleta mabadiliko ya Katiba, kuunda Tume huru ya Uchaguzi, iongozwe na wataalamu wasiofungamana na vyama vya siasa ili mchakato wa kuleta maridhiano ya kijamii na kutibu makovu yote tangu Mapinduzi ya mwaka 1964,” alishauri Zitto.

Alieleza kwamba maafikiano ya kisiasa ambayo yamekuwa yikifikiwa katika visiwa hivyo yamekuwa yakihusisha wanasiasa ndiyo maana hakuna suluhisho la kudumu, na kwamba kazi ya serikali hiyo ya mpito ambayo anashauri iwepo madarakani kwa kipindi cha miaka mitano, mpaka 2020, iwe ni kutafuta muafaka wa kijamii.

Kuhusu namna ya kuunda serikali hiyo alisema; “Katiba ya Zanzibar isimamishwe pande zote zihusishwe katika uamuzi huo, na kwa kuwa wabunge wa Zanzibar wa Bunge la Jamhuri ya Muugano walitangazwa, pale ambapo mambo ya kisheria yanapotakiwa kufanyika katika serikali hiyo ya mpito, wabunge hao wanakaa kama Baraza la Wawakilishi,” alisema na kuongeza; “Hatuna namna, ni lazima tufanye maamuzi magumu sana kuhusu Zanzibar ili tupate suluhisho la kudumu.”

Kuhusu majukumu ya msingi ya serikali hiyo ya mpito, alisema itakuwa ni kufanya uchambuzi wa kina kuhusu matatizo ya Zanzibar, na kuunganisha jamii ya Wazanzibari ambapo wataalamu hao kwa kusaidiana na mabaraza ya wazee, yatakayoundwa na serikali hiyo, waendeshe marekebisho ya jamii ya Wazanzibari bila kuruhusu vyama vya siasa kuwa na mkono wake.

Amtwisha mzigo Rais Magufuli

Katika kuhakikisha kwamba serikali hiyo inaundwa, Zitto, ametoa wito kwa Rais John Magufuli, kusimamia mchakato wa kuiunda na akifanya hivyo kwa nia njema ataweza kuumaliza kabisa mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

“Rais Magufuli ndiyo Mkuu wa Nchi, kwa mazingira ya dharura ndiye peke yake anaweza kuisimamisha Katiba ya Zanzibar, mamlaka haya hayako kwa mtu mwingine,” alisema.
Alifafanua kuwa Rais anayo nafasi kubwa kuingilia kati na kumaliza mgogoro huo kwa kuwa pande zote zinazosigana katika mgogoro huo bado zina imani naye.


Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari aliyoitoa juzi, Maalim Seif alisema kwa hali ilipofikia, inabidi Rais Magufuli aongoze juhudi za kuleta muafaka katika mgogoro huo.
“Rais alipozugumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na mimi Ikulu, Dar es Salaam, alisisitiza haja ya kukamilisha mazungumzo kwa kulipatia ufumbuzi wa haraka, tunaona wakati umefika yeye mwenyewe aongoze juhudi zenye lengo la kufanikisha hatua zilizopendekezwa (na CUF),” alisema Maalim Seif.


Baadhi ya hatua zilizopendekezwa na CUF ni pamoja na kusimamishwa kazi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanazibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, ZEC kutangaza matokeo ya majimbo tisa yaliyohakikiwa na kumalizia kuhakiki matokeo ya majimbo 14 yaliyobaki na kutangaza matokeo, vyama vya CCM na CUF kufanya mazungumzo na kukamilisha taratibu za kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kurekebisha mfumo wa uchaguzi Zanzibar.

Suluhu ya kudumu inawezekana Z’bar?

Katika andiko lake, The Zanzibar Conflict: A search for Durable solutions, Professa Gaundence Mpangala, wa Chuo Kikuu cha Dra es Salaam, anasema kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Zanzibar linapaswa kushughulikiwa katika ngazi ya chini na ya juu (micro and macro levels) na kuchukua hatua za kujenga jamii ya kidemokrasia iliyoendelea.

“Katika ngazi ya chini Muafaka I na II lazima utekelezwe pamoja na mapendekezo mengine. Wadau wengi wanaona muafaka II umetekelezwa kikamilifu, lakini hiyo haitoshi kuhakikisha suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa Zanzibar na kujenga amani ya kudumu. Hii ni kwa sababu muafaka huo ulijikita katika masuala ya uchaguzi zaidi. Jamii ya Zanzibar lazima itazamwe kwa uhalisia na kwa upana zaidi. Suluhisho lazima litazamwe kuhusisha masuala kama Muungano, uongozi, utawala wa sheria, elimu, ikiwemo ya uraia, na hali ya maendeleo ya kiuchumi,” inasema sehemu ya andiko hilo.

Njia nyingine ya kumaliza mgogoro

Katika mahoajiano yake na Raia Mwema, Zitto amesema namna nyingine ya kumaliza mgogoro huo ni kwa pande mbili kukubaliana kuongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kugawana vipindi vya miaka miwili na nusu kila chama.

“Maana yake hii ni kwamba matokeo ya wawakilishi yaheshimiwe, kwa sababu yalikwishatangazwa, na tume haina mamlaka ya kufuta matokeo yaliyotangazwa, Wawakilishi wakubaliane katika hili na iitishwe referendum (kura ya maoni) na wananchi waridhie, baada ya hapo CUF waongoze miaka miwili na nusu na CCM hali kadhalika,” alisema.

Hata hivyo alisema hilo litakuwa suluhisho la muda tu kwa kuwa litakuwa suluhisho la wanasiasa kama ambavyo imezoeleka, lakini suluhu ya kudumu ya matatizo ya Zanzibar ni kutafuta suluhisho la jamii ya Wazanzibari.

Matumaini ya muafaka shakani

Yale matumaini waliyokuwa nayo Wazazibari kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kutafuta muafaka wa mgogoro wa kisiasa visiwani, yaliingia doa juzi baada ya Maalim Seif kujitokeza hadharani na kuweka msimamo wa chama chake kuhusu hali hiyo.

“Hoja ya kurudia uchaguzi haina uhalali, haina msingi na ni chachu ya kuiweka nchi katika utawala usiokuwa halali na kusababisha fadhaa kuwa kwa wananchi. Ni hoja ambayo inaweza kuzaa fujo na vurugu katika nchi na kupelekea mzozo mkubwa zaidi wa Kikatiba na kisheria,” alisema Maalim Seif.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Maalim Seif alimshutumu Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kwa kuhujumu juhudi za utafutaji wa ufumbuzi wa haki na wana CCM Zanzibar kwa kauli zinazoashiria kujiandaa na uchaguzi wakati mazungumzo ya kutafuta muafaka yanaendelea.

Akijibu tuhuma hizo za Maalim Seif, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema chama chake kilihamasisha wanachama wake na wananchi kwa ujumla kujiandaa na uchaguzi kwa kuzingatia tangazo za ZEC la kufuta uchaguzi na kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio, huku akimshutumu Maalim Seif kuwa ameingia kwenye mazungumzo hayo siyo kwa nia ya dhati.

“Yako mambo hayasemwi, Seif alijitangazia ushindi akijua ni kinyume cha sheria, alipojua ameteleza akakimbilia kwenye mazungumzo ili kuepuka kushtakiwa,” alisema Vuai alipozungumza na Shirika la Utangazaji la Ujerumani mapema wiki hii.

Hatua hiyo ya Maalim Seif, inairejesha Zanzibar katika hali tete ya kutojua hatma ya muafaka wa mgogoro huo wa kisiasa visiwani humo, baada ya uchaguzi wa Oktoba 25 kufutwa.


Source: Raia Mwema
suala la Zanzibar ni dogo sana kinachotakiwa hapo ni kumalizia uesabuji wa kura na mshindi atagazwe na tume basi
 
Back
Top Bottom