Stories of Change - 2022 Competition

Ras Zimba

New Member
Jul 26, 2022
4
3
Imeandikwa na Ras Zimba

Kwa mujibu wa tovuti ya egscholars.com kupitia andiko lililotolewa tar 16/3/2022 linaonyesha nchi kumi zilizoendelea barani Afrika hasa katika upande wa teknolojia kwa mwaka huu nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Afrika Kusini huku nafasi ya nne ikishikiliwa na Kenya na ya 6 ikishikiliwa na Rwanda huku ya 9 ikishikwa na Uganda. Kwa tafsiri hiyo bila ubishi kwa Afrika mashariki Kenya ni ya kwanza ikifuatiwa na Rwanda alafu namba 3 anachukua Uganda. Sisi Tanzania tunakwama wapi? Tanzania ambayo haijawahi kupitia misuko mingi kama mauaji ya wenyewe kwa wenyewe, nchi iliyoishi kwa amani tangu 1979 haipo katika nafasi za juu hili zimwi litatutafuna mpaka lini? Unapozungumzia kukua kwa teknolojia unazungumzia kukua kwa uchumi pia.

Bila kupepesa macho leo tuweke bidhaa za Kenya na zetu, ubora wa bidhaa za Kenya ni mkubwa na kwa wale waelewa kidogo wa madawa kuna nyakati ukienda kununua Panadol mtu anamuambia muuzaji sitaki za Tanzania nataka za Kenya huo ndio uhalisia na mfano mdogo huku mitaani. Kwahiyo linapokuja swala la ushindani wenzetu wanatuacha mbali sana na hawana vitu vingi vya kujivunia kuwapa pato kubwa la taifa kama sisi ila ni mipango na uthubutu wao. Nikukumbushe tuu Desemba 1963 ndio Kenya inapata uhuru na kuanza kujitegemea katika mfumo wa kiuongozi.

Tanzania leo ana gesi asilia tangu 1970 ila ni nchi ambayo bado haina uhakika wa umeme tunategemea bado kwa kiwango kikubwa mifumo ya maji, tunasubiri nini kuwekeza huko kwa nguvu zote na kila siku tunapiga debe kukaribisha wawekezaji? Uhakika wa nishati ya umeme kunachochea maendeleo ya teknolojia na tusisahau wakati tunaendela na miradi kama SONGAS tuendelee kunoa wazawa wengi katika huo uwanja ili shughuli zikipamba moto isikosekane asilimia ya wafanyakazi wazawa wa ngazi za juu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Tukisema tuwekeze fedha katika miradi ya teknolojia hamna kinachoshindikana tukubali kutuma hata makachero wa teknolojia kwa wenzetu wakaibe ujuzi na kujifunza wenzetu wao wamefanikiwa vipi.

Kwanini teknolojia bado haikuwi kwa kasi Tanzania?

1. Serikali kutowekeza kwa wazawa; Ni aibu sana kuona wazawa wanaobuni vitu katika ulimwengu wa teknolojia hawathaminiki na nchi husika na nchi ikikuthamini tunategemea kuiona ikiwekeza kwako ili kukunyanyua na kunufaisha jamii yake. Tuna mifano michache mikubwa hapa nchini, wa kwanza ni NALA ikiwa ni mtandao unao rahisisha utumaji wa fedha ndani na nje ya Afrika uliotengenezwa na mtanzania Benjamin Fernandes, mwanzoni mwa mwaka huu 2022 umepewa $10 million sawa na 23,320,000,000 za kitanzania kama mtaji wa kwenda kutanua zaidi huduma na huu uwekezaji umefanywa na Amplo, Accel na Bessemer partners hao sio wawakilishi wa serikali ya Tanzania, mwaka 2020 Andron Mendes mtanzania mwingine ameuza mfumo wa mita ya kulipia gesi ya kupikia kadiri unavyotumia (PAYG) kwa kampuni ya Circle Gas ya Uingereza kwa Sh57.6 bilioni ili usambazwe kwa nchi nyingine za Afrika.

Mgunduzi huyo alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa kuendesha mradi huo kutahitaji mtaji mkubwa ili kuwafikia idadi kubwa ya Watanzania huku mahitaji yake yakiongezeka.(Chanzo cha hiyo habari ya Andron; tovuti ya Mwananchi.co.tz) kwahyo angepata kushikwa mkono na serikali leo taifa lingenufaika vikubwa kwa maarifa yake na inawezekana huduma ingekuwa kwa bei nafuu hiyo ni mifano miwili mikubwa ni kwa namna gani Tanzania hatuna muamko wa kuwekeza kwa wale wabunifu wetu na hii inapunguza morale kwa vijana wengi kwahyo tusiandae tuu mashindano ya maandiko ya miradi ila tuwekeze zaidi kwa miradi ya teknolojia ambayo tayari inafanya kazi. Tupo na Nyumbu mradi uliopo Kibaha chini ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kasi yake ya uzalishaji magari ingekuwa kubwa zaidi kama serikali itawekeza inavyotakiwa.

2. Sera mfu za kukuza teknolojia; sera mfu ni sera zisizokuwa za kishindani, sera ambazo hazifanyiwi kazi. Tanzania tunahitaji sera hai za kiushindani ili kuboresha sekta ya teknolojia.

3. Uzalendo wa viongozi; Viongozi wetu wakiacha ubinafsi hawataweka sahihi katika miradi mibovu/mfu ya teknolojia ambayo haina tija hata kimaandishi pia viongozi wakiwa wazalendo tutaibua wengi mno wabunifu waliopo katika ulimwengu wa teknolojia hapa nchini kuanzia ngazi ya kata mpaka taifa. Iringa kuna kijana aitwaye W.Lubida namfahamu ni mtengenezaji redio/amplifaya anatengeneza hivo kwa mfumo wake mwenyewe (Sakiti) na bidhaa zake zinaleta ushindani kwa kampuni kubwa zilizo zoelekea mtaani kama Aborder n.k ila ana miaka 5+ sasa na siamini kama viongozi wa pale hawaoni ile ni fursa, hawajui yule akiwezeshwa vijana wa lile eneo tunapata ajira chache kwasababu kampuni itahitaji watendaji kazi ila kukosa uzalendo wa kweli kwa viongozi wenye dira ya kuona taifa linafika mbali yule kijana bado anahangaika mwenyewe kwa kukosa mtaji mkubwa kitu ambacho kinakwamisha mengi.

Ukuaji wa teknolojia kutasaidia kupunguza uhalifu, kutaongeza fursa za kukuza uchumi kupitia vitu kama viwanda, ukuaji wa teknolojia kutasaidia kutangaza taifa katika nyanja nyingine kutokana udhalishaji wa bidhaa zetu wenyewe. Tanzania tuamke!
 
Safi Ras Zimba, teknolojia ina majibu kwenye changamoto nyingi zinazokwaza maendeleo yetu, ni kama adui ujinga bado yupo alipungua tu kipindi cha awamu ya kwanza lakini kwa sasa ujinga ni zimwi kabisa, hapo ndio chanzo cha hali hii tuliyo nayo, elimu yetu ni ya vyeti zaidi..imefikia hata wanaotuongoza tunaona elimu haijawasaidia, basi shida ni kubwa..ukiona usanii ndio kama kazi ya kwanza kwa nchi na inawekwa wekwa mbele na serikali ujue lipo tatizo kubwa kitaifa!
 
Sisi bado tunatenda na kuwaza kijimaa. Ukitaka kuamini tuma email kwenye ofisi yoyote ya serikali uone utajibiwa baada ya miezi mingapi
 
Msiwalaumu watanzania. Tatizo la hii nchi ni CCM pekee!

Matatizo mengine yote yanasababishwa na hilo tatizo kuu. Imagine hata Paypal imeshindikana kwenye hii nchi!

Tunaongozwa na mapopoma!
 
MAREKEBISHO:

Mfumo uliuzwa billion 5.5 hivi kama sikosei sio billion 57 mkuu..

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Chukua Chako Mapema ndicho tunachokiweza sisi wa TZ
 
Hakika...

Badala yake tunaenda kununua teknolojia nje kwa gharama kubwa sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…