Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 263
- 429
Kuelekea siku ya wapendanao "Valentine's day" watu wengi hukuna vichwa ni zawadi gani wawapatie wawapendao.
Wengine huwaza sana na kuwa na hofu kwa sababu hawana pesa nyingi kuweza kuwanunulia vitu vya thamani kubwa Kama magari na nyumba.
Makala hii inakusogezea uzijue zawadi zenye nyuvu ya Valentine's ambazo unaweza kumpatia umpendae kulingana na uwezo wako.
Zawadi ya kwanza ni kadi maalumu ya Valentine's, hii ni kadi iliyochapishwa kwa nakshi ya maua na rangi inaweza kuandikwa ujumbe wowote wa upendo na heri kwa mpenzi, mwenza au rafiki yako. Kadi hii huweza kufungashwa katika mfuko maalumu na kumfikia mlengwa aifurahie.
Marianne Stenger, kutoka London nchini Uingereza aliwahi kuainisha zawadi zingine kama kalenda maalumu, picha nzuri na vitabu maalumu, Kama zawadi muhimu kwa wapendanao ambayo inaweza kudumu kwa muda mrefu kwa mpokeaji.
Maua mazuri, ni zawadi nyingine inayotajwa kubeba ujumbe mzuri wa upendo wa Valentine's, watu wengi hupendelea maua yenye rangi nyekundu na nyeupe ambayo ni maarufu katika Kipindi cha Valentine's wahusika hupeana na kuyatunza.
Umewahi kufikiria kuwa mlo wa pamoja ni zawadi? basi ngoja nikujuze, mlo wa pamoja uwe wa mchana au wa usiku kwa wapendanao ni zawadi tosha ya Valentine's Unaweza kuandaa mlo huo vizuri kwa kuzingatia chakula pendwa kwa wahusika Kisha kumualika umpendae mle pamoja kwa wakati maalumu iwe nyumbani, hotelini au mgahawani.
Pia Zawadi ya nguo ni zawadi maarufu sana ya Kipindi cha Valentine's ambapo watu wengi huwanunulia nguo za rangi mbalimbali na kuwapa wawapendao, wengine huziandika ujumbe mbalimbali kama vile "Asante mama", "Nakupenda sana", "Uishi vema malkia, mfalme" na Kadhalika. Zawadi hii ya nguo huvaliwa katika siku hiyo maalumu ya Valentine's.
Ikiwa umpendae anapendelea manukato basi chagua manukato nzuri ili umzawadie kwakuwa ni zawadi ambayo inatajwa pia kuwa na nguvu ya Valentine's.
Kunukia vizuri ni chaguo la wengi, mnunulie umpendae marashi "Parfumes" Kisha mpelekee kama zawadi ya Valentine's atafurahi sana.
Hivi unajua tiketi za usafiri, ni zawadi pia? Unaweza kumzawadia umpendae kwa kumkatia tiketi ya safari kwenda eneo fulani alipendalo kisha imrudishe utakuwa umemfurahisha Sana na kumuonyesha upendo.
Kama umpendae ni mtu wa kupenda kuudhuria matukio mbalimbali Kama Muziki, sinema na michezo mingine mnunulie tiketi ya tukio husika.
Kuna wale wapenda vitu vidogo vidogo Sana Kama "chocolate" mnunulie kwa wingi kisha mfungashie akale huko atafurahi zaidi na kuhisi kupendwa.
Kama una nguvu ya Kiuchumi unaweza kumzawadia vitu vya thamani kama saa ya gharama kubwa, pete ya dhahabu au mkufu.
Walio na kifua cha pesa huwanunulia wawapendao magari, nyumba na vitu vingine vya gharama.
Asikwambie mtu kuwa kuna zawadi ndogo, zawadi ni zawadi na ina maana kubwa kwa kila inapotoka na kupokelewa hivyo usikae kinyonge.