Zijue sifa na gharama za kumiliki silaha Tanzania

𝗨𝗻𝗮𝗵𝗶𝘁𝗮𝗷𝗶 𝗸𝘂𝗺𝗶𝗹𝗶𝗸𝗶 𝘀𝗶𝗹𝗮𝗵𝗮

Najua watu wengi wanatamani kuweza kumiliki silaha yani mtu awe nayo kama msaada kwenye kujilinda na masuala mbalimbali lakini je unaweza kumiliki silaha?

1_20241028_164900_0000.png


Kwanza kumbuka maelezo ninayokupa ni kukupatia Elimu kuhusu masuala ya kumiliki silaha kihalali. Jambo muhimu zaidi kwenye sheria ya umilikaji wa silaha inaweza kubadilika hivyo ni muhimu kutembelea mamlaka husika kupata taarifa zaidi.

2_20241028_164900_0001.png


Wengi wanatamani kumiliki silaha lakini Kuna taratibu zake za kufuata ili uweze kuwa mtu mmoja wapo mwenye Uwezo wa kumiliki silaha. Kupitia kifungu namba 11 cha sheria za umiliki na usimamizi wa silaha ya mwaka 2015 imetaja sifa za mtu atayeweza kumiliki silaha nchini Tanzania 👇
  • lazima uwe umetimiza miaka 25 hii ni kuamini kuwa mtu anayemiliki silaha ni mtu mzima pia ana Uwezo wa kufanya maamuzi ya busara.
  • lazima uwe na Ujuzi wa kutumia silaha ni kama mtihani lazima ujue jinsi ya kutumia kwa usalama na nia njema.

images (18).jpeg

  • lazima uwe raia mtanzania au uwe na kibali cha ukaazi wa kudumu
  • lazima uwe na akili timamu pia mtu ambaye sie mgomvi.
  • usiwe mtumiaji wa dawa za kulevya
  • usiwe na rekodi ya mtu aliyefanya uhalifu
  • usiwe na ulemavu wa akili au uzembe

Pia sheria imezungumzia watu wengine wenye Uwezo wa kumiliki silaha ni wanaowalinda viongozi,watalii wa uwindaji,maafisa wanaosindikiza wafungwa.

images (19).jpeg


Kibali cha kumiliki silaha 👇
• mmiliki anapaswa kuinunua silaha kwenye maduka yanayotambulika na serikali
• lazima upitie serikali za mtaa wako kamati ya mtaa itaweza kukujadili Kisha kata, Kisha utapelekwa kwa OCD
• mmiliki lazima uwende na risiti uliyonunulia silaha kwenye kituo cha polisi cha wilaya utakabidhiwa fomu na kujaza
• Fomu ya mmiliki itajadiliwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya akishapitishwa itapelekwa kweye kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa
• Mmiliki atapatiwa kibali na kasha kuruhusiwa kwenda kuchukua silaha yake kwenye duka halali alilonunulia

Gharama za kumiliki silaha zinaanzia dola 150 kwa raia ambaye sio mtanzania
 
Kuna tetesi zinasema kipindi Cha Uchaguzi nyote mnarudisha bomba mpaka Hali iwe shwari. Je Kuna ukweli kuhusu hili.
 
Back
Top Bottom