Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 672
- 1,313
ANGALIZO
Maelezo yaliyotolewa katika uzi huu ni kwa ajili ya kuelimisha na kutoa taarifa kwa umma na hayapaswi kutafsiriwa kama ushauri wa kisheria. Sheria za umiliki wa silaha zinaweza kubadilika, na ni muhimu kushauriana na mwanasheria au mamlaka husika kwa taarifa zaidi na za kina. Mwandishi wa uzi huu hawajibiki kwa matumizi yoyote yasiyofaa ya taarifa zilizotolewa.

Habari zenu wapendwa wa JamiiForums,
Katika kona za mijadala na vijiwe vya mazungumzo, suala la umiliki wa silaha limeibua maswali mengi na mitazamo tofauti miongoni mwa Watanzania. Wapo wanaoamini kwamba uwezo wa kifedha na umiliki wa mali ndio vigezo vikuu vya kupata haki ya kumiliki silaha, huku wengine wakiona ada za leseni kama kikwazo kikubwa. Lakini, je, uhalisia wa sheria zetu unatuelekeza vipi katika hili?
Katika jitihada za kufafanua ukweli na kuondoa dhana potofu, nimeandaa uzi huu kwa lengo la kuelimisha na kutoa mwanga juu ya sheria za umiliki wa silaha nchini Tanzania. Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuelewa sheria hizi, si tu kwa ajili ya kujilinda, bali pia kwa ajili ya kuchangia katika usalama wa jamii yetu. Kifungu cha 11 cha Sheria ya Umiliki na Usimamizi wa Silaha, ya mwaka 2015 kimetaja sifa za mtu anayeweza kumiliki silaha nchini Tanzania. Sifa hizo ni pamoja na;

- Kwanza, kama unataka kumiliki silaha, lazima uwe umetimiza miaka 25. Hii ni kuhakikisha kwamba silaha zinaangukia mikononi mwa watu wazima wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara.
- Pili, lazima uwe na cheti cha uwezo. Hii ni kama mtihani wa kuonyesha kwamba unajua jinsi ya kutumia silaha kwa usalama na kwa nia njema.
- Tatu, ni lazima uwe raia wa Tanzania au uwe na kibali cha ukaazi cha kudumu. Hii ina maana kwamba wageni hawawezi tu kuja na kuanza kumiliki silaha hapa nchini.
- Nne, ni muhimu sana kuwa na akili timamu na usiwe na tabia ya ugomvi. Tunataka silaha ziwe mikononi mwa watu wanaoweza kudhibiti hasira zao.
- Tano, usiwe tegemezi wa dawa za kulevya au narkotiki. Hii ni wazi, tunataka kuepuka hatari zinazoweza kutokea mtu akiwa chini ya ushawishi wa vitu hivi.
- Sita, usiwe na rekodi ya uhalifu. Kama umewahi kufanya makosa makubwa, basi huwezi kupewa leseni ya kumiliki silaha.
- Na mwisho, usiwe na ulemavu wa akili au uzembe unaoweza kukufanya ushindwe kumiliki silaha kwa usalama.
Sheria pia inasema kwamba kuna watu wachache wanaoweza kupewa leseni ya muda ya kumiliki silaha, kama vile walinzi wa viongozi, watalii wa uwindaji, na maafisa wanaowasindikiza wafungwa. Sasa, je, mnafikiri sifa hizi zilizopo kisheria zinatosha kutulinda? Au kuna kitu kinapaswa kubadilishwa?
Kwa upande mwingine, gharama za kumiliki silaha kisheria ni kama zifuatazo :
- Dola za Marekani 150 kwa miezi sita kwa aina yoyote ya silaha
(b) Ada ya mafunzo ya uwezo
- Shilingi 40,000/=
(c) Upimaji wa uwezo wa mara kwa mara
- Shilingi 20,000/=
(d) Gharama za kurenew leseni
- Bastola Shilingi 70,000/=
- Bunduki Shilingi 35,000/=
- Bunduki za mzigo wa mbele Shilingi 35,000/=
- Nyinginezo Shilingi 35,000/=
- Bunduki ya risasi Shilingi 35,000/=
(e) Ada ya leseni ya ghala binafsi kwa mwaka
- Shilingi 1,000,000/=
(f) Ada ya kibali cha muuzaji wa silaha kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(g) Ada ya kibali cha fundi bunduki kwa mwaka
- Shilingi 500,000/=
(h) Ada ya kibali cha usafirishaji wa silaha
- Shilingi 500,000/=
Uzi huu umechambua sheria zinazosimamia umiliki wa silaha na gharama zinazohusiana na upatikanaji wa leseni za silaha nchini Tanzania. Uchambuzi huu unalenga kutoa mwanga na kuchochea tafakuri juu ya ufanisi wa sheria hizi katika kudumisha usalama na utulivu. Ni dhahiri kwamba uelewa wa sheria hizi ni muhimu kwa kila raia, na ni jukumu letu kama wanajamii kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga jamii yenye amani na usalama. Ni matumaini yangu kwamba, kupitia uchambuzi huu, wadau mbalimbali watapata uelewa juu ya suala hili kisheria.
View: https://youtu.be/keuwPn4oyx4?si=Zdr6b_61moIMFQ3C