Zijue faida za Mmea wa Mlonge, Jitibu magonjwa 300 kwa kutumia mlonge

Nawasalimu wana JF. Mimi nilipanda miti ya mlonge kutokana na ushauri juu ya mmea huu. Bahati nzuri miti imestawi vizuri na kutoa mbegu nyingi. Sasa najiuliza mbegu na majani nivitumie vipi kwa afya? Je, naweza kutafuna mbegu zikiwa kavu? Je nitafuna mbegu za mlonge kuna faida/hasara gani? Je, naweza kutafuna majani mabichi ya mlonge? Kufanya hivyo kuna faida na hasara gani? Je naweza kuchemsha majani au mbegu za mlonge na kunywa? kuna faida au hasara gani? Nawaombe mnisaidie. Asante sana

Mlonge ni mmea bora.
MATUMIZI.
1.Majani yake waweza kuyatumia kama majani ya chai.
2.Majani hayo pia waweza kupika mboga na ukaiunga nazi na viungo km kitunguu swaumu,giligilani n.k nzuri sana.
3.Magome yake hutumika kama mfano wa P.O.P kwa viungo vilivyo pata (STROKE),KIHARUSI au mivunjiko na huunga mara 1.
4.Mbegu hutibu PRESHA,UCHOVU wa UBONGO na MWILI
FAIDA
Hutibu magonjwa yote ya ndani na nje ya mwili.
Huongeza nguvu za kiume
Huponya HOMA,MAFUA n.k
 
Asante Nzuri pesa. Majani yake yanatengenezwaje kuwa kama majani ya chai (Uchakataji wake ukoje? Asante. Nimepata pa kuanzia. Japo nilitakua kujua nikila majani mabichi au nikiandaa juice ya majani mabichi ya mlonge inakuwaje?
 
Members,

Naomba kujua mlonge unasaidiaje kama tiba? wenye kujua naomba mtuhabarishe.
Mkuu Mlonge ni dawa kwa magonjwa mengi sana nadhani umesoma yote hapo juu. Mi nautumia tu hata pale nisipojisikia kuumwa kwani una madini madini mengi, vitamini nyingi na huondoa sumu mwilini kirahisi zaidi, lakini pia huongeza kiu cha maji kwahiyo kama upo sehemu za baridi au wewe ni mvivu kunywa maji ukitumia mlonge lazima utakunywa maji. Unauhitaji?
 
naomba uniwekee picha ya mti huo sijui unafananaje
 
Members,

Naomba kujua mlonge unasaidiaje kama tiba? wenye kujua naomba mtuhabarishe.

MLONGO NI MULTPAPAS MZEE. Mbegu zake ukichanganya kwenye uji, ule unga wake sio kupika, kunyunyiza kwenye uji au chai, husaidia kuengeza virutubisho vya mwili, na kwa wagonjwa wa ukimwi huongeza uwezo wa CD4.

Pia mbegu, majani na mizizi, ukitumia kwa namna yoyote ile, majani upike kama mchicha, uyatuie kama kiungo, huongeza nguvu za kiume, watu huwa rijali kwa mlonge tu
 
naomba uniwekee picha ya mti huo sijui unafananaje
Sogeza mouse juu ya picha:
Mlonge.jpg
 
Habari wana jamvi.
Leo ningependa tufahamu jinsi ya kupika mboga ya majani ya MLONGE.
1. Chuma majani machanga ya mlonge,
2. Chambua na kosha vizuri
3.Tia ktk sufuria safi tia chumvi na funika
4.Bandika jikoni acha ichemke km dk 5 halafu weka nyanya,kitunguu maji na kitunguu swaum vilivyosagwa.
5.Ichemke kwa dk10 zaidi hakikisha mvuke hautoki.
6.Tia naz yako pooza tui had lichemke vizuri.
Mboga yako tayari.
FAIDA YA MBOGA YA MLONGE:
1. KUONGEZA UWEZO WA KUMBUKUMBU
2.NGUVU ZA KIUME
3.KUONDOA UCHOVU WA MWILI NA AKILI
4.HULINDA MWILI NA KIHARUS,PRESHA,SUKARI N.K
 
Siku zote Nilifikiri majani ya mlonge yatakuwa machungu , kwa maelezo yako itabidi niyajaribu leo.
 
huo Mlonge nasikia ni mchungu inakuwaje upikwe kama mboga?
ooh mama kumbe mwarobaini nawe unaweza kuliwa kama mboga

asante kwa post
 
Habari wana jamvi.
Leo ningependa tufahamu jinsi ya kupika mboga ya majani ya MLONGE.
1. Chuma majani machanga ya mlonge,
2. Chambua na kosha vizuri
3.Tia ktk sufuria safi tia chumvi na funika
4.Bandika jikoni acha ichemke km dk 5 halafu weka nyanya,kitunguu maji na kitunguu swaum vilivyosagwa.
5.Ichemke kwa dk10 zaidi hakikisha mvuke hautoki.
6.Tia naz yako pooza tui had lichemke vizuri.
Mboga yako tayari.
FAIDA YA MBOGA YA MLONGE:
1. KUONGEZA UWEZO WA KUMBUKUMBU
2.NGUVU ZA KIUME
3.KUONDOA UCHOVU WA MWILI NA AKILI
4.HULINDA MWILI NA KIHARUS,PRESHA,SUKARI N.K

Pia unaweza kuchukua majani machache ya mlonge ukayaosha vizuri na kutumbukiza kwenye maji ya moto dkk chache ili kuua wadudu kisha unaweka kwenye blender na kublend kupata juisi. safi sana kwa kuongeza kinga ya mwili!
 
huo Mlonge nasikia ni mchungu inakuwaje upikwe kama mboga?
ooh mama kumbe mwarobaini nawe unaweza kuliwa kama mboga

asante kwa post
Mi huyachuma na kuyachemsha nakunywa kama juisi,majani ya Mlonge sio machungu yana utamu kwa mbali kama utamu wa sukari,ila vile vimbegu vyako vina ugwadu flani hivi ,pia huyatafuna pia hivi hivi hayana uchungu
 
Back
Top Bottom