Zenawi katika ubora wake: Magufuli aige mbinu na mikakati ya mwana huyu wa Afrika

Bukyanagandi,

..huyu jamaa ni wa kumsikiliza kwa makini.

..particularly msikilize dakika ya 14.35 na dakika ya 41.

..anatoa majibu ya maswali mengi ambayo tumekuwa tukijiuliza.

..kwa mfano anazungumzia masuala ya uwekezaji ktk umeme vs viwanda.

..ametoa mfano wa kuhusu kukaribisha wawekezaji binafsi/wa nje ktk sekta ya umeme na risks na athari zake ktk ukuaji wa viwanda ktk taifa changa.

..anadai muwekezaji binafsi ktk sekta ya umeme anataka FAIDA KUBWA, na atakayebeba mzigo wa kuhakikisha faida hiyo ni mtumiaji and most likely mwenye kiwanda. kwa hiyo anachofanya Meles Zenawi ni serikali yake kuwekeza ktk biashara ya umeme ili wenye viwanda wasibebe mzigo mkubwa wa gharama za umeme.

..Mimi natamani Raisi Magufuli aiwezeshe Tanesco kuwa na monopoly ktk biashara ya umeme mpaka pale ambapo nchi ime-industrialize vya kutosha na wenye viwanda wanaweza kujiendesha ktk mazingira ambapo sekta ya umeme imebinafsishwa.
 
Back
Top Bottom