Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

green rajab

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
11,314
35,856
Zanzibar watalii wanne wa Ki Israel wametimuliwa baada ya kuleta fujo ndani ya hotel baada ya kuona gari la manager wa Hotel Hiyo Ina stika za Free Palestine

🚨🇮🇱🇵🇸 FOUR ISRAELIS were KICKED OUT OF A HOTEL in Tanzania for complaining about the "FREE PALESTINE" badge on the manager's car.
IMG_20240420_034154.jpg

Four Israelis were kicked out of a hotel in Tanzania for complaining about the free Palestine badge on the manager's car.

The Canary Nungwi Hotel in Zanzibar kicked out four Israelis who interrogated a receptionist about a vehicle parked outside the premise with stickers that read "Free Palestine." The Israelis were told the vehicle belonged to the manager of the hotel, and they were eventually kicked out after complaining that the vehicle was causing them "concern."
 
View attachment 2968844

Hii habari imekaa kishabiki kuliko uhalisia, upande wa pili sio habari za kushabikia ikiwa mnapenda kuongeza mapato ya kitalii.
Kama ni kweli kuna tukio kama hilo, suluhisho lilikuwa majadiliano na kulimaliza kidiplomasia.
Sio sahihi sana kuweka itikadi kwenye biashara.
 
Hotel au sehemu yenye kutoa huduma kwa watu wenye itikadi, imani, maono mchanganyiko unawekaje vitu vitakavyowakwaza? Kutokujielewa huko na kuharibu biashara.
Umetafakari kwa kina au umekurupuka kumbuka Hilo ni gari binafsi ni kama wewe ukiwa na gari yako ndani umeweka bendera ya Chadema afu ukalipaki kazini kwako afu wafuasi wa CCM walalamike
 
Hiyo sasa ni Ant Semitism! Na inaonekana huenda kwa kujua ni Waisraeli, meneja amebandika stika hiyo ili kuwaudhi. Lakini hata kama walichukia wasingetimuliwa ndani ya Hotel.

Tuwe makini tusije kuharibu soko letu la Watalii.

Ukiigusa Israel umeigusa US, UK, umegusa nchi za jumuia ya Ulaya, EU!

Zinaweza kuzuia Watalii wasije.
 
Umetafakari kwa kina au umekurupuka kumbuka Hilo ni gari binafsi ni kama wewe ukiwa na gari yako ndani umeweka bendera ya Chadema afu ukalipaki kazini kwako afu wafuasi wa CCM walalamike
..."Kazini kwako"...! Ofisi binafsi, ya chama au ya umma? Kama ni binafsi au ya chama ni sawa kuweka bendera. Lakini, kama inatumiwa na watu wote/umma, kuweka bendera za kisiasa ni upumbavu uliopitiliza viwango.

Halafu; kulikuwa na ulazima au umuhimu gani wa kuwafukuza hao watalii/wageni wa Kiizraeli kwa sababu ya kuuliza walichouliza tu? Hakukuwa na namna ya kuwaelewesha kuhusu uhuru wa kufanya mambo katika nchi (Zanzibar) bila kuvunja sheria? Hoja kuu ya kuwafukuza ni ipi?
 
Zanzibar watalii wanne wa Ki Israel wametimuliwa baada ya kuleta fujo ndani ya hotel baada ya kuona gari la manager wa Hotel Hiyo Ina stika za Free Palestine

🚨🇮🇱🇵🇸 FOUR ISRAELIS were KICKED OUT OF A HOTEL in Tanzania for complaining about the "FREE PALESTINE" badge on the manager's car.
View attachment 2968844

Four Israelis were kicked out of a hotel in Tanzania for complaining about the free Palestine badge on the manager's car.

The Canary Nungwi Hotel in Zanzibar kicked out four Israelis who interrogated a receptionist about a vehicle parked outside the premise with stickers that read "Free Palestine." The Israelis were told the vehicle belonged to the manager of the hotel, and they were eventually kicked out after complaining that the vehicle was causing them "concern."
Watu wanajisahau sana, kama hawakupendezwa na hilo wangehama hoteli kimyakimya na sio kuanzisha fujo. Upo nchi za watu unataka kupangia watu maisha?
 
Kama ni Gari BINAFS la meneja sio issue sana ila kam ni gari la ki ofisi meneja amekosea
Hata kama ni gari binafsi la meneja, naona atakuwa kakosea. Yeye ni meneja au mtu binafsi. Sawa. Lakini, akumbuke amefika eneo la kazi ambalo anatakiwa ahudumie watu wenye imani, misimamo, itikadi, na maono tofauti tofauti. Kwa mfano, mteja Muizraeli akipatwa na dharura kiafya (au chochote) itakayohitaji apate usafiri, atakubali kutumia hilo gari kweli? Na tunajua watalii wengi Zanzibar siyo Wapalestina. Ni haohao "wazungu na waizraeli" anaowakwaza.
 
Back
Top Bottom