Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 14,403
- 29,557
Kama muumini mkubwa wa kutumia akili vizuri ili kupata maendeleo makubwa napenda kumpongeza sana Rais wa Zanzibar kwa anavyoitengeneza Zanzibar iwe na uchumi mkubwa unaojitegemea miaka ya mbeleni.
Rasilimali kubwa inayompa maendeleo ya kweli mwanadamu ni akili. Rasilimali si madini, si maliasili maana unaweza ukawa navyo vyote ila kwa kukosa akili vinaweza kutokupa maendeleo ya kweli.
Zanzibar wameweza kulithibitisha hili kwa kuwa wametumia akili kujua kuwa fursa ya utalii ndo njia inayoweza kuwapa mapato makubwa sana huko mbeleni na kuepuka utegemezi hivyo wameamua kuwekeza kweli kwenye utalii hasa kuvutia wawekezaji ambao wanajenga mahoteli yenye hadhi ya juu kabisa kwa ajili ya kujitengeneza kama sehemu kuu ya utalii katika kanda hii ya Afrika.
Kusema ukweli nimevutiwa sana na miradi mikubwa ya ujenzi wa hoteli kubwa na za kisasa kabisa inayoendelea kujengwa Zanzibar. Miradi hii inaitangaza Zanzibar zaidi, inaifanya Zanzibar ijulikane zaidi duniani na kuvutia watu wengi kuitembelea Zanzibar na kuihakikishia kuwa na mapato makubwa na ya uhakika huko mbeleni kiasi ambacho kitaondoa utegemezi wa Zanzibar katika misaada na hata mikopo.
Zanzibar wameshagundua kuwa sehemu ya kuitumia kutoka kiuchumi ni Utalii na wanafanya kweli.
Tukija kwa Tanzania bara huku ndo kuna mabingwa wa maneno, kujisifu, kulalamika na kupiga pesa. Huku hadi sasa ni kama mtu ambae bado anajitafuta na hajajua aweke nguvu kubwa kwenye nini ili kujihakikishia kupata mapato makubwa siku za mbeleni na kuondokana na utegemezi wa misaada na mikopo kichefuchefu.
Huku kila kitu tunafanya alafu mbaya zaidi tunafanya bora liende. Hakuna kitu ambacho tunafanya kwa nguvu na akili kubwa tena kwa ufanisi kiasi ambacho tunaweza sema hiki ndo tunakifanya ili kututengenezea mapato makubwa kwa ajili ya kuondoa utegemezi huko mbeleni.
Ninachosikitika zaidi miradi mingi ya huku bara sio miradi ya kutengeneza fedha na mapato huko mbeleni, miradi mingi ya huku ni kwa ajili ya kutumia tu pesa kujenga majengo ya shule, ofisi, miundombinu ambayo huko mbeleni itahitaji maintenance na repair ambazo zitahitaji pia pesa ambazo bado hatujatumia akili zetu kujua tutazipata wapi kwa miaka mingi huko mbeleni.
Naisikitikia sana Tanzania Bara maana kusema kweli siioni ikiendelea kuwa sustainable kiuchumi kwa miaka mingi mbeleni.
Viongozi wa Tanzania Bara siwaoni wakitumia akili vizuri walizopewa na Mungu kuwaza, kupanga na kufanya mambo makubwa tena kwa ufanisi mkubwa kuihakikishia nchi inakuwa na mapato makubwa huko mbeleni na kuondokana na utegemezi.
Naisikitikia Tanzania Bara.