Zanzibar: Mwanaume afikishwa Mahakamani kwa kukata viuno hadharani

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,246
4,831
Zanzibar ni nchi ya kiislamu?

===
Maulid Hussein Abdallah maarufu kama Mauzinde (29) amefikishwa Mahakama ya Mwanzo katika Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja Kisiwani Zanzibar, kwa tuhuma ya kukata viuno hadharani.

Kijana huyo mkazi wa Rahaleo anatuhumiwa kutenda kosa hilo huko Kibole, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja saa 11 jioni, ambapo mshitakiwa akiwa amevalia mtandio alicheza kwa kukata kiuno mbele ya hadhara jambo ambalo ni kosa kisheria.

Mshitakiwa huyo amepinga mashtaka hayo na kuiomba Mahakama kumpa dhamana kwa kuwa yupo kituo cha polisi siku nyingi.

Amri ya kupelekwa rumande imetolewa na Hakimu Safia Waziri, baada ya mshitakiwa kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya TZS 100,000 pamoja na barua zikiambatana na kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar.

Mshitakiwa baada ya kushindwa kutekeleza masharti hayo, mahakama ilimuamuriwa kwenda rumande hadi Aprili 25, 2022 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ushahidi.

PIA SOMA
- Msanii Baby J na mwenzake Mauzinde watakiwa kukamatwa wakidaiwa kuandaa sherehe iliyokuwa na vitendo vya kuvunja maadili

- Watu wasiyojulikana wamshambulia Mauzinde kwa kumtaka masikio na kumtelekeza msituni

- Nani kamfadhili Mauzinde kwenda Canada?

Source: Swahilitimes
 
kwa watakaoomba picha,nimeweka hapo chini
IMG_3249.JPG
 
Maulid Hussein Abdallah maarufu kama Mauzinde (29) amefikishwa Mahakama ya Mwanzo katika Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja Kisiwani Zanzibar, kwa tuhuma ya kukata viuno hadharani.

Kijana huyo mkazi wa Rahaleo anatuhumiwa kutenda kosa hilo huko Kibole, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja saa 11 jioni, ambapo mshitakiwa akiwa amevalia mtandio alicheza kwa kukata kiuno mbele ya hadhara jambo ambalo ni kosa kisheria.

Mshitakiwa huyo amepinga mashtaka hayo na kuiomba Mahakama kumpa dhamana kwa kuwa yupo kituo cha polisi siku nyingi.

Amri ya kupelekwa rumande imetolewa na Hakimu Safia Waziri, baada ya mshitakiwa kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya TZS 100,000 pamoja na barua zikiambatana na kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar.

Mshitakiwa baada ya kushindwa kutekeleza masharti hayo, mahakama ilimuamuriwa kwenda rumande hadi Aprili 25, 2022 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ushahidi.

Source: Swahilitimes
 
Hii habari inachanganya sana,Kukata kiuno Hadharani Zanzibar ni kosa kweli??sehemu ambako ndiko makao makuu ya taarabu na nyimbo za kukata mauno?

Mi nahisi huyo jamaa labda ni Shoga sasa wakaona wamtafutie namna ya kumshtaki,maana ukisoma kuna mahali wanasema kavaa mtandio,mwanaume anayeweza kuvaa mtandio ni mwenye tabia hizo tu,vinginevyo niambiwe maana ya mtandio kwa muktadha wa huko Kisiwani.
 
Back
Top Bottom