Masaki
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,463
- 753
Huu ni mfano mzuri wa namna tunavyoshindwa kujiendeshea mambo, hata yenye manufaa makubwa kwa uchumi wetu.
Hebu tufikirie tu mara moja, kama Zanzibar wangeamua tu na kutoa kipaumbere sekta hii ya utalii na kuiendeleza ipasavyo, si ingetosheleza kabisa kuinua pato zima la visiwa vile?
Kwa mfano: wangeweza kuingia watalii million moja kwa mwaka, pato linalotokana na hawa watalii halitoshi kubadili hali ya uchumi?
Ni kitu gani kinachozuia pasiwepo na maandalizi ya kutimia kwa azma kama hiyo?
Na kila mtalii mmoja akatumia japo dola 400 tu ndani ya Zanzibar, basi kwa mwaka pato la ndani la Z'bar lingekuwa linaingiza dola miloni 400 kutokana na utalii.