Yule kichaa aliyekuwa akipita Mikumi kwa miguu kaliwa na simba miezi 2 iliyopita

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
859
1,865
Wadau wanaosafiri na kupita njia ya mikumi watakuwa wanamfahamu yule kichaa anaetembea barabara ya mikumi mwanzo mwisho ,yeye huwa anakatisha mikumi kwa miguu iwe asubuhi ,mchana au usiku na ni maarufu sana .mara nyingi huwa anatembea/anakatisha barabara ile

Imepita miezi 2 kichaa yule kaliwa na simba na inaonyesha alivamiwa na kuliwa usiku maana viatu na nguo zilizoraruriwa zilionekana pembeni ,kwa miaka mingi amekuwa akipita bila kudhuriwa ila siku ile sijui alikutana na simba aliyevurugwa

RIP kichaa Ras
 
Serikali ikubali lawama kwa uzembe, kwanini iliruhusu mtu kuingia kwenye mbuga bila kufuata taratibu!
 
Lazima ataondoka na mtu,believe me!....Simba aliekula nyama ya mtu lazima ataonja tena,nyama ya mtu ni tamu kuliko ya swala!!
Yaan kama jamaa wamelitambua hilo kuwa simba kamtafuna basi hata huyo simba atakuwa kishauawa siku zilezile alivyomtafuna Ras! .
Simba akishakula mtu ni hatari sana hata kwa askari wenyewe hivyo wanafanya lolote lazima auawe!.

Kuna kisa kilitokea hifadhi ya ruaha jamaa walikuwa wanatengeneza barabara toka idodi kuelekea hifadhini basi wale mafundi usiku walikuwa wanaenda kunywa kwenye lodge za hifadhini siku moja usiku Simba alimkamata jamaa mmoja alimtafuna na alibakisha kichwa pekee....weee ulianza msako wa kumtafuta simba mpaka alipatikana na kuuawa maana hakuna namna nyingine
 
Back
Top Bottom