Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 337
- 699
Miriam Thomas Chirwa, anayejulikana kwa jina la "Mwinjilisti Miriam," alizaliwa tarehe 15 Septemba 1998, akiwa na ulemavu wa macho
Alianza safari yake ya muziki akiwa na umri wa miaka 6, ambapo alirekodi nyimbo 5. Akiwa na miaka 10, alirekodi nyimbo 10 na kutoa albamu yake ya kwanza "Mseme Yesu Watu Wapone," kisha akaanza kuimba nyimbo za kuelimisha jamii.
Ameshiriki katika kampeni mbalimbali za kutetea Watoto na Walemavu na mwaka 2011-2012 alipewa Tuzo ya 'Best Ambassador to the Community' na Tanzanian Gospel Music Awards.