Yoweri Kaguta Museveni alizaliwa 19 September 1944, ni mwanasiasa wa Uganda ambae amekua rais wa Uganda tangia 29 January, 1986.
Museverni alijiunga na majeshi ya uasi ambayo yamtoa aliyekua rais wa Uganda Idi Amin (1971-79) na Milton Obote (1980-85). Mafanikio ya Museveni Uganda ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi, utulivu na pia ameweza kusimamisha mapigano ya vikund vya waasi pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ugana.
Museveni amerithi jina lake la katikati kutoka kwa baba yake Amos Kaguta, mfugaji wa ng'ombe. Kaguta pia ni baba wa kaka zake Museveni Caleb Akandwanaho, maarufu anajulikana Uganda kama Salim Saleh na dada yake Violet Kajubiri.
Museveni alisoma Kyamate Elementary School, Mbarara High School na Ntare School. Mwaka 1967, alikwenda University ya Dar es Salaam Tanzania. Kule, alisome economics na siasa ya jamii na akawa Marxist. Alijuhusisha sana na siasa za Umoja wa Africa. Akiwa chuo kikuu alianzisha Umoja wa wanafunzi waleta Mapinduzi wa Kiafrika, shughuli za chama hicho kilipelekea kwenda na ujumbe wake FRELIMO ambayo ilikuwa koloni la Wareno ambayo ni Msumbiji. Kule alipata mafunzo ya kupigana nyikani na mkufunzi wao alikuwa Walter Rodney. Katika insha yake ya kumaliza shule Museveni alitetea (thesis) juu ya uwezo wa hoja za Frantz Fanon katika kuleta vurugu ya mapinduzi ndani ya Afrika huru.