Youtube ni fursa nzuri ya kujiajiri

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,880
6,365
Platform ya Youtube ikitumika vizuri, inaweza kuwa full time job kabisa. Kwa wenzetu Marekani, Uingereza na hata barani Asia, hii (vlogging na blogging) ni kazi mtu kajiajiri kabisa na inalipa vizri sana endapo tu utakuwa serious na namba zako yaani subscribers na views zitakuwa zimeshiba.

Ukiachana na huko mbele, hata majirani zetu kabisa Kenya, Nigeria na South Africa nao naona wanaitumia effectively katika kujiajiri kujitengenezea kipato. Watanzania sijui tunashindwa wapi kuchangamkia fursa, tunaishia kuangalia tu video.

Sifahamu kila kitu kuhusu jinsi ya kutengeneza kipato kupitia Youtube, lakini kwa research niliyofanya, hizi ni baadhi ya njia ambazo unaweza kutumia kujiajiri na ku money off of Youtube:

1. Google Adsense: Without doubt, hii ndio njia maarufu zaidi ya kutengeneza pesa YouTube. Adsense inamilikiwa na Google na kazi yake kuu ni kuwawezesha wafanyabiashara kuweka matangazo yao katika chaneli yako. Kwa lugha nyepesi, Adsense ni dalali ambaye biashar hutumia ili kusaka wateja.

2. Uwakala: Inawezekana kabisa kuingiza kipato kizuri kwa kuwa mshirika au wakala wa makampuni makubwa kutoka duniani kote. Unachotakiwa kufanya ni kuweka link na kuelezea bidhaa husika pamoja na jinsi watu wanavyoweza kuipata. Mtu atanunua bidhaa hiyo kupitia ‘link’ yako, basi utapewa chako.

3. Kuwa Mshauri: Ikitokea una maarifa na unaweza kutoa ushauri then unaweza kujiajiri kwa kuandaa video zenye ubora wa hali ya juu kushauri wafuatiliaji wako. Ukipata credibility unaweza kuanza kucharge fedha katika huduma hizo.

Wanaofahamu zaidi kuhusu hili wanaweza kushare maoni yao pia.

Karibuni.
 
Zoezi la kupata viewers na subscribers kama hujulikani sio la kitoto.
 
mchagger,
Sawa ni maskini ila pamoja na umaskini kaamua akushirikishe ili asije AKAFANIKIWA ukaanza kusema "jamaa mchoyo, hashirikishi wenzake michongo" maana ndio akili zetu wabongo zilivyo!!
 
Kupata Viewer nazani sio swala dogo kabisa lazima ujitoe Ufahamu haswa. Ingawa inawezekana make hakuna kisicho wezekana chini ya Jua
 
Ukijiunga na ads network ya KWANZA lazima uwe na leseni. Leseni utaipata wapi? TCRA baada ya kutoa milion 1 na haijalishi blog yako inahusu nini. Hapa kwa watu wenye blog zenye content za Kiswahili.
Kama content zako ni za elimu/maarifa sidhani kama sheria inakuhusu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom