Yeriko 'Nyerere' apandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka, aachiwa kwa dhamana

Unaweza kufikisha ujumbe wako bila kutumia uongo. Ntashangaa kama kuna watu huwa wanaunga mkono mtu kushawishi kwa misingi ya uongo na ulaghai ingawa mleta uzi ujatuwekea huo uongo alioudanganya huko FB na kumfanya avunje sheria hiyo ya mitandao
Tuna utapia ukweli, ni vigumu sana kwa Mtanzania kuisema kweli yote kwa mtu wa mrengo tofauti naye
 

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Yericko Nyerere amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa Facebook.

Kwa mujibu wa kesi hiyo namba 184, 2017, Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri kuwa mshtakiwa huyo alifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandao Namba 14 ya 2015

Ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye amesaini bondi ya Sh 10milioni.

Kesi imeahirishwa Juni 5, 2017 kusomewa maelezo ya awali (PH)

Chanzo: Mwananchi
Huyu Afungwe Tu Maana Huwa Anatumia Mitandao Vibaya. This Time Hachomoki
 
Huyu Afungwe Tu Maana Huwa Anatumia Mitandao Vibaya. This Time Hachomoki
Mimi huwa namwita mtaalam wa majungu.
Hata kama ni mtu wa upinzani unatakiwa kuwa factually correct
Kuweka na kuandika hisia halafu kutetea hisia hizo zisizo na ukweli mtandaoni ndo kinachompeleka kwa Pilato.

Tumemwonya humu JF lakini naona ni tabia aliyozaliwa nayo.
 
Back
Top Bottom