Yanga, yasema mchezo dhidi ya Simba upo palepale hakuna mabadiliko yoyote

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
953
1,510
Yanga yasema mechi dhidi ya Simba ipo
482084474_1206445090841420_7385920241097743550_n.jpg

TAARIFA KWA UMMA
MACHI 08, 2025​
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa, mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC, uliopangwa kuchezwa leo tarehe 8/3/2025, dhidi ya Simba SC, saa 1:15 usiku upo palepale na hakuna mabadiliko yoyote.

Young Africans SC kama wenyeji wa mchezo, tunaamini taratibu zote za mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni za Ligi Kuu ya NBC, ziko sawa na maandalizi yote yako tayari.

Soma Pia: Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Uongozi wa Young Africans SC utapeleka timu uwanja wa Benjamin Mkapa kama inavyoelekezwa kwenye kanuni, na hatutakuwa tayari kucheza mchezo huu siku nyingine tofauti na leo.

Tunawaalika uwanjani Wanachama, Mashabiki, Wapenzi wa Klabu yetu na Wadau wengine waliosafiri kutoka mikoani, nchi za jirani na sehemu mbalimbali duniani kote kuja kushuhudia mchezo huu mkubwa Barani Afrika.

Imetolewa na Mtendaji Mkuu
Andre Mtine
Young Africans Sports Club
 
CCM Ndio inapenda vijana Wa Tanganyika waweke nguvu zao huko kwenye simba Na YANGA".

Great Thinker
.

Leo Tutaona Nyuzi za Simba na Yanga zaidi ya elfu 60 humu jukwaani.

TUKIWAAMBIA KUSHABIKIA SIMBA NA YANGA NI UPUMBAVU HAMUELEWI
 
Back
Top Bottom