Live coverage on JamiiForums

Sitaki kuamini

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
343
1,021
Ukanda wa Gaza: Makumi ya roketi yarushwa kuelekea Israeli.

Makumi ya roketi yamerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel Jumamosi asubuhi, Oktoba 7, na kusitisha makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyoheshimishwa kwa ujumla tangu kumalizika kwa vita vya siku tano mwezi Mei. Tawi la kijeshi la Hamas limetangaza kuwa limeanzisha operesheni iitwayo "Mafuriko ya Al-Aqsa" dhidi ya Israel.

Ufyatulianaji wa risasi, kuanzia maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza, ulianza kabla ya 6:30 asubuhi saa za Mashariki ya Kati na kuendelea karibu dakika arobaini na tano baadaye.

Nchini Israeli, ving'ora vya onyo vimesikika katika miji kadhaa karibu na Palestina, pia huko Jerusalemu lakini pia ndani zaidi katika eneo hilo, kaskazini na mashariki, kulingana na jeshi.

Roketi imeanguka kwenye mji wa Yavne, kusini mwa Tel Aviv, ambapo mtu mmoja amejeruhiwa kidogo, kulingana na Magen David Adom, sawa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Israel. Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini ameuawa "kwa pigo la moja kwa moja", na watu wengine 15 wamejeruhiwa kusini mwa Israeli, linasema shirika la Magen David Adom.

Jeshi la Israel limeripoti kupenya kwa "idadi isiyojulikana ya magaidi" kwenye ardhi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza. "Wakazi katika maeneo jirani ya Ukanda wa Gaza wametakiwa kusalia nyumbani," jeshi limeongeza.

Mwezi Mei, Israel ilianzisha mashambulizi dhidi ya Islamic Jihad ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha vita vya siku tano kati ya jeshi la Israel, Islamic Jihad na makundi mengine yenye silaha katika eneo hilo, na kugharimu maisha ya Wapalestina 34 na mwanamke mmoja wa Israel.

Zaidi ya roketi elfu moja zimerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel, nyingi zikiwa zimenaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel. Israel kwa upande wake ilikuwa imeongeza mashambulizi ya anga katika eneo hilo dogo.

Hamas, ambayo ilichukua mamlaka huko Gaza mwaka 2007, ilikuwa imejitenga na mzozo huu.

Imechapishwa: 07/10/2023 - 08:13 Na:RFI

Video na TRT AFRIKA

 
Hawa Hamas wanauwezo mdogo sana wa kupambana kijeshi na wayahudi feki wa kizungu, cjui kwanin hawataki kuishi kwa amani.

Kama hii habari niya kweli basi Hamas niwapumbavu tena waoga sana kwa kuua raia wasio na hatia na kushindwa kupambana na wanajeshi wa kiyahudi.

Hapa naona ile hali ya mwaka 2014 inaweza ikajirudia au kuwa mbaya zaidi maana Benjamin Netanyau huwa hacheki na kima. MUNGU awasaidie kwakweli.
 
Hawa Hamas wanauwezo mdogo sana wa kupambana kijeshi na wayahudi feki wa kizungu, cjui kwanin hawataki kuishi kwa amani, Kama hii habari niya kweli basi Hamas niwapumbavu tena waoga sana kwa kuua raia wasio na hatia na kushindwa kupambana na wanajeshi wa kiyahudi. Hapa naona ile hali ya mwaka 2014 inaweza ikajirudia au kuwa mbaya zaidi maana Benjamin Netanyau huwa hacheki na kima. MUNGU awasaidie kwakweli.
Hii ni mbaya sana bora wangetulia vita si vya kukurupuka mtaisha vibaya mno ,raia bora waanze kukimbia kabisa wale wajomba wakianza kurusha yao hawajui huruma ina rangi gani ...
 
Back
Top Bottom