Kauli hii ni rasmi ya serikali:
Ukichanganya na mfano wa kauli kama hizi (kwenye kesi ya Mbowe) zenye kutokea upande wa serikali:
1. Mahakama si mama yako,
2. Waraka wa mshitakiwa kama nyenzo yake kujitetea ni "takataka,"
3. Mtake msitake mawakili wa serikali ni mawakili wa mahakama,
4. Washitakiwa rumande au magereza hawana haki zozote,
5. Washitakiwa hawaruhusiwi kuletewa chakula au chochote cha kunywa isipokuwa jumamosi tu,
6. "Sisi tunaingia mahabusu mpaka ndani kuonana nao, ninyi ni kuwabakia nje."
7. Nk
Kwa hakika ni kauli tata, zenye kukosa staha na zenye kujaa ukakasi kuhusiana na haki za msingi za watu.
Tuko katika mazingira ambayo serikali iko kwenye mvutano na raia wake. Mbaya zaidi serikali inahusishwa moja kwa moja kwenye kunyima watu haki ikiwamo kuwabambikizia kesi na hata hukumu.
Vipi serikali ndani ya sufuria basi itegemewe kututendea haki kina yakhe nje ya sufuria hili?
Hivi ni kweli kuwa wakuu wetu hawa hawaioni hali hii ya kutokuwepo kwa uhalali?
Hivi waheshimiwa hawa wakiwamo Rais Samia, Mpango, Majaliwa, Jaji Mkuu, Spika na wengine wote wanaiona hali hii kuwa ni muafaka kabisa?
Hivi waheshimiwa hawa wanapokuwa wanasali wanategemea kuiona pepo hii hii tunayofunzwa kuiona tukiwa tumemtendea jirani yetu kama ambavyo mtu ungependa kutendewa nafsi yako?
Kwa hakika zikizingatiwa pia kauli kama hizi kwa mustakabala mwema wetu sote, mahusiano mapya baina ya serikali na watu wake ni jambo la dharura sana.
Ama hakika tofauti na hapo tunakoelekea kama jamii, itakuwa ni kudhamiria kupaelekea njia panda, kusikokuwa na tija kwa yeyote.