SoC04 Yanayojiri katika usiku wa kutoa zawadi kwa Washindi wa Shindano la Stories of Change 2024

Tanzania Tuitakayo competition threads

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,228
5,283
Baada ya miezi mitano (5) tangu Msimu wa Nne wa Stories of Change 2024 ulipotangazwa, kuanza na baadaye kufuatiwa mchakato wa Majaji kufanya uhakiki wa Vigezo vilivyowekwa, hatimaye usiku wa leo Septemba 21, 2024, maandiko yaliyoshinda yatatangazwa na Washiriki walioyaandika watakaofanikiwa kujishindia zawadi mbalimbali watafahamika/julikana.

Kuhusu Shindano la Stories of Change
Huu ulikuwa ni Msimu wa Nne wa Shindano la Stories Of Change ambapo Msimu wa kwanza ulikuwa mwaka 2021, Msimu wa pili ulikuwa mwaka 2022 na Msimu wa tatu ulifanyika mwaka 2023. Kama ilivyokuwa katika Misimu mitatu ya Stories of Change iliyopita katika msimu huu wa nne wa Shindano la Stories of Change 2024 Jamii Forums (JF) iliendelea kutoa nafasi kwa wadau wake na Wananchi wote kuwa sehemu ya watu wanaoleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa kushiriki katika shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta tija.

Mwaka huu 2024 Washiriki walishindana kuandika maandiko yanayoonesha na kupendekeza taswira ya Tanzania Tuitakayo kwa kuanzia miaka 5-25 ijayo. Awamu ya nne (2024) ya Shindano hili ilianza Mei 01 mwaka huu na jumla ya Machapisho (1,893) yaliwekwa katika Jukwaa la JamiiForums.com na kupita kwenye Mchujo wa Majaji ambapo leo, Septemba 21, 2024 tutayafahamu Maandiko kumi yaliyoibuka kidedea.

Kaa karibu na uzi huu kufuatilia matukio yanayotokea.

Mgeni rasmi Balozi wa Umoja Wa Nchini Tanzania, Christine Grau, Mkurugenzi wa Asasi ya Jamii Forums, Maxence na Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum tayari wamewasili Ukumbini, Johari Rotana.

Baadhi ya picha zinazoonesha nini kinaendelea kwenye tukio kubwa la Stories Of Change 2024:








Ziada Omary (Meneja Programu JamiiForums) atoa neno la kukaribisha wageni
Meneja programu wa Jamii Forums Ziada Omary amewakaribisha wageni wote waliofika kwenye ukumbi wa Johari Rotana kwa ajili ya kushuhudia tukio kubwa la kuwazawadia washindi wa msimu wa 4 shindano la Stories Of Change.

Kwenye hotuba yake fupi lakini iliyojaa taarifa za kutosha, Ziada amewapongeza wote watakaoshinda usiku wa leo na kuwataka wachukue ushindi huu kama daraja la wao kuweza kusaidia zaidi jamii inayowazunguka.

Mkurugenzi wa Asasi ya Jamii Forums atoa neno


Kwenye hotuba yake, Maxence Melo amewashukuru wote waliojitokeza kushiriki tukio na Stories Of Change 2024 na kuongeza kuwa tukio hili na hafla ya kusheherekea miaka 5 ya JamiiForums tangu kuanzishwa kwake.

"Tunachoenda kukifanya le oni kusherekea mafanikio ya Miaka Mitano ya JamiiForums tukiwa kama Taasisi Isiyo ya Kiserikali, huu nim waka wa Tano wenye mafanikio ambapo tumefanya kazi na Wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri kwa JamiiForums"

"Mwaka huu (2024) kwa mara ya kwanza tutakuwa na Tuzo zikatazotolewa kwa Viongozi ambao wamekuwan wakijitoa na kuwajibika kujibu na kufafanua hoja mbalimbali za Wananchi kupitia njia ya Mtandao"

"Kuna Jukwaa la JamiiCheck ambalo limesababisha JamiiForums kushinda Tuzo ya EU na kutokana na uwezo mkubwa wa kutoa taarifa sahihi na kurekebisha taarifa na Habari ambazo zinakuwa potofu"

"Leo (Septemba 21, 2024) tutakuwa na tuzo ya Kiongozi ambaye amekuwa akijitoa na kushirikiana na Wanahabari, Wananchi katika kujibu hoja muda wote anapotafutwa bila kujali ni usiku au Mchana"

"JamiiForums imekuwa ikitoa mafundisho ya kuwajengea uwezo kwa Wadau wote wanaozalisha maudhui ili kuwa na ufahamu kuhusu uwezo wa kutambua taarifa sahihi na zisizosahihi kama Jukwaa la JamiiCheck linavyofanya"

"Wakati tunafanya utAFITI Mwaka 2020, tukiwa Zanzibar, tulipata wazo la kuanzisha Shindano ambalo litawawezesha Watu kuandika maandiko ambayo yanaweza kuwa na faida kwa JamiiLeo hii tutawatunza Washindi wa Shindano la Stories of Change kwa kushirikiana na Wadau wakiwemo TAKUKURU, ZAECA, WAJIBU"



Balozi Wa Sweden Nchini Tanzania, Charlotta Ozaki Macias atoa neno


Akiongea katika halfa ya Tuzo za Shindano la Stories of Change, Balozi wa Sweden, Charlotta Ozaki amesema amefurahi kuwa mmoja wa Washiriki Tuzo za Shindano hilo, kwasababu stori zinazoandikwa zinakuwa na ujumbe mzito kwa jamii ambao unaweza kuwa sehemu ya kufanyika kwa mabadiliko

Balozi Ozaki Amesema:

"Naipongeza JamiiForums kwa tukio hili, simaanishi kuwa bila wao stori hizi zisingekuwa hewani, lakini wao wamekuwa na nguvu na wazo la kuyakusanya Mawazo ya Waandishi na kuyafikisha katika njia iliyo sahihi"

"Pia nakupongeza Maxence kwa kuiongoza JamiiForums, umekuwa mstari wa mbele katika mabadiliko na hata haya mabadiliko yanayoenda kutokea kutokana na maandiko ya Washiriki wewe ndio umechangia"

""Nilipopata mwaliko wa tukio hili, nilifikiria kuhusu kazi kubwa ambayo imefanywa na JamiiForums kwa kushirikiana na Wadau wao wakiwemo WAJIBU, TWAWEZA, UTPC na wengine"


Balozi wa Umoja Wa Ulaya (EU) atoa neno

"Suala la taarifa potofu ni jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi na limekuwa changamoto, kwanini elimu ya suala hilo ni muhimu kwetu? Ni kwa kuwa kumekuwa na taarifa nyingi za Demokrasia"

"Kuhusu tukio la leo, napongeza JamiiForums kwa jinsi iliyobuni tukio kama hili, mmekuwa na ubunifu katika kuhakiukisha upatikanaji w ataarifa sahihi"

"Kuwa na taarifa sahihi ni haki ya Msingi ya Mwananchi na JamiiForums imekuwa ikifanya uhakiki wa taarifa na hiyo inatengeneza usalama katika Mtandao kutokana na upatikanaji wa taarifa sahihi"


Baadhi ya taasisi zilizoshinda tuzo usiku wa leo ni:

1. SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TANESCO ni moja ya Taasisi zilizojisajili ndani ya JamiiForums.com na ‘Akaunti’ yao imekuwa ‘hai’ katika utoaji wa taarifa mbalimbali

JamiiForums.com imetumika kama daraja la kusikilizana, kuwasilisha hoja, mijadala, maoni na changamoto zinazohusu huduma hiyo kati ya Wananchi na Shirika husika

Kutokana na Uwajibikaji huo, JamiiForums inathamini mchango wa TANESCO katika kujibu, kufafanua na kufanyia kazi hoja na kero za Wadau ambao wamekuwa wakiwasilisha maandiko yao kupitia majukwaa mbalimbali ya JamiiForums.com

2. MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA DAR ES SALAAM (DAWASA)

Jaribu kufikiria Maisha ya Mwanadamu, Mimea na Viumbe hai wote bila Maji. Ni jambo ambalo haliwezekana ndio maana Huduma ya Maji inapokuwa na changamoto hata kwa udogo ni rahisi kubainika

Hapo ndipo umuhimu wa mamlaka za Maji unapoonekana, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ni moja ya Taasisi inayowajibika kujibu, kufafanua, kuelezea hoja zinazoanzishwa na Wananchi Mtandaoni

JamiiForums inathamini mchango DAWASA inaouonesha katika Ulimwengu wa Kidigitali kupitia majukwaa mbalimbali ya JamiiForums.com

3. WIZARA YA MAJI

Wizara ya Maji ni Mamlaka ambayo inafuatilia kwa ukaribu kile kinachoendelea kwenye Ulimwengu wa Kidigitali na kisha inatumia nafasi hiyo kuwa na uhusiano wa karibu na jamii, ikisaidia kutatua changamoto zao kwa haraka

Mara kadhaa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Timu yake wamechukua hoja za Mtandaoni na kuzifanyia kazi, kwa msingi huo JamiiForums inathamini mchango wa Mamlaka hiyo kwa kile inachokifanya

4. MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANANYAMAPORI TANZANIA (TAWA)

Mamlaka ya Usimamizi wa Wananyamapori Tanzania (TAWA) ni moja ya Mamlaka inayojihusisha na masuala ya Wanyama ambayo imekuwa na ukaribu na Jamii katika kutoa ufafanuzi wa masuala kadhaa

Mbali na ufafanuzi, TAWA imekuwa Mdau mzuri wa kutoa ufafanuzi wa masuala ya uhakiki wa taarifa za Wanyama, kwa msingi huo pia TAWA mara kadhaa imekuwa sehemu ya Wadau wanaofafanua hoja zinazohusu Wanyaka kupitia Jukwaa la JamiiCheck.com

JamiiForums inathamini hicho kinachofanywa na TAWA kwa kuwa Mdau mzuri wa masuala ya Kidigitali

5. HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

Manispaa ya Ubungo imejiweka karibu na Jamii, hasa katika Sekta ya Usafiri, Mamlaka hiyo imejibu mara kadhaa kuhusu kero za Kituo cha Mabasi cha Magufuli (Magufuli Bus Terminal), ikiwemo ya hivi karibuni kuhusu changamoto ya kukosekana kwa maji kituoni hapo

Manispaa hiyo imelazimika pia kujibu kuhusu hoja kadhaa za Wadau wa JamiiForums.com

JamiiForums inathamini jitihada zote zinazofanywa na Manispaa hiyo katika kuwa karibu na Wananchi hasa wale wa kawaida

6. CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

UDOM ni moja ya Vyuo ambavyo vimekuwa vikitajwa mara nyingi katika Majukwaa ya JamiiForums.com, baadhi ya hoja zilizotajwa hazikuwa nzuri katika macho ya Jamii lakini kwa ujasiri mkubwa Uongozi wa UDOM ulijitokeza na kuzijibu

Wasomi wengi wa Chuo hicho ni Vijana na ndio ambao wanatumia muda mwingi kuwa Mitandaoni, hivyo kitendo cha UDOM kuwa huru kujibu hoja zao mbalimbali kinastahili pongezi

JamiiForums.com inathamini kile kinachofanywa na UDOM kwa kuwa ni sehemu ya Uwajibikaji

7. SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC)

Moja ya Mashirika ambayo kwa wakati huu yamekuwa gumzo kutokana na huduma zake kutajwa mara nyingi ni Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Bila hofu wala kusitasita, TRC imekuwa ikijitokeza na kujibu hoja za Wadau wengi wa Mtandaoni wakiwemo wale wa JamiiForums.com

JamiiForums inashukuru TRC kwa kuwajibika na kuwa karibu na Wateja wao wanaofikisha ujumbe kwa njia ya Mtandao

8. BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI YA MAZINGIRA (NEMC)

Suala la kushughulikia matatizo kama kelele za Sauti, uondoaji wa taka na harufu za Kemikali na mengine ya aina hiyo, yamekuwa yakijibiwa na kutolewa ufafanuzi na Baraza la Usimamizi wa Mazingira la Taifa (NEMC)

JamiiForums inathamini jitihada hizo za Mamlaka hiyo ya Mazingira

9. WIZARA YA ARDHI

Baadhi ya hoja za Mtandaoni zimekuwa zikijibiwa na hata kuchukuliwa na Wizara ya Ardhi, mfano Nyumba zaidi ya 400 eneo la Mapinga (Bagamoyo) zilikuwa hatarini kubomolewa. Kupitia ushawishi wa Mtandao, Waziri wa Ardhi akafika eneo la tukio na kutatua changamoto hiyo.

JamiiForums inatambua na kuthamini mchango huo wa Mamlaka hiyo ambayo imekuwa ikifanya kazi na Wananchi kwa ukaribu kila siku

10. TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU)

TAKUKURU imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na JamiiForums katika kushughulikia masuala ya rushwa yanayoibuliwa na wananchi kupitia Jukwaa la Fichuo Uovu.

Kwa kutambua jitihada hizi, JamiiForums imeamua kuipa tuzo kwa mchango wake katika kupambana na rushwa na kuimarisha uwazi nchini.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorothy Gwajima Ashinda Tuzo


Waziri Dorothy Gwajima ni Mwanachama hai wa JamiiForums.com amekuwa mstari wa mbele kujibu na kufafanua hoja nyingi zilizo chini ya Mamlaka yake.

Zile za Mamlaka nyingine amekuwa akichangia mada iwe ni kwa kutoa maoni au kufikisha hoja kwa Mamlaka inayohusika.

Kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Gwajima amekuwa mstari wa mbele kulaani ukatili, pia ameshiriki katika mijadala au kutoa maoni kwenye Mitandao ya Kijamii na hivyo kuwa ni rafiki wa wananchi wengi wanaotumia Mitandao.

JamiiForums inathamini mchango wake hasa anaoutoa kwa wale wanaohitaji msaada wa masuala ya Kijamii, ameonesha uongozi kwa vitendo na hilo limemfanya kuwa Kiongozi anayajua kipi ambacho Dunia ya Digitali inahitaji

Waziri Gwajima atoa neno

'Naona Fahari kwa kuwa fursa hii ya kuhudumia Jamii. Tuzo hii niliyopewa na JamiiForums inakuwa kama chachu kwangu na kwa Idara yangu Pamoja na wengine wote tunaofanya kazi pamoja, ni wajibu wetu kama Viongozi kujibu hoja za Wananchi"

"Ni jambo gumu kujibu hoja za Wadau mbalimbali Mtandaoni lakini uvumilivu na kuelewa vinanifanya nakuwa na nguvu ya kuendelea kutimiza wajibu


Washindi wa Stories of change 2024
Mshindi namba 10 ni Nimechoka Sana

Nimechoka Sana (Jina analotumia JamiiForums.com) kupitia andiko lake lililosema 'Tanzania yenye kiwango kidogo cha Usugu wa Vimelea vya Magonjwa Dhidi ya Dawa (UVIMADA) ifikapo Mwaka 2035' ameibuka Mshindi wa Kumi na kujinyakulia Tsh. 500,000
-
Nimechoka Sana anashauri Mamlaka zihakikishe zinadhibiti Magonjwa yanayosababishwa na Bakteria kwa kusambaza huduma za Maji Safi na Salama, Kuwe na kampeni za Afya na Usafi wa Mazingira, Elimu ya kudhibiti Magonjwa yanayochangia utumiaji mkubwa wa Antibayotiki pamoja na matumizi sahihi ya Dawa

Andiko lililompa ushindi: Tanzania yenye kiwango kidogo cha Usugu wa Vimelea vya Magonjwa Dhidi ya Dawa (UVIMADA) ifikapo Mwaka 2035

Mshindi namba 9 ni Charles Malale

Charles Malale kupitia andiko lake lililosema 'Tanzania mpya yenye matumizi bora ya Nishati ya Gesi Asilia' ameibuka Mshindi wa Tisa na kujinyakulia Tsh. 500,000

Charles alishauri kuanzishwa kwa Tume Maalum ya kusimamia Gesi Asilia, kuweka Magari Maalum ya Usambazaji wa Gesi Nchini kwa haraka na urahisi, kuwekeza zaidi kwenye kuwa na Wataalamu wenye uzoefu ili kuhakikisha Usalama na Ufanisi wa mfumo huu.

Charles ameshinda Tsh.500,000

Andiko lake lililoshinda: Tanzania mpya yenye matumizi bora ya nishati ya gesi asilia

Mshindi wa 8 ni Pius Singu Chaba

Pius Singu Chaba kupitia andiko lake lilisemalo 'Tanzania we want, the one with effective and functional pre hospital care system leading to minimal lives loss due road traffic accidents' ameibuka Mshindi wa Nane na kujinyakulia Tsh. 500,000
Pius anapendekeza kuanziswa Mfumo wa Huduma Bora za Dharura kwa Majeruhi kabla ya kufikishwa Hospitali kupitia Uokoaji utakaofanywa na Madereva wa Vyombo vya Moto na Jamii

Mshindi wa 7 ni Constantine Mauki

Constantine Mauki kuptia andiko lale lililosema 'Mashine za EFD Zitolewe BURE kwa Wafanyabiashara Ili Iongeze Wigo wa Walipa Kodi' ameibuka Mshindi wa Saba na kujinyakulia Tsh. 500,000

Constantine anaeleza kuwa Serikali ikiweka mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara hasa Wadogo kwa kuwapa EFD itawasaidia waendelee kukua bila mzigo wa gharama za ziada na kuwabadilisha mtazamo juu ya ulipaji Kodi kuwa ni kitu cha kawaida na muhimu.

Mshindi wa 6 ni Conrad Masoro

Conrad Masoro kupitia andiko lake lililosema 'Matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa' ameibuka Mshindi wa Sita na kujinyakulia Tsh. 500,000

Conrad anasema upigaji Kura usiohusisha Makaratasi unaongeza Usalama wa Kura na Wapiga Kura wenyewe kwa kuepuka mikusanyiko inayoweza kusababisha Vurugu au Magonjwa ya milipuko, kupunguza muda wa Kuhesabu Kura na Kuhifadhi Mazingira

Mshindi wa 5 ni ANGYELILE99 (Jina analotumia Ndani ya JamiiForums.com)

ANGYELILE99 (Jina analotumia Ndani ya JamiiForums.com) kupitia andiko lake lililosema 'Serikali iweke mpango wa uanzishwaji wa Lugha ya Alama kwa Shule zote Nchini' ameibuka Mshindi wa Tano na kujinyakulia Tsh. 1,000,000

Angyelile99 anasema kuanzishwa kwa Elimu hiyo mashuleni kutachochea fursa sawa, kuimarisha mawasiliano na kuleta mshikamano katika Jamii. Pia, kutasaidia katika kujenga kizazi kinachoheshimu na kuthamini tofauti zilizopo katika Makundi ya Watu na hali zao na kikiongeza uelewa na ujuzi wa lugha

Mshindi wa 4 ni Novart Idapo

Novart Idapo kupitia andiko lake lililosema 'Kutumia mfumo wa kielektroniki ili kuboresha huduma za NHIF' ameibuka Mshindi wa Nne na kujinyakulia Tsh. 2,000,000

Novart alishauri kuwa Kadi za NHIF ziboreshwe kwa kuwekwa 'Chip' ambayo itafanya kazi kwa kutumia Mashine za Kielektroniki mfano wa ATM ambapo Mgonjwa ataweza kuhakiki mwenyewe Kadi yake na kuendelea na matibabu. Pia, Kadi itakuwa na taarifa zote za Matibabu na pia iwepo 'App' itakayomsaidia Mgonjwa kufuatilia Afya yake kwa urahisi.

Mshindi wa 3 ni Frank Nyachuma

Frank Nyachuma kupitia andiko lake lililosema 'Mfumo wa E-Afya kwa Taifa lenye Afya Aora' ameibuka Mshindi wa Tatu na kujinyakulia Tsh. 3,000,000

Frank anasema e-Afya itarahisisha mawasiliano kati ya Wagonjwa na Watoa Huduma kwa njia ya Kielektroniki ikiwemo kuhifadhi kumbukumbu zote Matibabu katika Kanzidata ambayo Mgonjwa ataweka utambulisho wake katika Hospitali yoyote na hivyo kupunguza muda wa kusubiri huduma na kuongeza ufanisi wa matibabu

Mshindi wa 2 ni Magreth Joseph

Magreth Joseph kupitia andiko lake lililosema 'Kuundwa kwa Kanzidata ya Vyeti vya Elimu vya Kidijitali: Maboresho ya utunzaji wa taarifa za kitaaluma' ameibuka Mshindi wa Pili na kujinyakulia Tsh. 4,000,000

Mageth anasema Mfumo huu utaunganishwa na Taasisi na Mashirika yanayoajiri yakiwemo ya Serikali, Sekta Binafsi na Mashirika kwa kuwa ni muhimu Nyaraka na Vyeti vya wahusika ziunganishwe kwenye Kanzidata moja ambapo Waajiri na Waomba Kazi wataweza kuona Nyaraka zao kwa urahisi, lengo likiwa ni kutunza kumbukumbu na kulinda ithibati ya vyeti.

Mshindi wa 1 ni Nurdin R. Almas


Nurdin R. Almas kupitia andiko lake lililohusu 'Uboreshaji wa Huduma za Maji Safi na Salama yaliyosafishwa kutoka Maji Machafu kwa kutumia Nishati ya Jua' ameibuka Mshindi wa Kwanza na kujinyakulia Tsh. 7,000,000

Nurdin anasema Mfumo huu utatumia Paneli za Sola kugeuza Miale ya Jua kuwa Umeme utakaoendesha Pampu za kuvuta Maji kutoka vyanzo mbalimbali na kuyasafisha kwa Teknolojia kama Reverse Osmosis (RO) ambayo hutumia utando maalum kuondoa Uchafu, Chumvi na Kemikali mbalimbali kwenye Maji.
 

Attachments

  • Mshindi Takukuru.jpg
    841.8 KB · Views: 15
  • Mshindi Takukuru.jpg
    841.8 KB · Views: 19
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…