HKBW
JF-Expert Member
- Aug 4, 2009
- 468
- 342
Ni jipu sugu, Bora litumbuliwe tu. Naomba jinsi Magu anavyoanza kupoteza sita kutokana na huyu jamaa. Tangu hili jambo la bunge lilivyoanza kuibuka Magu nae anaanza kufifia na kufanya mambo kwa kukurupuka. Walianza vyema, ila wameshaanza kupoteza dira.Niliwahi kusema, Nape Nnauye lazima abadilike. Uwaziri si kazi ya uenezi wa chama
Kuhusu Bunge live, sasa hivi anababaika baada ya jamii kuwa dhidi yake
Nape aliongopea jamii gharama ni kubwa. Bila hesabu akataja kiasi ambacho mfuko wa Wakfu ukaamua kulipia. Nape ''akakataa'' Wakfu isigharamie matangazo akijua kabisa alichosema ni uongo! na nia si kupunguza gharama, ni kuficha uovu na maovu
Kabadili kauli , wananchi wapo makazini hawatakiwi kuangalia TV.
Huyu ni kijana,hakuwahi kuishi zama hizo tunazozijua.
Nape anapangia watu muda wa kuangalia TV.
Anasema wanabana matumizi, wakati TV zipo 24 hrs zikionyesha Isidingo n.k
Nape kadai wananchi wengi wanaagalia vipindi jioni, hakutupa utafiti huo aliufanya lini na kwa njia gani hadi kupata takwimu zinazoitwa 'wengi'
Sasa hivi anasema suala linajadilika, wakati hakutaka kulijadili kwasababu aliamini katika FFU na Polisi kutekeleza azma zake na wenzake wa CCM, kuficha maouvu
Leo anataka kubadili msimamo kwasababu ametambua UMMA upo against yeye na CCM, na hilo ni andiko la kwanza la anguko la Nape.
Atakuwa waziri lakini tayari ameshapoteza public trust!
Tayari umma unamuona kama tatizo na akae akijua Umma unamwangalia kwa jicho baya
Nape asibadili msimamo kuhusu kuzuia matangazo maana haitamsaidia!
Tayari kabeba mzigo iwe ni yeye au kwa kutumwa.
Hili keshalibeba, asigeuke nyuma maana hatabadili mtazamo wa Jamii dhidi yake!