Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,662
- 8,787
Kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3 inaendelea mahakamani leo Novemba 30, 2021
=======
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa, Naomba tupatiwe Nyaraka ilikuweza Kuzikagua.
Wamekabidhiwa Nyaraka na Kuanza Kukagua Moja baada ya Nyingine.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Tuna mapingamizi Kuhusiana na Upokelewaji Wa Nyaraka hizo Nne Zinazotaka Kutolewa na Shahidi Wa Pili Mheshimiwa Jaji tumeandaa Mapingamizi ngamizi ifuatavyo.
Vilivyotakiwa katika Vifungu Vya 65, 66, na 67 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya Sita.
Mheshimiwa Jaji Kuhusiana na Dispatch, Shahidi aliyepo Mahakamani siyo Competent Witness Kuweza Kuitoa hiyo Dispatch.. Mheshimiwa Jaji sisi tupo tayari Kuendelea na Hizo Hoja zetu za Kisheria kwa maana Kufanya Submission na ataanza Pius Hilla..
Jaji: Kwa hiyo ni Mapingamizi Matatu
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Nyaraka ambazo Wenzetu Wanataka Kutender Kwenye Ushahidi..
Jaji: Hapo unamaanisha Dispatch?
Wakili wa Serikali: KUHUSU RELEVANCE Nyaraka Wanazotaka Kutumbukiza Kwenye Ushahidi Barua, Proceedings, na Charge sheet
Wakili wa Serikali: Nyaraka hazina Indicator Zozote kama D/C Msemwa aliwahi Kufanya Kazi Kituo cha Polisi Oysterbay kipindi cha Mwezi May 2020, Nyaraka hizi pia hazina Bearing yoyote ile za Ukamatwaji Wa Ling'wenya, Uandikaji wa Maelezo Ya Ling'wenya, Mambo ambayo Ndiyo Issue Iliyopo Mbele Yako
Nyaraka hizi pia Mheshimiwa Jaji hazina Bearing yoyote ile Kwamba Lembrus MCHOME (DW2) Kuwa amewahi Kukaa Kituo cha Police Oysterbay.
Mheshimiwa Jaji Jaji Kwa Mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, Kwamba Ushahidi Mheshimiwa Jaji, Utatolewa na Kupokelewa Mahakamani Kama Upo Relevant, na wala sio vinginevyo.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mahakama Yako hii inaongozwa na Sheria, Kwamba Kila Kinachofanyika Mahakamani lazima Kifanyike Kwa Mujibu wa Sheria.. Kila kitakachopokelewa lazima Kiwe na connection (Uhusiano)
Mheshimiwa Jaji Kesi ya DPP VS SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHERS Criminal appeal namba 74 ya Mwaka 2016 katika Ukurasa Wa 6 Aya ya Mwisho Mahakama Ya Rufaa Ilipata Kusema Kwamba, Ushahidi ambao ni Irrelevant ni inadmissible
Mheshimiwa Jaji Page ya 7 ya Hukumu hiyo paragraph Ya Kwanza, Mahakama Ya Rufani Inasema Kwamba fact inakuwa Relevant kama Inakusudia Ku Prove au Ku disaprove Ushahidi, Bila Kuzingatia hayo Mahakama Ingaletewa Mambo Mengi ya siyo Ya Msingi.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mahakama Inapaswa Kuletewa Mambo ambayo ni Relevant.
Mheshimiwa Jaji Barua inayo taka Kuletwa Mahakamani inatoka TANAFRICA LAW imesainiwa na Wakili Peter Kibatala Imeelekezwa kwa Hakimu Mkazi Kisutu imenakiliwa kwa Lembrus MCHOME na Kwa Deputy Registar wa pale Oysterbay Police.. Mheshimiwa Jaji Charge Sheet na Proceedings Zinahusiana na Mashtaka, Publication of photographs. Shahidi aliyepo Mahakamani alikamatwa kwa Kupigwa Picha Fulani Kwa Kiongozi Fulani akashtakiwa Kwa Matumizi Mabovu ya Mtandao.
Mheshimiwa Jaji Swali la Kujiuliza ni Je Shauri hili lina Uhusiano gani na Matumizi Mabovu ya Mtandao, Yana Uhusiano gani wa Kupiga Picha Kiongozi Fulani au Taasisi fulani.. Mashtaka haya ya Publication of Photograph Yana Uhusiano gani na D/C Msemwa Kuwepo Oysterbay police?
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Nyaraka zinatakiwa kujiongelea Zenyewe, Ni Wasilisho letu Kwamba Nyaraka hizi haziongelea Chochote Kuhusiana na Ishu iliyopo Mahakamani, Nyaraka zinaongelea Vitu Vingine kabisa, Nyaraka hazina Uhusiano na Ukamataji na Uchukuliwaji wa maelezo ya Ling'wenya
Alitakiwa aieleze Mahakama Yako Tukufu Kwenye Hizo Nyaraka Kuna Moja Mbili Tatu Kuhusiana na D/C Msemwa, Mheshimiwa Jaji Shahidi alijaribu Kueleza Mahakama Yako tukufu Kwamba alikaa na Msemwa Kwa Muda, Hicho siyo Kigezo Cha Kuleta Hizo Nyaraka.
Nyaraka zilitakiwa zijitambulishe Zenyenwe na Shahidi aongee Kuzitambulisha, Kwa Kifupi pasipo Kuichosha Mahakama Yako tukufu Nyaraka hizi ni Irrelevant, Hazina Sifa za Kupokelewa, Kwamba Kitendo Cha Shahidi Kutokuongelea ni Kitu gani kwenye Nyaraka Kinahusiana na D/C Msemwa
Wakili wa Serikali: Inabainisha Kwamba Wala Hana Knowledge Ya Kile Kilichopo Katika hii Nyaraka, Mheshimiwa Jaji nizungumzie Sasa Kuhusiana na Charge Kuwa Nakala, Mheshimiwa Jaji Kinacholetwa Mbele Yako Hakuna Ubishi it's a photo Copy.
Tunasema Hakuna Ubishi Kwa Sababu Shahidi Mwenyewe Alianza Kwa Kusema Hivyo, Rules of Evidence zinademand Kufuatwa Kwa Procedures ili Kuleta Ushahidi, Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho Letu kuwa Nyaraka hii Imeletwa kwenye Violation.
Ni Violation ya kifungu cha 63 - 66 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, Kwamba Kwakuwa Walifahamu Kwamba Nyaraka ni Photocopy (Secondary) Walitakiwa Mheshimiwa Jaji Wa Comply na Masharti.. Mheshimiwa Jaji Ushahidi Ambao ni Photocopy (Secondary) it's a General Rule Kuwa ni Admissible.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji baada ya Kusema hayo naomba Wakili Mwenzangu Abdallah Chavula aendelee pale Nilipo Ishia, atakuja kwa suala la Dispatch.
Mheshimiwa Jaji ni Kama alivyotanguliq Kusema Mwenzangu, Nitaanzia Hapa Alipoishia Yeye.
Na Yeye Aliishia Kwamba hii Hati ya Mashtaka Imekiuka Kifungu namba 63 Mpaka 66.. Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 63 kimatoa Ruhusa kwa Nyaraka kwa namna mbili.. Kwa primary Evidence na Secondary Evidence.
Na Kifungu ha 64 kimeweka Bayana Kwamba Primary ni Documents, Mheshimiwa Jaji Shahidi akaweka Bayana kwamba alipewa Photocopy. Kwa hiyo siyo Primary Evidence, Kwa Maana hiyo anataka Kuijulisha Mahakama Hii ni secondary Evidence.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 65 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, kinasema kwamba ANASOMA.. (a), (b) (C), (d), na (e).. Mheshimiwa Jaji Katika Ushahidi Wake hajaeleza Mahakama Kwamba Nyaraka hii Imekuwa Certified na Ukatazama Nyaraka Yenyewe Pia Hazijawa Certified
Shahidi hajaeleza Mahakama Kwamba Nyaraka hii Imetengenezwa Kutoka Kwenye Nyaraka, Hajaileleza Mahakama Mheshimiwa Jaji Kwamba Baada Ya Kufanyiwa Photocopy Wali linganisha Kujiridhisha Kwamba Kilichopo humu ndiyo Kipo kwa Original Charge Sheet
Vilevile Hajaelezea Kwa mdomo Kwamba hii ni sehemu ya Ile Original Document. Mheshimiwa Jaji Ni Hoja yetu Kwamba Shahidi huyu wakati wa Kuomba Kutoa Nyaraka Hajakidhi Matakwa ya Kifungu cha 65.
Wakili wa Serikali: Twende Mbele zaidi, Fungu la 67 liinaweka Masharti Kwamba Secondary Evidence Inapaswa Kutolewa Mahakamani. Ni Maoni yetu Siye kwa Madai Ya Kwamba Eti Kule Mahakamani Kisutu Kwamba walielezwa Nyaraka Ya Mashtaka ipo Moja tu, Kwa Bahati Mbayo siyo Sababu Iliyo Tajwa Kisheria
Kuleta Nyaraka hiyo.. Ni Maoni yetu Vigezo Vilivyomo Katika Kifungu cha 65 vinakosekana kwa Ushahidi na Shahidi Mwenyewe. Na hii ya Kupewa Photocopy Haikamiilishi Kifungu. Kifungu Cha 68 Kinachotaka Wao Ku Introduce hiyo Document na Wao hawakufanya.
Na Kwa Sababu HawaKutumia hiyo nafasi, Basi Maombi yao yanakuwa Batili Mbele ya Mahakama hii. Mheshimiwa Jaji naomba tuelekee Kwenye Pingamizi La Dispatch.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni Msimamo Wa Sheria na Katika Nyakati tofauti Tofauti Tumekuwa tulielekeza Mahakama Yako Kwenye Shauri la JAMHURI Vs CHARLES GAZILABO NA WENZAKE Katika Ukurasa Wa 12, Na Pia Kesi ya DPP VS MIZIRAHI
Mheshimiwa Jaji hapa Kuna suala la Knowledge, Ilikuwa ni Lazima Kuonyesha Mahakama Kwamba alishawahi Kumiliki Kielelezo hiki. Sisi ni Maoni yetu Kwamba Kuna Eneo Muhimu Sana ambalo tunaona ni lazima Mahakama itambue.
Wakati anaeleza Kuhusu Barua, alieleza Barua ile Ina Reference namba, Mheshimiwa Jaji Shahidi a Kwenda Mbele na Kutuambia hizo Reference Nmab ni zipi.. Ni Maoni yetu Kwamba Shahidi ameshindwa Kunukuu Reference namba za Barua ambazo yeye Anadai Kwamba hazikamiliki.
Wakili wa Serikali: Ni Maoni yetu Kwamba Shahidi hana Knowledge ya Kielelezo ambacho anataka Kukitoa. Na Vilevile Kwamba Kielelezo hicho Hakina Uhusiano na Kesi iliyopo Mahakamani.
Nashon Nkungu: OBJECTION Mheshimiwa Jaji tungejikita na P. O zile tatu naona hii ni P. O Mpya Na Yalifanyika Tarehe 23 November Mwaka huu, na Yeye alikuja Tarehe 24 November 2021, Hakuna Sehemu alitaka Kwamba FAITH Alimkabidhi Dispatch, Lakini hajaileleza Mahakama Kwa Namna alivyo Kihifadhi Kielelezo Hicho Haja eleza Mahakama Kwamba Mpaka anafika hapa Kielelezo hicho Kilivyo kuwa wapi na Kilikuwa kinatunza kwa namna gani, Naomba Niezekee Mahakama Yako Kwenye Kesi Ya DPP Vs SHARIF MOHAMMED ATHUMAN na Wenzake
Wakili JOHN MALLYA: OBJECTION naona Wakili analeta Jambo Jipya, Sababu Hapa P.O ilikuwa ni Kuhusu Competence ya Shahidi Juu ya Kielelezo..
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji nafikiri Wakili angetulia kwanza anisikilize na Mahakama Yako iniachie nafasi Nionyeshe Natokea wapi..
Kufungua Bonet ilioneshe Ushahidi Wake.. Na Wakati Wa Ushahidi Wale alisema Anatokea Himo wakati Gari Ipo Moshi Ndiyo zikatokea Hizo Issue.. Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Shahidi Ilikuonyesha Kwamba Alilipata wapi Kielelezo na alikaa nacho ilikuweza kukileta Kielelezo hilo hakufanya na wala Hakuileza Mahakama Hiki Kielelezo alikabidhiwa na nani, Ni Hoja yetu Kwamba Kukosekana Kwa Ushahidi huo, Kwa hayo tuliyoyaeleza ni Maoni yetu Kwamba Kielelezo Hiki (Dispatch) haiwezi Kupokelewa, Mheshimiwa Jaji naomba Kumalizia Kwa Kurejea kwenye Hati ya Mashtaka
Wakili wa Serikali: Hati ya Mashtaka ina walakini na Ushahidi Wa shahidi, Pale anaposema alikamatwa na Kufunguliwa Mashtaka kwa Makosa aliyofanya Wilaya ya Mwanga, Hati anayotaka Kuleta Yeye inaongelea Makosa Yaliyofanyika Dar es Salaam.
Hakuna Sehemu aliyoweza Kulinganisha Kosa alilofanya Wilaya ya Mwanga na Makosa aliyoshtakiwa Dar es Salaam, Haya yote Kwa Ujumla hayana Sifa Ya Kupokelewa na Mahakama hii, Ni Maoni yetu Kwamba Katika Mazingira haya Tunaomba Mahakama Isipokee Vielelezo hivyo.
Jaji: Mmemaliza..?
Wakili wa Serikali: Ndiyo
Jaji: Nakukumbusha Wakili Nashon Nkungu Kwenye Sababu Zako Za Kuunga Mkono Usijibu Hoja ambazo zimetolewa na Upande Wa Mashtaka.
Nashon Nkungu: Sawa Mheshimiwa Jaji, Ingawa napata Ugumu, Naomba Mahakama inivumilie naona Hoja Nyingi Zinakuwa against na Hoja zao
JAJI: Ndiyo Changamoto tunazopata eneo hili
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naomba Kuwakumbusha Kwamba Siyo Haki yao Kujibu, Huyu siyo Mtu aliyeleta Motion.
Jaji: Nakukumbusha Mr. Hila Kwamba Hilo siyo Jambo Jipya, nimemkumbusha Kwa sababu Hakuwepo Mahakamani
Nashon Nkungu: Mhe Jaji Naunga Mkono Upokelewaji wa Vidhibiti hivi Kwa Pamoja kwa sababu Nimeona vimekidhi Matakwa Makubwa 3 ambayo ni RELEVANCE, MATERIALITY na COMPETENCE
Nashon Nkungu: Kabla Sijaenda Kwa Haraka Haraka kwenye Proceedings Za Mahakama hii, Lakini niliona ina Case Namba, Ina jina la Mshtakiwa,
Jaji: Hiyo ni Nyaraka gani
Nashon Nkungu: Court Proceedings
Nashon Nkungu: Pia Nikihamia Kwenye Charge sheet, Sitoenda Kwenye Content nitajikita Hasa Maeneo alisema ni Copy, Nimeona kweli ni Copy Nimeona namba ya Kesi namba 77/2020 na Relevance InaKuja Kwa sababu akishatueleza Kwamba alipelekewa Oysterbay na Kwa kutumia Charg Sheet hii alipelekewa Mahakama ya Kisutu. Kwa Suala la Relevance Kwa Mujibu Wa Kifungu cha...
Wakili wa Serikali: OBJECTION Mheshimiwa Jaji anachokifanya Wakili anajibu....
Jaji: Mr. Hila anachokisema Unaenda Ndani Sana
Nashon Nkungu: Sawa Mheshimiwa Jaji, Kingine Kinachonifanya niunge Mkono ni Kesi ya DPP VS MIZIRAHI Ukurasa wa 8,
Jaji: Wewe Unayo hiyo Nakala ya MIZIRAHI Kwa Maana Nakumbuka Inachukuliwa na kutoka. Kwenye kesi ya ABEL GAZILABO.
Nashon Nkungu: Mimi ninayo tutawapatia pia, Nimeona Kwenye kesi hii Inasisitiza Knowledge Wala Siyo Sufficient Knowledge. Kwa hayo Machache, Naomba Sababu za Kuunga Mkono Zichukuliwe.
Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji Nitaongea kwa Kifupi Sana na Kwa Bahati Nzuri sikuwa nawasikiliza Upande wa Mashtaka. Suala la Kwanza la Barua Naona Lazima Barua Isomwe na Charge Sheet na Proceedings kwa hiyo Barua ni Relevant.
Mallya: Zaidi Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 8 cha Sheria Ya Ushahidi, Kwamba Matters ambazo zipo Connected at anytime zinaweza kuibuliwa, Shahidi alieleza Ni Muda gani Kila Nyaraka aliiimiliki, kwa Madhumuni gani na alishughulikia Vipi, kwa Hiyo naona ni Shahidi Competent!
Mallya: Kwa sababu hiyo tunaomba Nyaraka za Shahidi Zipokelewe Bila Wasiwasi wowote.
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa Nne tunaunga Mkono, Kupokea Kwa Set Ya Nyaraka zote Nne, Kwa Maana Nyaraka zote zimekidhi Vigezo Vya Msingi. Na Yeye Mwenyewe ameweza Kutengeneza Misingi ya hizo Nyaraka!
Kibatala: Ameeleza Kwa namna alivyokaa na Vielelezo Vyote kuanzia alipokabidhiwa, Na sisi Washtakiwa wanne tunasubiria Kuja na kuzijaribu Velacity yake Mbele ya Safari wakati wa Cross Examination.
Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa tatu ataanza Wakili Matata Na Baadae nitafuata Mimi.
Wakili Dickson Matata: ASANTE Mheshimiwa Jaji, Upande wa Jamhuri waliweka Mapingamizi Matatu, Moja ikiwa kwa Nyaraka ambazo Shahidi anaomba Kuingiza Mahakamani kwa Maana Barua, Charge sheet, Proceedings na Dispatch hazina Relevant.
La Pili Ni kwamba Hati Ya Mashtaka ni Photocopy na Kwamba haijakidhi Kifungu Cha 66 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, Na Pingamizi la Tatu Kwamba Dispatch, Shahidi Siyo Competent Kuweza Kutender Dispatch.
Mheshimiwa Jaji nitajibu Kwa Ujumla na Wakili Mwenzangu atakuja Kujibu pale Nitakapo Ishia, Mheshimiwa Jaji nianze na Swala la Relevance
Matata: Mheshimiwa Jaji ipo katika Kumbukumbu Za Mahakama hii Kupitia Shahidi Kwamba Jana alieleza Mahakama Kwamba alipata Taarifa za Shahidi D/C Msemwa ambaye alikuwa Shahidi Wa Jamhuri Katika Shauri Dogo.
Shahidi anasema hiyo tarehe Hakuwa Kweli Kwa sababu yeye Mwaka Jana, Tarehe 14 May 2020 baada ya Kukamatwa Mwanga na Kuletwa Dar es Salaam alipokelewa na D/C Msemwa
Sitaki Kuzungumza Sana Kuhusu D/C Msemwa Pale Oysterbay, Itoshe Kusema Kwamba baada ya Kuongea Sababu hiyo na Kwamba Kwa Sababu anajua D/C Msemwa alikuwa Oysterbay aliamua Kuja Kujitolea Kutoa Ushahidi Ili Kuja Ku Disaprove alichokisema D/C Msemwa
Matata: Shahidi akasema ili Kuthibitisha Hayo, aliwasiliana na Wakili wake (Peter Kibatala) Kwamba Ni Wakili aliyehusika Kumtetea Mwaka Jana Katika Kesi namba 77 ya Mwaka 2020 ambayo ni Jamhuri Vs Lembrus MCHOME ambayo ilikuwa Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu
Matata: Aliwasilina na Wakili wake ili aweze Kupata Charge sheet na Proceedings Za Kesi hiyo na Alisema Kwamba Sababu ya Kuomba Nyaraka hizo, Ilikuwa ni Kuthibitisha Kwamba aliwahi Kufika Kituo cha Polisi Oysterbay Na Baada ya Hapo Ndiyo alipelekewa Kwa Hakimu Mkazi Kisutu!
Matata: Na Kwamba alipokuwa Kituo cha Polisi Oysterbay Ndipo alipokutana na D/C Msemwa, Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Ni Wasilisho letu Kwamba Nyaraka hizi ni Relevant na Kwa sababu Malengo ya Nyaraka hizo ni Kutaka Ku' Disprove Kile alichokisema D/C Msemwa
Matata: Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Pingamizi walilileta Upande wa Serikali Kwamba Nyaraka hizi siyo Relevant, Tunaona ni Pingamizi ambalo halina Mashiko. Kwa Sababu Hakuna Namna D/C Msemwa angeweza kuwa Oysterbay na wakati huo huo akawa Polisi Central DSM Wakati ni Vituo tofauti
Matata: Na Mheshimiwa Jaji Bila hata Kuingia Kwenye Barua yenyewe, ilikuwa ni Barua ya Kuomba Nyaraka Kuja kutumika Kwenye Kesi hii.
Matata: Mheshimiwa Jaji nije kwenye suala la Photocopy, ni Pingamizi la JAMHURI Kwamba Hati ya Mashtaka ni Photocopy na Kwamba Imekiuka Kifungu cha 66 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kama Ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2019... Wamesema Kwamba Imekiuka Kifungu Cha 65,66,67 na 68
Mheshimiwa Jaji Nianze Kwa Kusema Kwamba Shahidi Alianza Kwa Ku' lay Foundation Vizuri kwa kuieleza Mahakama ni Kwanini amekuja na Photocopy.. Ni Maelezo ya Shahidi Kwamba Yeye Mwenyewe akiwa na Dada anayeitwa FAITH
Baada ya Kukabidhiwa Barua Kama Nyaraka Walizooomba Mahakama Ya Kisutu, Kwamba alienda Kisutu akiwa na FAITH na Alipofika Alikutana na mama Kwenye Chumba ambacho alikitaja.
Matata: Na Kwamba Baada ya Kufika alimkabidhi Barua aliyopewa na Peter Kibatala ya Kuomba Nyaraka hizo, na Kwamba Yule Mama baada ya Kujiridhisha inafananq na Barua iliyopo Pale Mahakamani, Alimpitia Lembrus MCHOME Court Proceedings na akampa Photocopy ya Charge sheet.
Matata: Shahidi akauliza mbona nimeomba Certified Copy, Mama akajibu Kwamba hii Ndiyo tuliyonayo. Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Fault ya Kupewa Photocopy haijatokana na Mteja wetu ni Fault Ya Mahakama. Sisi tunaona Pingamizi Halina Mashiko.
Matata: Kwa sababu Kifungu cha 67 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kama Ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2019 Inaruhusu Kutumiwa Kwa Photocopy pale ambapo Kuna Mazingira kama Yaliyotokea Kwenye kesi hii.
Matata: Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho la Upande wa Jamhuri Kwamba tulitakiwa Kuomba Notice to Produce Chinese ni ya kifungu cha 68, Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho Letu Kwamba Kifungu Hiki hawajakitazama kwa usahihi, Katika Mazingira ya kesi yetu Ili kifungu cha 68 ya Sheria ya Shahidi Kiweze Kutumika ni pale ambapo Masharti Yaliyowekwa Katika Kifungu (a), Mheshimiwa Jaji naomba kukisoma.
Matata: Mhe Jaji Kwa Kifupi Kifungu cha 68 kinasema Kwamba huwezi Kutumia Evidence ambayo ni Secondary Kama Inaangukia Kwenye Kifungu 67(a), Kwa hiyo ni Wasilisho letu Kwamba Kielelezo Kinacho Ombwa Kuingia Mahakamani Kipo sahihi na hakija Kosa Sifa yoyote ya Sheria Ya Ushahidi
Matata: Mheshimiwa Jaji Kwa namna Nyingine Kwamba, Tufanye Kweli Tulitakiwa Kutoa Notice to Produce Kitu ambacho nakipinga Kwa Nguvu zote, Lakini Bado Mahakama Inayo Uwezo Wa Kupokea Secondary Evidence Kwa Kutumia Kifungu hicho hicho cha 68(g).
Matata: Mheshimiwa Jaji Kwa kuzingatia Kwamba Photocopy hii alipewa na Mahakama na Kwa Kuzingatia tupo Kwenye kesi Ndogo inayohitaji Uharaka, Na Kwa kuzingatia Kipengele (g) Mahakama Inayo Mamlaka ya Kukipokea, Ni Wasilisho letu Pingamizi hilo halina Mashiko na litupiliwe Mbali
Matata: Mheshimiwa Jaji nije kwenye suala la Competence. Na specifically nitazungumzia Kuhusu Dispatch. Mheshimiwa Jaji Ni Submission ya Shahidi Kwamba alipofika Dar es Salaam alienda Kuonana na Wakili wake Peter Kibatala. Na Baada Kuonana na Wakili wake, Wakili wake alimkabidhi Barua na Dispatch akiwa yeye Shahidi Na Mtu anaitwa FAITH, Na Kwamba Baada ya Kukabidhiwa yeye na FAITH waliongozana Kwenda Mahakama Ya Kisutu Wakiwa na hiyo Barua na Dispatch.
Matata: Na ni Ushahidi Wake Kwamba kwanza Alipopewa Dispatch na Barua alijiridhisha Kama Dispatch na Barua Zinahusiana na Kesi namba 77 ya 2020. Na Kwamba waliofika Mahakamani Walienda Kuonana na mama Katika Chumba ambacho alikitaja yeye Shahidi akiwa na Barua na Dispatch
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tumevumilia Sana Lakini Sasa Wakili asitoe Ushahidi, Hakuna Sehemu Shahidi alisema alienda akiwa na Dispatch alisema alienda na Barua..
Matata: Naomba Mahakama itukumbushe, Mimi Nilisikia Kwamba Walienda na Barua pamoja na Dispatch
Jaji anapekua faili lake
Jaji anasoma ila Hakuna Sehemu Kaandika Kuhusu Dispatch kabisa
Jaji: Mimi niliandika kwamba alikabidhiwa barua sioni sehemu ya Dispatch Wakili
Peter Kibatala: Kuna mahala tunalinganisha hapa KWAMBA, panaonyesha majibu ya wakili na shahidi Kibatala ANASOMA
Jaji: Unalinganisha wapi.. Kwenye LIVE?
Kibatala: Sawa, lakini Kama Mahakama Haikuandika hatuwezi Kufanya lolote.. Kwamba Hakusema suala la Dispatch?
Jaji: Mbeleni Mpaka Wanafika Mahakamani hapa Walikuwa na Dispatch Ila sijaona sehemu Kwamba FAITH Alimkabidhi Barua na Dispatch, Ila Baadae alikuwa na Dispatch!
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Hiyo Dispatch ipo au Haipo? Jaji: Dispatch ipo kwa Sababu Mbeleni huku naona Kuna sehemu alisema Kwamba walipo fika hapa walikuwa na Dispatch
Wakili wa Serikali: Lakini haionyeshi Dispatch alipata wapi na Ilikuwa Kwenye Custody yake tangu saa ngapi.
Matata: Mheshimiwa Jaji Shahidi aliweza Kusema Kwamba alikabidhiwa Barua na Dispatch na Aliweza Kutaja Kuwa Ilikuwa na Rangi ya Pinki, Juu Imeandikwa Classic Dispatch Book Ina maneno yameandikwa COURT 2, Ndani yake ina anuani ya Mahakama.
Matata: Kwa Maoni yetu shahidi aliweza Kusema Kwamba alipata wapi na alikaa nayo, Ni Ushahidi Wetu Kwamba Shahidi ni Competent. Kwa sababu Pingamizi lao Lilikuwa linahusiana na Competence na siyo suala la Chain of Custody.
Matata: Tunaiomba Mahakama Inapokuwa inatoa Maamuzi Juu ya Competence, Ijielekeze kwenye Kile Kilicho amriwa Katika Kesi Ya DPP VS MIZIRAHI na wenzake Watatu Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam, Criminal appeal namba 293 ya Mwaka 2016, Ukurasa wa Saba na Nane aya ya kwanza.
Matata: Iliposema posseser anaweza Ku tender Document, Inasema(ANASOMA) Shahidi alionyesha ana hiyo Knowledge na ali' posess Nyaraka hiyo tunaomba Mahakama Imuone ni Competent na Tunaomba Mahakama Itupile mbali Pingamizi hilo.
Mhe Jaji naomba Wakili Mwenzangu amalizie
Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Mimi nitakuwa na Jambo Moja Mheshimiwa Jaji Wakili Wa Serikali Wakati anazungumzia suala la Dispatch, alisema Kutajwa kwa Reference namba kwenye Dispatch, Kwa Maoni yangu Mhe Jaji alikuwa anazungumzia Authentication ya Dispatch hiyo
Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Wakati Shahidi anatoa Ushahidi Wake, Alizumgumzia Kidogo Kuhusu Dispatch hiyo kwa Kutaja unique Features Mbalimbali kama Rangi, Jina Lililopo Juu Kwa Maana Classic Dispatch Book na COURT 2
Kihwelo: Na Shahidi alikwenda Mbali Kwamba Ndani palikuwa na Tarehe, Anuani ya Barua na Sahihi ya Mpokeaji, Kwa Maoni yangu Kwamba aliweza Ku authenticate, Mheshimiwa Jaji Pia naomba nizungumzie Kuhusu suala la Hati ya Mashtaka.
Kwamba Shahidi Ameleta Nakala, Na Shahidi alieleza kwamba Kwanini alileta Nakala, Kwa kuwa Shahidi amesema Kwanini Shahidi Ameleta Nakala, Ni Submission Yetu Kwamba Ushahidi Wa Shahidi Unapaswa Kuchukuliwa akwa Uzito unaostahili.
Kihwelo: Na hilo pia lipo Katika Sheria Kesi Ya GOODLUCK KYANDO Vs REPUBLIC Criminal appeal 118, ya 2003 ipo kwenye Tanzania Law Report Kwenye Ukurasa wa 363 na Specifically 367.
Mheshimiwa Jaji Kwa hili na yake ambayo yemezungumzwa na Wakili Mwenzangu Dickson Matata Naomba, Itupilie Mbali Mapingamizi na Ikubali Vielelezo Vilivyoletwa Mbele Yako Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
Jaji: Jamhuri?
Wakili wa Serikali: Mhe Jaji Kwa Ufupi sana Naanza na Hoja ya Wakili Msomi Dickson Matata Alianza Kujibu Hoja ya Relevance, Wakati anazungumzia Hoja ya Relevance, Ni kweli Shahidi alieleza hayo, lakini Hoja yetu ya Msingi ni Hayo aliyosema alipaswa aoanishe kwenye Hizo Nyaraka
Wakili Peter Kibatala: OBJECTION Wakili anaruhusiwa Kwenda Ndani tena ya Proceedings????
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Eneo Lingine Mwenzetu aligusia Swala la Secondary Evidence. Mwenzetu alielekeza Mahakama Kifungu cha 67 1(c) na aakaisomea Mahakama Kwa Ufasaha, Katika Hiki Kifungu, Wenzetu hawawezi Kupata Hifadhi hapa.
Walitakiwa Kuieleza Mahakama Kati haya Matatu, Nyaraka Halisi either Imepokea, ama Nyaraka halisi imeharibika, ama kwa Sababu ambazo hazitokani na wao Wameshindwa Kuleta Nyaraka hiyo Ndani ya wakati. Sasa Kusema Pekee Kwamba aliyetuhudumia akituambia Kwamba hii Ndiyo Nyaraka pekee, haitoshi kwa Kusema.. Badala yake Walipaswa Waonyeshe Jitihada Walifanya Nini Baada ya Kuambiwa Hivyo.
Wakili wa Serikali: Badala yake wanaitupia Mahakama Lawama Badala ya Kusema Walifanya nini, Kwa Maoni yetu siyo Sahihi. Vilevile Mheshimiwa Jaji Mwenzetu anaomba Mahakama Ipokee Nyaraka hiyo kwa kutumia Kifungu Cha 68(g).
Huu siyo Wakati wake Kitendo Cha Kuto Jibu Maana yake Wenzetu wamekubali na hawana Kipingamizi nalo, Vilevile Wenzetu Wamezungumzia Kuhusiana Na Suala la Competence Ya Dispatch, Wamezungumzia Competence Ya Shahidi Yenye Connection Na Dispatch Mheshimiwa Jaji hapa tunaona Wenzetu walichanganya Mambo mawili Kwa Wakati Mmoja, Wenzetu Wanasema Kwamba Kwa Sababu Shahidi ameweza Ku Identity Unique Features basi ana Knowledge
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Utambuzi wa Nyaraka na Kilichopo ndani ya Nyaraka Ni Vitu Viwili tofauti, Kutambua Nyaraka Pekee yake Haitoshi, Kwa Maoni yetu Kutambua Nyaraka Na Kujua Kilichopo ndani ya Nyaraka Ni Tofauti. Wenzetu Walitakiwa Wajibu Hoja yetu Katika Misingi huu, Kitu ambacho hawajafanya, Mwisho Wenzetu Wameielekeza Mahakama Katika Kesi Ya GOODLUCK KYANDO, Kitu ambacho sisi tunasema Principle hii haiwezi Kutumika hapa, Kwenye kesi hii Wanaongelea Kielelezo ambacho Kipo Kwenye Kumbukumbu za Mahakama, Sisi tunasema Hoja za Wenzetu hazijajibu Hoja zetu, Sisi tunaomba Mahakama Isizingatie Hoja zao Kwa Sababu Hazina Nguvu Kisheria.
Jaji: Nimewasikia pande zote mbili kwa hoja zote mbili nahitaji ku' digest Nahitaji muda wa dakika 45 kama naweza kuwaita mapema nitawaiteni
Tutarudi saa nane na dakika 25
Jaji anatoka
====
9:00 Mchana jaji bado hajarudi
Jaji: Muda Mfupi Uliopita kabla Mahakama Kupumzika, Niilisikiliza Hoja za Pande zote mbili, Sasa Uamuzi ni Kama Ufutavyo
Shahidi Wakati anatoa Ushahidi Wake ambapo ni Barua Kutoka Kwa Wakili Wake Peter Kibatala Kwenda Mahakama Ya Hakimu Mkazi, Dispatch na Mwenendo Wa Kesi pamoja na Hati ya Mashitaka Kutaka Kuingia Kama Kielelezo.
Jambo ambalo lilipingwa na Mawakili wa Serikali Kwamba Moja Nyaraka hizo hazina Uhusiano na Kesi (Relevance), Na Pia Kwamba Hati Ya Mashitaka Ilikuwa ni Nakala na siyo Nakala Halisi. Tatu ilikuwa Kwamba Shahidi ajaonyesha Kwamba anaifahamu Dispatch, Mahakama Kwa kuzingatia Hoja zote za pande Mbili, Na Mahakama Ikazingatia Kwamba Nyaraka hizi Zinazoombwa Kuingia zitaishia Kwenye kesi hii Ndogo.
Jaji: Pia Kwamba Shahidi ana tatizo la kina Ki Afya, Na Kwamba Ni Kweli Kwamba Nyaraka zinatumika Kuuliza Maswali lakini Mahakama Inayo Muda wa Kuzichunguza, Kwa Sababu hiyo Mahakama Imeona izipokee Nyaraka kuzingatia Uamuzi Wake utaokuja Kutoa Mbele
Jaji: Mahakama Inapokea Barua Kwenda Kwa Hakimu Mkazi Kisutu kama Kielelezo Namba 1.. Mahakama Inapokea Dispatch Kama Kielelezo Namba 2.. Mahakama Inapokea Nakala ya Hati Ya Mashtaka ambayo ilikuwa imefunguliwa Mahakama ya Kisutu Jamhuri Vs Lembrus MCHOME, Mahakama Inapokea Pia Mwenendo Wa Kesi hiyo namba 77 ya Mwaka 2020, Kama nilivyosema Kwamba Mahakama Itatoa Uamuzi Juu ya Nyaraka hizi wakati Maamuzi wa Kesi Ndogo.
Wakili wa Serikali: Naomba Kwa Record Juu ya Namba, Kuna Kielelezo Cha Goodluck.
Jaji: Basi naomba Kubadilisha Namba,
Barua itakuwa D2
Dispatch Itakuwa D3
Hati ya Mashitaka ni D4
Na Mwenendo ni D5
Jaji: Naomba Sasa Shahidi akabidhiwe aweze Kusoma
Jaji: Shahidi nakukumbusha kwamba uliapa, na utaendelea kuwa chini ya kiapo Wakili Fredrick: Isome barua
Shahidi: ANASOMA BARUA Kutoka TANAFRICA LAW kwenda kwa Hakimu Mkazi Kisutu Shahidi anasoma kwa kiingereza kile cha ndani ndani kabisa (yaani kutoka Buckingham Palace)
====
Mahakama imetupilia mbali mapingamizi yote ya Jamhuri dhidi ya vielelezo vya shahidi wa pili wa utetezi, lakini Jaji amesema vielelezo hivyo vitazingatiwa zaidi katika maamuzi ya mwisho wa shauri katika kesi ndogo hii. Hivyo shahidi ameingiza vielelezo.
Jaji: Soma na dispatch book
Shahidi: anasoma dispatch Book.
Wakili Fredrick: Nakukabidhi hati ya mashtaka shahidi Shahidi: shahidi anasoma Hati ya Mashtaka pia Kwa Kiingereza kizuri
Wakili Fredrick: Nitakukabidhi Mwenendo Wa Kesi na Usome Page ya Kwanza na Ya Mwisho
Wakili Fredrick: Kihwelo Shahidi Ulisema Kwamba Oysterbay Ulikaa Siku 14 Je Ulimaanisha nini
Shahidi: Nikipofikishwa Oysterbay Mara ya Kwanza Nilikaa Siku Tano Kuanzia Tarehe 14 May Mpaka Tarehe 15 May 2020, Nilipopelekwa Kisutu
Wakili Fredrick: Baada ya Hapo, Nilisomewa Kesi Na Kunyimwa Dhamana Nakutakia kwenda Magereza nikarudishwa Oysterbay Siku 14,
Fredrick: Ilikuwaje Ukarudishwa Oysterbay
Shahidi: Baada ya Kukosa Dhamana, Hakimu alisema Nipelekwe Keko, Wakati Ule Palikuwa na Corona Sikupelekwa Magereza Badala Yake nikapekwa Oysterbay tena
Wakili Fredrick: Kwanini Sasa Hawakukupeleka Magereza Kama Hakimu alivyosema Shahidi: Kwa Uelewa Wangu Sababu ya Corona
Wakili Fredrick: Ulipimwa lini Corona
Shahidi: Siku ya Tarehe 19 May 2020
Wakili Fredrick: lini tena Ulipima Corona
Shahidi: Hakuna zaidi Ya Kusubiri Majibu ya Corona
Wakili Fredrick: lini Ulirudishwa tena Mahakamani
Shahidi: Siku ya Tarehe 19 ambapo Hakimu alikataa Kunipokea Kwa Sababu Nilikuwa Nimtokea Polisi na siyo Magereza kama alivyoagiza
Wakili Fredrick: Siku ya Tarehe 03 nini Kilitokea
Shahidi: Siku niliyopelekwa Magereza
Wakili Fredrick: Na Siku ya Tarehe 05 June nini Kilitokea
Shahidi: Nilisomewa Mashtaka Kwa Njia Ya Mtandao na Hakimu akasema Kwamba Naweza Kupata Dhamana
Wakili Fredrick: Na Tarehe 08 June, Nini Kilitokea
Shahidi: Siku ambayo nilipata Dhamana Maana Siku ya Tarehe 05 June sikukamilisha Masharti ya Dhamana
Wakili Fredrick: Umetaja Tarehe Nyingi Nyingi Je zote zipo Kwenye Mwenendo Wa Kesi
Shahidi: Ndiyo zote zipo
Fredrick: Tarehe 03 Mwezi Wa Sita Utaipata Ukurasa wa Ngapi
Shahidi: Ukurasa wa Tano
Wakili Fredrick: Tarehe 08 June 2020 Utaipata Ukurasa Upi
Shahidi: Kwenye Ukurasa Wa Sita
Wakili Fredrick: Nini Kilitokea Mwezi wa 10 August 2020
Shahidi: Hakimu aliniachia Kwa kifungu 225 baada Ya Upelelezi Kutokamilika
Wakili Fredrick: Nini Kilitokea tena
Shahidi: Nilikamatwa na kurudishwa tena Oysterbay
Wakili Fredrick: Uliwakuta Askari Gani
Shahidi: Mkuu wa zamu alikuwa Afande Msemwa, khadija na Sam
Wakili Fredrick: Umekuwa Ulimtaja Afande Msemwa wa Oysterbay
Shahidi: Mwonekano wake ni Mweusi Kidogo kwangu, Ana mwili kunizidi Kidogo
Shahidi: Kitu Kingine ni Namba Yake
Wakili Fredrick: Namba gani
Shahidi: Namba Yake Ya ajira
Wakili Fredrick: ambayo ni namba Ngapi
Shahidi: H4323
Fredrick: Wakati Unajitambulisha Umesema Wewe Ni Mkulima, Ukiachana na Kilimo unafanya Shughuli Gani Nyingine
Shahidi: Najihusisha na siasa
Wakili Fredrick: Kule Mwanga Ulihojiwa Kwa Kosa gani
Shahidi: Makosa ya Kupiga Picha Gari ya Kiongozi Fulani wa Taasisi Fulani Tanzania
Wakili Fredrick: Ukashtakiwa kwa Makosa gani
Shahidi: Kwa Makosa ya Kimtandao, Kitu ambacho Kilinishangaza
Wakili Fredrick: Unasema Ulitambua Afande Msemwa Kwa Namba Yake, Je Ilikuwa sehemu gani
Shahidi: Upande wa Kulia Kifuani
Wakili Fredrick: Wakati Unahojiwa hapa ulisema Kwamba Mwanga hukuandika Jina Popote na Ulipokuwa Moshi pia Huku andikwa Popote
Shahidi: Watu wengi wana fikishwa Vituo Vya Polisi bila Kuandikwa Mahali Popote
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hayo ni Maoni yake
Wakili Fredrick Kihwelo: Naondoa Mheshimiwa Jaji, Na huo utakuwa Mwisho Wangu
Wakili Nashon: Nkungu Shahidi Ulisema Kwamba Askari walikuja Nyumbani Kwako Kukukamata, Je Walikuja nyesha Arrest Warrant.?
Shahidi: Hapana
Nashon Nkungu: Nilisikia Pia Unasema Waliruka Geti
Shahidi: Ndiyo
Nashon Nkungu: Je Walikuja na Kiongozi yoyote Wa Mtaani Kwako
Shahidi: Hapana
Nashon Nkungu: Nilisikia Unasema Ulishtakiwa Kwa Matumizi Mabaya Ya Mtandao
Shahidi: Ndiyo
Nashon Nkungu: Nilisikia Ulikamatwa Kwa a Kupiga Picha Kiongozi Fulani Mkuu wa Taasisi Fulani hapa Nchini
Shahidi: Ndiyo
Nashon Nkungu: Nilisikia Unasema Kuhusu Askari Msemwa hapa Mahakamani, Je Mna ugomvi
Shahidi: Hatujawahi Kuwa na Ugomvi
Nashon Nkungu: Nilisikia Pia Kwamba Uliletewa Dar es Salaam Tarehe 14 May 2020
Shahidi: Ni sahihi
Nashon Nkungu: Ulimuona Afande Msemwa Siku hiyo
Shahidi: Ndiyo
Nashon Nkungu: Alikuwa Wapi
Shahidi: Mapokezi Oysterbay
Nashon Nkungu: Ulikuwa Unapata Huduma Za Kibinadamu
Shahidi: Ndiyo
Nashon Nkungu: Kama Nini
Shahidi: Kama Chakula na Maji
Nashon Nkungu: Nani alikuwa anakuhudumia Chakula
Shahidi: Mimi nilikuwa Simfahamu Kwa sababu Nilinyimwa Kuonana Na Ndugu zangu
Nashon Nkungu: Askari gani alikuwa anakuhudumia Kule Mahabusu
Shahidi: Askari wengi akiwemo Msemwa
Nashon: Ahsante Mheshimiwa Jaji
Mallya: Sasa Umesema Wewe Mwanasiasa Je Wa Chama Gani
Shahidi: Wa Chadema
Mallya: Je Nikisema Wewe Mwanachama Umekuja Kusema Uongo Mahakamani Kumuokoa Mwenyekiti Wako Mahakamani, Nitakuwa nasema Uongo.?
Shahidi: Uongo Mkubwa
Mallya: kwanini
Shahidi: Kwa sababu hata Ingekuwa Mtu wa CCM anatoa Ushahidi Wa Uongo ningekuja Kuisaidia Mahakama..
Mallya: Je Namba ya Msemwa Iko Kwenye Nini
Shahidi: Beji Kama Chuma Kifuani
Wakili Peter Kibatala: Shahidi Oysterbay ipo sehemu gani au kuna kitu gani Kimepakana Nacho?
Shahidi: Ubalozi Wa Marekani
Kibatala: Asante Mheshimiwa Jaji sina Swali lingine
Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu tutajie Majina yako
Shahidi: Lembrus Kapuya Mchome
Wakili wa Serikali: Ulisikia Mtu anaitwa Mchome Je ni Ndugu yako
Shahidi: Hapana, Utakuwa ni Ukoo labda
Wakili wa Serikali: Kinachotofautisha MCHOME wewe na Wengine ni nini
Shahidi: Maboma ya Kifamilia
Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini
Shahidi: Ukoo Mkubwa au Kuna wachome Wengine Wala Hatufahamiani
Wakili wa Serikali: Sasa Umetuambia Kwamba Ulikuwa Unafuatilia Mwenendo wa kesi Hii kwa Mtandao na Magazeti
Shahidi: Sahihi
Wakili wa Serikali: Ulimaanisha Mtandao ni Mitandao ya Kijamii
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Katika Social media unatumia mtandao upi!?
Shahidi: T W I T T E R
Wakili wa Serikali: Unatumia majina gani
Shahidi: Lembrus Mchome
Wakili wa Serikali: Umesema pia wewe ni mwanasiasa
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Katika Sasa unanafasi gani
Shahidi: Ni Katibu Wa Chadema Wilaya ya Mwanga na Pia Katibu Wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro
Wakili wa Serikali: na utakuwa Mwanachama Hai wa Chadema Kwa Muda gani
Shahidi: Kwa Muda wa Miaka 11 Sasa hivi
Wakili wa Serikali: Katika Muda wote wa Kuwa Mwanachama Mwenyekiti Wako ni nani
Shahidi: Ni Freeman Aikael Mbowe
Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sawa Nikisema Kwamba Kwenye Nyanja za Kisiasa Mnafahamiana Sana
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Unapendezwa na Uongozi wake
Shahidi: Sana
Wakili wa Serikali: Kwenye Kesi hii, Ya Uhujumu Uchumi namba 16 ya 2021, Unafahamu alishitakiwa lini
Shahidi: Hapana Sikumbuki
Wakili wa Serikali: Ya Mwaka huu au Mwaka Jana
Shahidi: Mwaka huu
Wakili wa Serikali: Wakati unashtakiwa Hati yako inasema Kwamba Unashtakiwa Kwa Publication of Ponograph
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Unasema Kwamba Kesi hiyo ili maliza Tarehe 10 Mwezi 08 2021
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Wakati Huo Freeman Mbowe ameshashrakiwa tayari
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Baada Ya Kuwa Umeshaaachiwa Je Ulifunguliwa Kesi Nyingine tena
Shahidi: Hapana
Wakili wa Serikali: utakubaliana na Mimi Kwamba Kwa Kipindi hicho kabla ya Kufahamu.. Kwanza Nikuulize Swali, Je Ni kweli Ulifahamu Msemwa alitoa Ushahidi Kupitia Mitandao
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Ni kweli Kwamba, Kabla ya Kuona Taarifa hizo na Ulichukulia Kwamba Shitaka lako limefutwa, Kabla ya Hapo Ulikuwa hujawahi Kuomba Kupatiwa Mwenendo na Hati ya Mashtaka!?
Shahidi: Hapana
Wakili wa Serikali: Katika Mitandao ya Kijamii Haswa Twitter Ambapo Unajulikana Kama Lembrus MCHOME, Namna ya Kutuma Ujumbe Unautengeneza Mwenyewe yaani (User generator)
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Ukitaka Kuchukua Ujumbe wa Mtu Mwingine yani Retweet Unafahamu
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Kwenye Mtandao Wa Twitter, Kama Naelewa Utanifahamisha, Ni Information Ambazo Mtu anaweza Kuona zile ambazo umetweet na Kuziona
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Sasa na Mara Nyingine Umekuwa ukiandika Ujumbe Unaohusiana na Kesi hii Kule Twitter
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Katika Moja wapo ya Vitu Ulivyo tweet Ukasema "kesi Mikazo, Mashahidi wa Michongo" ulikuwa unamaanisha nini
Shahidi: Maana yake ni Mashahidi Wa Kuungaunga!
Wakili wa Serikali: Vipi Kuhusu Mawakili wa Serikali wa Michongo na Majaji wa Michingo
Shahidi: Kwa sababu Mawakili wa Serikali Wanateta Mashahidi Wa Uongo
Wakili wa Serikali: Na Vipi Kuhusu Majaji wa Michongo?
Shahidi: Ndiyo Kuna Hukumu ambazo Wanatoa hazipo Sawasawa
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Una malalamiko Kuhusu Kesi hii
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo wewe ni Shahidi Mwenye Malalamiko
Shahidi: Ninayo Malalamiko Kwa Sababu Mahakama inadanganywa
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Unatamani Siku Moja Mawakili Wa Serikali unaowataka Wewe?
Shahidi: Nataka Haki itendeke tu
Wakili wa Serikali: Jibu swali Langu
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Unatamani Siku Moja Mawakili Wa Serikali unaowataka Wewe
Shahidi: Ambao Watakuwa Wapo Sahihi, Ndiyo kabisa.
Wakili wa Serikali: Ni kweli Watu walikuwa wanakupa Pole Kwenye Mitandao yako Baada ya Kupata Ajali
Shahidi: Ndiyo
WS: Walikuwa wa nakupa Moyo Kamanda Nenda Kapambane
Shahidi: Hiyo sijaona
WS: Kitu Kilichokufanya Uje Kutoa Ushahidi, Unamfahamu linamuhusu Mshtakiwa yupi?
Shahidi: Ndiyo
WS: Nani?
Shahidi: Katika Shitaka hili Dogo ni Mohammed Ling'wenya
WS: Wakati Unaongozwa na Wakili Dickson Matata Na Fredrick Kihwelo Ni kweli Hukutoa Ushahidi huyu Mohammed Ling'wenya Mnafahamiana Lini na Wapi, Ni kweli Kwamba Wakili Peter Kibatala ambaye Ulimpa Maelekezo Kwamba aandike Barua Kwenda Kisutu, Yeye Siye anayemwakilisha
Mohammed Ling'wenya?
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Wakili wa Serikali: Kama unafahamu Sema sasa ni Lini sasa Ulifahamu Kwamba Peter Kibatala hamuwakikishi Mohammed Ling'wenya
Shahidi: Kwenye VYOMBO Vya Habari
Wakili wa Serikali: Na Unafahamu Kwamba Peter Kibatala ana mwakilisha Freeman Mbowe?
Shahidi: Nafahamu Ndiyo
Wakili wa Serikali: Mwanzoni Nilikuuliza Kuhusiana na Jina Mchome, Turudi Sasa Kwa Jina la Msemwa, Je litakuwa na Watu wengi wanaoitwa hivyo?
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Katika Ushahidi Wako Tangu Unaongozwa Jana Hukutoa Ushahidi Kwamba Kwa Jina hilo la Msemwa Wapo Watu Wengi Kwa jina la Msemwa
Shahidi: ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Hukusema hawa watu wa Jina la Msemwa Wapo Wangapi Kwa Jeshi la Polisi
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Kwa Sababu Ulikuwa Ukifuatilia Kesi hii, Unafahamu Kwamba hii ni Kesi Ndogo Ya Pili
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Unafahamu pia Kwamba Katika Kesi Ndogo Ya Adam Kasekwa Msemwa alitoa Ushahidi
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Ulifahamu Lini Siku hiyo hiyo au
Shahidi: Sikumbuki
Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Katika Ile Barua iliyopokelewa Mahakamani ilivyoandikwa na Kibatala Kwenda Kisutu, Ni kweli Kwamba haina Jina la Mohammed Ling'wenya Popote pale
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Kutokana na Jinsi ilivyoandikwa ndiyo inaakisi Kile Ulicho Muelekeza Peter Kibatala
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Hata Ile reference namba Uliyosoma pale Juu ina Neno Mbowe
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Sasa Kwa Mazingira hayo hata Katika Ushahidi huu, Ni Makubaliano Yako Kuja Baina yako na Peter Kibatala
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba Wenzangu Waendelee
WS: Mheshimiwa Jaji naomba ni Muonyeshe Shahidi Exhibit D2.. Umeona eeh? Nyaraka inaelekeza akwa nani
Shahidi: inaelekezwa Kwa Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu
Wakili wa Serikali: Ni sahihi Ilimfikia huyo Hakimu Mkazi Kisutu
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Nyaraka hiyo Wamepewa nani na nani
Shahidi: Lembrus Mchome Na Naibu Msajili Wa Mahakama hii
Wakili wa Serikali: anapaitika Wapi
Shahidi: Mahakama hii
Shahidi: Hapana
Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Kwamba Umekuja baada ya Kusikia, DC Msemwa Kusema Kwamba alimpokea Mohammed Ling'wenya Pale Kituo cha Polisi Central, Reference namba zinamuhusu Nani+
Shahidi Mbowe
Wakili wa Serikali: Wakili Wako ni nani
Shahidi: Peter Kibatala
Wakili wa Serikali: Anamwakilisha Nani katika hili Shauri
Shahidi: Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi nikisema Freeman Mbowe anaitambua Barua hii
Shahidi: Hilo silijui
Wakili wa Serikali: Ni kweli Kwamba Mohammed Ling'wenya atakuwa anajua Barua hiyo
Shahidi: Ndiyo
Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji Napinga Swali na Jibu sababu Lina Suggest Opinion
Jaji: Ngoja tumsikie
Wakili wa Serikali: Swali langu Kwamba Hiyo Barua haionyeshi Kumfikia Bwana Mohammed Ling'wenya
Jaji: ni Wakati gani hapo Opinion,
Wakili Dickson Matata: Kauliza Ni kweli Kwamba Mohammed Ling'wenya hajui kuhusu Barua hiyo
Jaji: Basi Wakili wa Serikali Rudia Swali
WS: Shahidi Ni kweli Kwamba Kwa Maudhui ya Barua hiyo haionyeshi Kumfikia Mohammed Ling'wenya
Shahidi: Hilo sijui
WS: kuanzia Siku ya Jana Mpaka Leo Hii hakuna Sehemu yoyote Uliyo eleza Kwamba Uliwasiliana na Mohammed Ling'wenya
Shahidi: Ni sahihi
WS: Ni sahihi Mahakama Haijaonyesha Kwamba Mohammed ana ufahamu wako wewe Kuwepo Mahakamani
Shahidi: Ndiyo
WS: Kwa hiyo nitakuwa nakosea Nikisema Wewe Umeletwa Kwa Madhumuni fulani fulani
Shahidi: sawa
Jaji: Shahidi Umesema
Shahidi: Sawa
Matata: Mhe Jaji Shahidi Ameshajibu
Wakili wa Serikali: Hakuna Kurudia Swali
Jaji: Mie Mwanzo nimesikia SANA
Wakili Dickson Matata: Na mimi nimesikia SAWA
Jaji: Wakili wa Serikali, Kwa Maslahi Ya Haki hebu rudia Swali
Wakili wa Serikali: Hebu Soma hii Nyaraka Paragraph Ya Pili
Wakili wa Serikali: Hebu ijibu Mahakama Mr. Freeman Aikael Mbowe ndiyo Mohammed Ling'wenya
Shahidi: Hapana
Wakili wa Serikali: Hebu iambie Mahakama Ni sehemu Gani imeandikwa Kwamba hizo Taarifa unazoomba Umelenga Kuthibitisha Kwamba Mr. MSEMWA Hakuwepo Central
Shahidi: Hakuna
Wakili wa Serikali: Katika hiyo Barua ni sehemu Gani Inaeleza Kwamba Ulikuwa Kituo Cha Polisi Oysterbay
Shahidi Hakuna
Wakili wa Serikali: Ni wapi Katika Barua hiyo Sehemu Inavyoonekana Kwamba Wakili anaye Mwakilisha Mohammed Ling'wenya Kwenye hiyo Barua
Shahidi: Hakuna
WS: Mwanzoni ulilenga Kuonyesha hizo Barua Ili Kuthibitisha Kwamba Mr Msemwa alikuwa Oysterbay
Shahidi: Ndiyo
WS: Ulisema Tarehe 14 Maya 2020, Wakati Umefikishwa Oysterbay Polisi, Miongoni Mwa Askari Aliyekuhudumia alikuwa na DC Msemwa
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Na Ulisikika Ukisema Kwamba ulimtambua DC. Msemwa kupitia Beji yake aliyo vaa
Shahidi: Hapana
Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sahihi Nikisema Kwamba Huyo DC Msemwa Uliyemtambua wewe alikuwa amevaa Uniform
Shahidi: ndiyo
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo nitakuwa Sahihi Nikisema Ulimtambua DC Msemwa Baada ya Kuona Beji yake yenye namba yake 4323
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Toka Umeanza Kutoa Ushahidi Wako Siku ya Jana Mpaka Leo Hii Hakuna Mahala Umesema Kwamba alikwambia ni wakati Gani anaitwa DC Msemwa na Hukusema ni Wakati gani ulipata Kujua
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Kwa Kushindwa Kusema Ulijuaje anaitwa DC Msemwa, Mahakama ipo gizani
Shahidi: Si Kweli
WS: Kwa Ruhusa Yako tunaomba tuendelee Kesho Kwa sababu Muda hautoshi
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tulishaliomgea hilo Kwenye Briefing Kwamba Tumlimde Shahidi Haki yake ni Mtu aliye Pata Ajali.
Kibatala: Na Kwamba tulimuomba Mpaka Kwa Wazazi wake, Shahidi Ni Mgonjwa na Haki yake inaonekana..
WS: Mheshimiwa Jaji Magereza Waliomba Asubuhi Kwamba tujitahidi tumalize Saa 11 ili Wapate Muda wa Kuwahi Kurudi Magereza
Jaji: ni Kweli Kwamba tulikaa pamoja Asubuhi Kwamba Kuna Jambo hilo la Hali ya Shahidi, Ni suala linahusu Haki.. Lakini pia ni Haki Upande wa Mashtaka Kusikilizwa, Na Hali ya Shahidi Tunaona pia, Je Shahidi Unaweza Kesho kuwepo?
Jaji: Nikuombe Shahidi, Je huwezi Kuja Kesho?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Hali yangu inaniwia Ngumu, Ila Kwa Sababu ni Ombi lako inanibidi nikubali..
Jaji: jitahidi tu, jitahisi.. ni Ombi kutoka kwa Jaji, Na hilo nimekuomba wewe Binafsi Siyo Kupitia Kwa Wakili.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Hairisho Mpaka Kesho Tarehe 01 Mwezi wa 12 ilituweze Kuendelea na Cross Examination..
Jaji: Upande Wa Utetezi Mnae Shahidi Mwingine?
Wakili Peter Kibatala: Tunaye Mmoja
Jaji: Shahidi Baada ya Kuwa Nimekuomba na Umenikubalia naomba Kesho Uje
Jaji: Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi. Saa 3 Asubuhi, nawatakia Jioni Njema.