Yaliyojiri Bungeni: Mbowe, Naibu Spika wazozana tena kuhusu swali kwa Waziri Mkuu

Siku zote mtu anayeogopa changamoto hafai kuwa kiongozi, baba Jeska anapaswa kutambua kuwa upinzani ndio ulimsaidia kuwa hapo alipo. Maana uchaguzi uliopita ulikua na msukumo mkubwa wa mabadiliko ndipo viongozi wa CCM wakaona ni vyema waweke mgombea ambaye at least ataweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi, lkn km upinzani ungekuwa legelege basi CCM walikua na kila sababu ya kumpitisha membe au Lowasa.
 
Tatizo mtasema mahakama zinaingiliwa na serikali amejibu hawezi kuingilia kazi mahakama bado mnalalamika tuwaelewe wapi mnasimamia
.....kesi hizo hizo wangeshinda wangesema wao ni wajuvi wa sheria na serikali haina wanasheria na wangesema kuna haki. Natamani aje aingie 18 adakwe ahukumiwe na afungwe huyu
 
Kweli,mbowe anashindwa kupeleka impact sahihi anapouliza maswali,suala la vyama ni la kikatiba,nadhani angelijenga swali kwa vigezo vya kikatiba na atumie lugha kali.

Swali limeeleka vizuri sana achani spinning...
 
Huyu naibu spika lazima atetee kiti chake kwa kuwa ubunge wake ni kwa hisani ya mtu wa ikulu, hataki hata kukubali kuwa mteule wake anavunja katiba?! saibu tupu kwa kiongozi huyu mpalilia kibarua.
 
Kama ni hivi ni bora kutokuwa na Naibu Spika mwanamke.Ni aibu kubwa.Lakini miaka mitano ni michache sana.
 
Wanabodi,
Leo katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo na Waziri Mkuu, Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe, alimtuhumu Rais Magufuli kutoa kauli za viashiria vya kutokomeza Upinzani kabla ya 2020 ikiwemo kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.

Waziri Mkuu alijibu hakuna kitu kama hicho.

Mhe. Mbowe akaongeza kama ataleta ushahidi Bungeni wa kauli za rais Magufuli kufifisha Upinzani, Jee Waziri Mkuu atakuwa tayari kujiuzulu?.

Naibu Spika akaingilia kati kumzuia Waziri Mkuu asilijibu.

Hivyo natoa wito kwa Mhe.Mbowe, japo Naibu Spika amemuokoa Waziri Mkuu, lakini kama Mbowe ni mkweli na ushahidi anao, hana haja ya kumuuliza Waziri Mkuu kama atakuwa tayari kuwajibika bali a proceed kuuleta ushahidi huo Bungeni na kuutumia kumwajibisha Waziri Mkuu kupitia kura ya Kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Ila pia Mhe.Mbowe asaidiwe kidogo kwenye phrasing ya maswali yake ili ku hit hard na kuacha no room ya kukwepa kujibu.

Paskali.
Mbowe alitudanganya kuwa Lowasa ni fisadi na dhaifu, sasa hivi tena ana kesi ya kukwepa kodi ,anatakiwa awajibishwe na kufukuzwa ukiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni
 
.....kesi hizo hizo wangeshinda wangesema wao ni wajuvi wa sheria na serikali haina wanasheria na wangesema kuna haki. Natamani aje aingie 18 adakwe ahukumiwe na afungwe huyu

Ameshahukumiwa tayari,ahukumiwe mara ngapi??Naona unafurahia watanzania wenzako wakinyanyaswa sababu ya kiitikadi,kuna siku utawatafuta waje wkausaidie ndipo utajua nini maana ya maumivu.

Kwa sasa hivi chekelea lakini hata huyo Waziri Mkuu anajua kuna shida kubwa huko juu
 
Dkt Magufuli ni mpaka 10 years, yaani nyie na roho zenu za wivu mzoee! Serikali yote ipo chini yake na wananchi tuna mkubali kwa 100%

Wewe ndio utakufa kwa kuona hakuna atakayema kura hata mkewe nina imani hiyo hawampi.
 
Mimi sina imani kabisa na huyo naibu spika, anatekeleza matakwa ya Serikali na ndiyo maana mihimili mingine inadharauliwa kwa kuonekana haijachimbiwa kwenda chini sana kama Muhimili wa Serikali
 
Alichokisema Mbowe kiko sahihi kabisa. Kila chama kina lengo hilo hilo, yaani kuhakikisha chama kingine kinadhoofika na hata kufa ili wao washike madaraka. Kwa sababu tunapendaga uongo uongo, tutaanza kukimbilia kukanusha bila sababu za msingi. Hata Chadema nao wanafanya hivyo hivyo, kuhakikisha CCM inakosa nguvu na kusambaratika. Lakini swali lake liko deep zaidi, na kwa maoni yangu linaigusa zaidi katiba yetu. Ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi ktk nchi yetu unakuwa na matatizo mengi kwa sababu ya Ma- Rais wa nchi (Ambao by virtue of their positions) wanapaswa kuwa neutral na kuvitendea haki vyama vyote, wanakuwa "wenyeviti wa vyama vyao" zaidi. Wenye kuelewa wameelewa. Hilo ndilo tatizo letu kubwa. Hatujaweza kufikiria mbali zaidi kuhusu hizi kofia mbili. Rais akishachaguliwa kushika wadhifa huo, anapaswa kuwa Rais wa wote, na si kiongozi wa chama kimoja cha siasa.
 
kwanini huwa kiti kinazuia bwana pm asiwe anajibu maswali...? anaogopa kuaibika...? hajajiandaa? hajui kinachoendelea katika jami...? kitu gani zaidi?

Anajua ila akisema ndiyo ujue sahani la ugali limeondolewa.SO either akubali au asijibu.Halafu ona alivyokuwa anajibu hata yeye mwenyewe hajiamini na majibu yake
 
Alichokisema Mbowe kiko sahihi kabisa. Kila chama kina lengo hilo hilo, yaani kuhakikisha chama kingine kinadhoofika na hata kufa ili wao washike madaraka. Kwa sababu tunapendaga uongo uongo, tutaanza kukimbilia kukanusha bila sababu za msingi. Hata Chadema nao wanafanya hivyo hivyo, kuhakikisha CCM inakosa nguvu na kusambaratika. Lakini swali lake liko deep zaidi, na kwa maoni yangu linaigusa zaidi katiba yetu. Ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi ktk nchi yetu unakuwa na matatizo mengi kwa sababu ya Ma- Rais wa nchi (Ambao by virtue of their positions) wanapaswa kuwa neutral na kuvitendea haki vyama vyote, wanakuwa "wenyeviti wa vyama vyao" zaidi. Wenye kuelewa wameelewa. Hilo ndilo tatizo letu kubwa. Hatujaweza kufikiria mbali zaidi kuhusu hizi kofia mbili. Rais akishachaguliwa kushika wadhifa huo, anapaswa kuwa Rais wa wote, na si kiongozi wa chama kimoja cha siasa.

Uko sawa kabisa,kila chama cha siasa kinataka chama kingine kiwe dhoofu ili kipate ridhaa ya kutawala,lakini si kwakutumia POLISI,MAHAKAMA au KUUA UHURU wa BUNGE.
 
Maswali kwa waziri mkuu yanajibiwa na naibu spika, huyu naibu spika hakuna kitu kabisa pale
 
Back
Top Bottom