Yahya Jammeh akataa kuachia uongozi Gambia

MASAA 2 YALIYOPITA:

Jeshi la Senegal limesema kuwa majeshi ya Afrika Magharibi yataingilia suala la Gambia usiku wa kuamkia tarehe ya mwisho wa madaraka ya Rais Yayha Jammeh ili akabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi uliopita.

Vikosi kutoka Senegal vimesogea katika mipaka ya Gambia, Nigeria pia imetuma vikosi vya anga katika eneo hilo.

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz yuko nchini Gambia kwa kile kilichotajwa kuwa ni juhudi za mwisho za kumshauri bwana Jammeh kuachia madaraka kwa Rais mteule wa Gambia Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal.

Senegali imeomba Jumuiya ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kushinikiza Umoja wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuchukua hatua za msingi katika kuhakikisha Rais mteule wa Gambia anakabidhiwa madaraka.
 
Kitu nachoona,inawezekana pia upinzani ukafanya mambo kinyume na sheria,upinzani waweza jipenyeza kwa watu wa ndani kabisa ktk serikali na tume ya uchaguzi na wakapindua mambo,sema tu kwa kua watu wanakua wanaupenda upinzani wanadhani upinzani hauwezi kucheza lafu
 
Kampa kampa tena:hivi akiba yao ya chakula ni tani ngapi ili kikinuka na sisi tukavamie magala yao ya chakula kwa kua vita vya panzi ni neema kwa kunguru ukizingatia unenge unatunyemelea Bongo
 
Jamiiforums nayo imtume mwandishi wa kujitegemea PASKALI Mayala kwa gharama zetu apande boti na kuvuka bahari kwenda mahali fulani na kumhoji mkuu wa huko nini msimamo wake kuhusu sakata la Gambia"
Ni mawazo yangu tuu, nimewaza kwa sauti.

ha ha ha ha ha uchokozi huu.
 
Huyu Rais wa GAMBIA Yahya Jemmey naona amedata kabisa

kama alikuwa hataki kuwachia madaraka kwanini alikubali kushindwa na kumpigia simu Rais mteule wa Gambia na kumpogeza kwa ushindi anaonekana mpumbavu kabisa

Na yakumbuka yale ya Rais wa Ivery Cost walimtoa Ikulu kama kuku yeye na mkewe na sasa cjui yupo Jela yule ...maan hawa watu hawana akili hata kidogo hii ngozi nyesi cjui tulikosa nn kwa mmungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…