Wizi wa udanganyifu wa tiketi katika SGR umenikumbusha walafi enzi za shule. Hakika "samaki mkunje angali mbichi"

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
45,371
64,010
Katika shule za secondary nilizosoma nyama na wali vilikuwa vyakula adimu sana hivyo siku vikipikwa ilikuwa ni harakati kubwa mithili ya "survival for the fittest". Nyama ilikuwa inapikwa mara mbili au mara moja kwa wiki, hivyo pia kwa wali. Watu wengi ambao walikuwa wanaonekana wastaarabu siku ya nyama au wali walikuwa tofauti kabisa, tabia zao hazikuwa mbali sana na zile za ngedere wanaovamia mashamba.

Mara nyingi siku za nyama au wali ugwaji wa chakula ulivuruga hadi vipindi vya masomo katika siku hizo. Kuna wanafunzi walililazimika kutohudhuria vipindi au kukatisha vipindi hadi kwa nusu saa kabla ya muda wa vipindi kuisha ili tu wawe mstari wa mbele kuwahi kuchukua chakula. Pia mara nyingi vipindi vingi vya baada ya lunch vilikuwa vinavurugika kwa sababu ugawaji wa chakula ungeweza kutumia hadi zaidi ya masaa mawili katika siku hizo tofauti na muda uliopangwa wa lisaa limoja.

Wanafunzi waliokuwa wanawahi zaidi kuchukua chakula walikuwa wanarudia kuchukua chakula tena mara ya pili ili jioni wasile maharage au ugali( huo mtindo ulipewa jina maarufu Paper 2). Ilibidi viranja wawe wengi sana kukagua wanaourudia kuchukua chakula mara ya pili(Paper 2). Pia viranja walikuwa wanajazana sana jikoni kujipakulia minyama au wali kwenye sado. Naona kama hizi tabia zimeakisiwa kwa wezi wa tiketi kwenye SGR, Hakika ni muhimu kuwa na malezi bora ya raia tangu wakiwa wanafunzi wadogo mashuleni.
 
raraa reree
Capture.PNG
 
Back
Top Bottom