Kila Rais (sio Chama wala Serikali wala wananchi) amekuwa na maamuzi yake mwenyewe ya kuhusu idadi ya Wizara, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu. Hii imekuwa na usumbufu sana sana kwa watendaji na pia imekuwa ikiathiri Bajeti na hata Mipango ya nchi.
Kwa mfano ukiangalia hivi karibuni Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa na mabadiliko sana. Kabla ya Wakati wa Uchaguzi mwaka juzi Ofisi hiyo ilikuwa Mawaziri wawili Jenister na Kairuki na Makatibu Wakuu watatu. Kwa maana hiyo suala la Uwekezaji lilikuwa chini ya Waziri Kariuki huku Mkongwe Jesnister akiwa na Kazi, Ajira, Vijana, Walemavu, Mambo ya Sera, Uratibu wa Kazi Serikali, Bunge . Yote hayo yalikuwa kwake Jenister. Kulikuwa na Maktibu Wakuu watatu ambao haijuilikani mipaka yao ilikuwa wapi. Baada ya Uchaguzi JPM akahamishia mambo ya Uwekezaji kwake na kumpa Kitila Mkumbo na wakati huo huo Waziri Mkuu akabakiwa na hayo mengine huku Jenister akiendelea kuyasimamia akiwa na Makatibu Wakuu wale wale watatu, Masawe, Nzunda na Mwaluko. Baada ya JPM kuondoka Samia akairudisha tena Uwekezaji kwa Majaliwa akimpa Waziri Mwambe na Naibu wake Marehemu Olenasha na Katibu Mkuu Kahyara. Kule Jensiter akabakishwa na akapewa Katibu Mkuu mmoja tu na Manaibu wawili na Manaibu Waziri Wawili tena.
Yaani ukiangalia muda wa mabadiliko yanavyofanyika na kutokana na tu na discretion ya mwenye mamlaka unaona kabisa kuwa hili jambo linapaswa liwekwe kwenye Katiba ili hata ikija tokea upinzani wakachukua nchi wasiweze kuyumbisha mpangapilio wa Mawizara na hata idadi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu wao. Hili ni suala la wananchi kwa sababu gharama za muundo wa utawala unahusisha kodi zao.
Kikubwa katika mipangilio hiyo ni namna wafanyakazi wa chini wanavyopata shida. Kila mabadiliko haya yakitokea Mawaziri, Makatibu Wakuu wao wakiapishwa tu na Rais tayari Ofisi zao zinawapokea na wanaendelea kama kawaida. Sasa ngoma huku chini huku. Ndugu yangu ambaye alikuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa sasa hata haelewi atahamishiwa wapi? Hajijui kama atakuwa Afya kwa Ummy au atapelekwa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wenye Mahitaji Maalum sijui kule kwa Dorothy Gwajima au viipi? yupo yupo tu hajui cha kufanya na pengine inaweza ikaisha hata mwaka akiwa hajijui. Kuna suala hili Kundi la atu wenye Mahiataji Maalum - ambalo kwa kawaida ni wazee, watoto, vijana, na walemavu, sasa hiyo ya Walemavu bado ipo kule kwa Ndalichako - je ni tofuati na hawa waliopelekwa kwa Gwajima? Yaani mambo ni mchanganyikeni tu!
Tukijiuliza ni kwa nini kwa mfano kusiwe na Wizara inayosimama yenyewe kwa mujibu wa Katiba inayohusu mambo ya Utumishi wa Umma, Kazi na Ajira? Kwa nini Kazi, Ajira na Vijana na Watu wenye Ulemavu imekuwa hivyo na ikawekewa kwa Waziri Mkuu? Kwa nini? Kwa nini kwa mfano kusingekuwa na Wizarailiyowekwa kwenye Katiba inayohusu Maendeleo ya Jamii na Mazingira? Why kuchanganya Maendeleo ya Jamii na makundi ya Watu wenye Uhitaji Maalum?
Kwa kweli katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa kimuundo watendaji wa chini wanapata shida sana - rafiki yangu mmoja aliyeamua kuajiriwa Serikalini tulipomaliza Chuo Kikuu mwaka 1997 ananieleza kwa muda wa miaka miwili hii amejikuta Ofisi yake ikibadilishwa Zaidi ya mara tatu na hivyo ameshindwa hata kujijua utendaji wake ukoje.
Ni vema sisi wananchi tuamue sisi Serikali yetu ime na Wizara ngapi, Zipi na idadi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wa kuziongoza! Tusikubali kuburuzwa buruzwa tu wkatik kodi zetu zinatumika. Tukiweka mpangilio huo katika Katiba hata watakaowekwa kushika nafasi hawatasemwa kuwa wanakula kwa umbali wa Kamba zao. Tunaweza tukaamua kumpa Rais mamlaka ya ya kuunda Wizara za dharura tu ambazo zitakuwa ni ndogo na zisizidi tano ili kubaki na Wizara Mama ambazo zinaweza kuundwa kwa mujibu wa Sekta husika bila athari zozote.