Wizara ya Habari acheni kuonea watumishi maskini, mnawasimamisha kazi waliowashauri mtoe fedha za matengenezo ya mfumo wa umeme mkakataa?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,038
4,752
Mhe. Rais kilichofanywa na wizara ya Habari hakina hata chembe ya Haki. Ukisoma barua ya wizara inasimamisha wafanyakazi kazi kisha barua hiyo hiyo inaeleza kwamba wanaharakisha mchakato WA tenda; unajiuliza Nani kawaambia wizara kama hitilafu ilivyotokea inahitaji tenda? Maana yake wanayo taarifa yenye mapendekezo kuhusu maboresho makubwa yanyohitajika katika mfumo wa umeme Ila wao waliyapuuzia nakukaa kimya.

Kinachosikisha ni kwamba Yule aliyeshauri matengenezo yafanyike anasimamishwa KAZI then Yule aliyekataa ushauri WA wataalamu anabaki ofisini. Huu ni ukatili Kwa watumishi WA chini; kibaya zaidi ukatili huu unafanywa siku ya wafanyakazi. Hizi nguvu za kisiasa zinatumika vibaya na panahitaji MTU wakuwasemea hawa wasio na hatia.

Niombe hatua zichukuliwe Kwa maafisa masuuri pamoja na waliopaswa kutangaza tenda ya ukarabati siyo waliotoa mapendekezo.

Mwisho, wataalum waliosimamishwa kazi wamekuwa walishauri michezo ya usiku isiruhusiwe lakini hakuna mtendaji WA Wizara aliyechukua hatua ; Leo yametokea maafa wale wenye akili wanasimamishwa na waliopuuza ushauri. Tutende Haki. Siyo hivyo tusome pia mapendekezo ya timu iliyoundwa baada ya MECHI yetu na Uganda utabaini hawa waliosimamishwa walipaswa kupandishwa vyeo wakachukue nafasi za hao waliopo wizarani wasiotaka kutumikisha ubongo.

Let assume taa zingezima YANGA WAKIWA WAMEFUNGWA MAGOLI MAWILI NA UMEME UKAKOROFISHA NA TAA ZISIWAKE HAYO MAUAJI TUNGEYAZUMZIAJE? TUTENDE HAKI TUACHE UONEVU KWA WASIOWEZA KUJIELEZA
 
Katibu Mkuu wa wizara ndio accounting officer, anashindwa kununua jenereta?

Halafu kama timu mwenyeji hujaza Lita 400 kwenye hiyo jenereta kwa ajili ya mechi yake, kwa nini tena inasomeka kwamba huwa wanatumia umeme wa tanesco? Ina maana timu mwenyeji ikishajaza mafuta, wao wanafunga wa tanesco, halafu hayo mafuta wanayauza?

Lita 400 sio pesa kidogo, tena ukipiga hesabu kwa mwaka, mara idadi ya mechi.
Nilikuwa nashangaa trend ya mechi za usiku, kumbe watu Wana jambo lao
 
Back
Top Bottom