Wizara ya Fedha na Mipango, Dangote walipe Kodi

Hivi tajiri nambari moja afrika unampigia kelele kwa milioni 400 ambazo wakinga hapo kariakoo wanatembea Nazo kwenye buti ya gari? This is non sense,mi nilijua bilioni 400!!
 
Hakuna nchi hata moja duniani ambayo hailindi wazalishaji wa ndani.
Ndiyo sababu ukiagiza bidhaa kutoka nje wakati hapa nchini zipo unahitaji kibali maalum.
Lazima upate kibali cha sekta husika kuwa wazalishaji wa ndani hawawezi kukidhi mahitaji yako.
Kama unaingiza sukari, unahitaji kibali toka Wizara ya Kilimo.
Kama unaingiza madini, (coal, gypsum, nk), unahitaji kibali toka Wizara ya Madini.
Mkaa wa Mawe (Coal) na Jasi (Gypsum), vinapatikana kwa wingi hapa nchini.
Kuagiza toka Afrika Kusini ni kudharau nchi yetu na serikali ya JPM ambayo haiwezi kuwekwa mfukoni na mfanyabiashara yeyote.
Ni kweli kabisa kuwa wakati wa awamu ya serikali iliyopita, Dangote alikuwa haguswi, na alitumia udhaifu huo wa utawala uliopita kufanya mengi ya hovyo, ikiwemo kukwepa kodi na kuajiri mpaka wafagiaji toka nje bila vibali.
TRA wamefanya special audit na kugundua ukwepaji wa kodi wa zaidi ya TShs Bilioni 20, ambapo Mhasibu Mkuu wa Dangote amepewa adhabu ya kulipa TShs Bilioni 1.5 kwa kuidanganya TRA,(filing false reports)
Upo uzi hapa JF uliolieleza hili jambo vizuri.
Kwa taarifa tu ya wanaJF, baada ya Dangote kuagiza meli hiyo (MV OLYMPIC PIONEER) ya tani 35,000 za gypsum toka Oman, Wazalishaji wa ndani ambao wana LPO za Dangote za ku-supply gypsum wameandikiwa kuwa bei imeshuka na asiyekubali aache kuendelea ku-supply.
Ni wapi hapa duniani, mtu mwenye LPO ya tani 1000, ambaye ameisha supply tani 500, anaambiwa, tena kwa maandishi, kuwa sasa bei imepunguzwa, na akitaka kuendelea ku-supply, akubali bei pungufu, au aache kumalizia ku-supply?
Kama Wizara ya Madini itaruhusu madini hayo yashuke katika Bandari ya Mtwara au kwingineko Tanzania, utakuwa usaliti mkubwa sana kwa nchi yetu na kwa Serikali ya Hapa Kazi Tu.
Watanzania tabia ya kujisikia na kujiona nyie miamba kumbe hamna lolote,bilioni ishirini dangote alisema hesabu iwekwe mezani watalipa baada ya kuwasiliana na Mtaalam wao wa mahesabu,mtu aliyewekeza trilioni moja juzi tu unampigia kelele za bilioni 20!! Hiyo migodi ya almas ya mwadui inayopata hasara kila mwaka je?na haijawahi kulipa hata mia kama kodi? U
 
Mitambo ya hizo kampuni ni ya kale....kila siku wanagombana na wakazi wa wazo kuhusu uchafuzi wa mazingira.....dangote ni state of the art technology ,hivyo viwanda vingine mitambo yake unaweza kuichonga hata juakali kwa wale watengeneza karai kwa kutumia mapipa @chipukizi,mbeya cement na tanga cement ni hovyo
 
Kaka Tatizo si kununua kutoka Afrika kusini,Tatizo ni KUTOKULIPA KODI VAT 18%
Ulipeleka madai ya kodi hayakulipwa? Na unafikiri ukipeleka tu unalipwa? Kuna wahasibu ambao ni the best brain na kuna makampuni bora kabisa ya kihasibu ya ku-verify claims pamoja na wanasheria makini na bora kabisa Tanzania na afrika wa kutafsiri sheria,dangote sio sehemu ya kuleta madai ya hovyo ukataraji kulipwa,hivi unafikiri tajiri namba moja afrika atakaa mbali na wataalam namba moja afrika na duniani?wahasibu namba moj afrika,wataalam wa kodi namba moja afrika ,wanasheria namba moja afrika??? Mtakaa chini Mwaka huu
 
STAMICO wataanza kuzalisha makaa ya mawe KIWIRA hivi karibuni.Tatizo hilo (la kuimport COAL) litaisha mara moja
 
DANGOTE yalipa kodi ya zaidi ya milioni 400.

Serekali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania yalipwa kodi wa zaidi Milioni 400 kutokana na uingizaji wa Chokaa (Gypsum) katika kiwanda cha Dongote Cement Mtwara.

Kodi hii imelipwa baada ya serekali kukataa maombi yaliyo ombwa na kampuni ya Dangote kwamba isamehewe kodi ya kuingiza Makaa ya mawe na Chokaa (GYPSUM), Wizara ya fedha na mipango mnamo tarehe 06 June2016, iliiandikia barua kampuni ya Dangote ikiwataarifu kwamba ni lazima walipe kodi kama inavyotakiwa. (..In view of our above, we would like to advise you to pay the required taxes accordingly.) kwa mujibu wa sharia ya kodi ya ongezeko la thamani VAT ya mwaka 2014. Barua hii imesainiwana Katibu Mkuu.

Malipo haya ni kwa ajili ya kuruhusu meli ya MV OLYMPIC PIONEER kutoka Omani, kuingiza chokaa (GYPSUM) mwezi huu wa Juni.

Hata hivyo meli hiyo haitaweza kuruhusiwa kushusha chokaa hiyo kwani bado wanadaiwa zaidi ya bilioni Moja (1billioni) ya malimbikizo yanayotokana kuingiza Makaa ya mawe mwezi Novemba 2015.

Pamoja na Serekali kupata kiasi hiki kidigo cha pesa ya VAT kutokana na uingizaji wa chokaa (GYPSUM) na makaa ya mawe, kuna Maswali ya kujiuliza.

1. Je ni kwanini kiwanda hiki kimetengeneza mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia Mkaa wa mawe badala ya kutumia gesi ambayo inapatikana Mtwara?

2. Na Je? Kwanini Wanaagiza makaa ya mawe kutoka afrika ya kusini badala ya kutumia makaa yam awe yaliyopo hapa Nchini?

3. Je ni kwanini hawanunui chokaa (GYPSUM) ya Lindi, Itigi na Makanya.

4. Je? lile lengo la kiwanda hiki kutumia mali ghafi za hapa nchini limetaifishwa na nani?
Kwa hiyo ulitaka umpangie hata mitambo ya kuweka? Una ubia wewe au serikali? Kama akiagiza nje wewe kinakuuma nini? Asipouza si hasara kwake? Unafikiri biashara kaanza juzi huyu eti? Tanzania kama nchi imeshindwa nini kujenga kiwanda hicho mpaka ikamfuata dangote? Unajua dangote ana viwanda vingapi vya simenti? Hebu usituchoshe....kanunue dagaa umpelekee mkeo akupikie.....Dangote habari ingine,na sio dangote platnumz diamond wa tandale....huyu ni dangote haswaaaaa na uwe na heshima unapomjadili
 
Chuki binafsiiiiiimakazini,majumbani........sasa ni kero......inaweza kuzua tafaraniiii,

Unaonekana una chuki binafsi,wa mbele wa mbele tu,dangote habari engine wewe,anaweza akawaambia muache kulipa vi kodi vyenu nchi nzima kwa miaka mitano na kila mtu,ukiwemo wewe,ukalipwa mshahara

Kulipa kodi ni wajibu wa kila mtu katika nchi yoyote Duniani. Hakuna mwenye chuki nae.

Lengo la kujenga kiwanda lilikuwani kutumia gesi lakini wanasema walijenga mtambo wa makaa ya mawe kwa makosa, nimeona kakipande ka waraka wao kamevuja mtandaoni

kwa hiyo wakati wakiendelea kujenga mtambo utakao tumia umeme wanaomba waingize makaa ya mawe bure yaani wasamehewe kodi.

Hapo sasa ndipo serekali ikakataa kuwasamehe kodi na wamelipa huto tusenti.
angalau watachangia madawati. Lengo letu walipe na zile nyingine walizokwepa mwezi wa Novemba mwaka jana, zaidi ya Bilioni Moja.
 
Attachments

  • tulikosea.jpg
    tulikosea.jpg
    168.2 KB · Views: 48
STAMICO wataanza kuzalisha makaa ya mawe KIWIRA hivi karibuni.Tatizo hilo (la kuimport COAL) litaisha mara moja
Dangote anazalisha mifuko 7500 kwa siku mkataba wa Tanzania na iliitaka serikali kuiuzia Tani 13,500 za makaa ya mawe ya Ndani kila mwezi,Tancoal wakasema wanauwezo wa kuzalisha Tani 3000 tu kila baada ya wiki mbili ukiangalia kwa umakini bado tunasafari ndefu sana katika uzalishaji na mifumo yetu kiwanda kile kinauwezo mkubwa kuzalisha kinahitaji malighafi nyingi kuliko uwezo wa wazalishaji wa ndani Maswali magumu
1 Tumepewa fulsa Tumeitumia?
2 Watu tulio wapa dhamana wanatekeleza majukumu yao ipasavyo
3 Wabongo wenyewe tunatambua fulsa hii?
4 Nini jukumu la Serikali kuhakikisha vifaa mitambo na wataalamu wanaingia mzigoni kukilisha kiwanda hiki?ama tutakuwa na malalamishi yasiyoishaa??Kaka Iparamaswa njoo na hoja zitakazo amsha hamasa kwa Taifa maswala ya vijembe kejeli porojo tuu havitu saidii but hayo ni mawazo yako anyway.
 
Hakuna nchi hata moja duniani ambayo hailindi wazalishaji wa ndani.
Ndiyo sababu ukiagiza bidhaa kutoka nje wakati hapa nchini zipo unahitaji kibali maalum.
Lazima upate kibali cha sekta husika kuwa wazalishaji wa ndani hawawezi kukidhi mahitaji yako.
Kama unaingiza sukari, unahitaji kibali toka Wizara ya Kilimo.
Kama unaingiza madini, (coal, gypsum, nk), unahitaji kibali toka Wizara ya Madini.
Mkaa wa Mawe (Coal) na Jasi (Gypsum), vinapatikana kwa wingi hapa nchini.
Kuagiza toka Afrika Kusini ni kudharau nchi yetu na serikali ya JPM ambayo haiwezi kuwekwa mfukoni na mfanyabiashara yeyote.
Ni kweli kabisa kuwa wakati wa awamu ya serikali iliyopita, Dangote alikuwa haguswi, na alitumia udhaifu huo wa utawala uliopita kufanya mengi ya hovyo, ikiwemo kukwepa kodi na kuajiri mpaka wafagiaji toka nje bila vibali.
TRA wamefanya special audit na kugundua ukwepaji wa kodi wa zaidi ya TShs Bilioni 20, ambapo Mhasibu Mkuu wa Dangote amepewa adhabu ya kulipa TShs Bilioni 1.5 kwa kuidanganya TRA,(filing false reports)
Upo uzi hapa JF uliolieleza hili jambo vizuri.
Kwa taarifa tu ya wanaJF, baada ya Dangote kuagiza meli hiyo (MV OLYMPIC PIONEER) ya tani 35,000 za gypsum toka Oman, Wazalishaji wa ndani ambao wana LPO za Dangote za ku-supply gypsum wameandikiwa kuwa bei imeshuka na asiyekubali aache kuendelea ku-supply.
Ni wapi hapa duniani, mtu mwenye LPO ya tani 1000, ambaye ameisha supply tani 500, anaambiwa, tena kwa maandishi, kuwa sasa bei imepunguzwa, na akitaka kuendelea ku-supply, akubali bei pungufu, au aache kumalizia ku-supply?
Kama Wizara ya Madini itaruhusu madini hayo yashuke katika Bandari ya Mtwara au kwingineko Tanzania, utakuwa usaliti mkubwa sana kwa nchi yetu na kwa Serikali ya Hapa Kazi Tu.
Baadhi ya watu ndani ya mamlaka wamenufaika sana na mpango huu,kampuni Tatu za ulinzi zote ni za wageni na moja inamilikiwa na aliekuwa mkuu wa Jeshi la China nyingine ambyo inanyanyasa vibaya wazawa inamilikiwa na Mhindi aliewatukana uhamiaji wakamtia ndani,JKT yetu Njee...Walikiuka taratibu za wizara ya madini hawakuwa na vibari vya wizara husika walifanya hivyo mwezi November walipoingiza Tani Elfu 45 wakapigwa jalambe la kulipa wakatoa miezi mitatu hawakulipa hadi leo wamekuja tena bila kibali wakaja na Meli mbili moja ina Tani Elfu 36 za Makaa toka AK na nyingine Tani 36 za chokaa toka Omani bila kibali cha Wizara husika acha dharau hiyo ambapo ndugu zangu kwa Taarifa tu hata Dangote alikuwa hajui,ni Dili za wahindi na wale Wanaijeria pale na baadhi ya Wabongo wa TIC,Uzuri Idara zote zimelivalia njuga swala hili na Dangote mwenyewe tayari amesha leta Mkurugenzi mpya na uongozi wa kale unarudishwa nyumbani,

Iparamasa haoni Tatizo kuacha watu kuingiza mizigo kwa njia hii ni hatari kubwa kwa usalama wa Nchi anasema ni
"Chuki binafsiiiiiimakazini,majumbani........sasa ni kero......inaweza kuzua tafaraniiii,

Unaonekana una chuki binafsi,wa mbele wa mbele tu,dangote habari engine wewe,anaweza akawaambia muache kulipa vi kodi vyenu nchi nzima kwa miaka mitano na kila mtu,ukiwemo wewe,ukalipwa mshahara"
 
Mnasherehekea Dangote alipie VAT wakati mlipaji wa VAT ni mlaji? Dangote hapo ni kama mkusanyaji tu.

Hakika Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.
Kweli tupu dada FF. unajua watu wasichokijua ni Kodi ya ongezeko la thamani. Hapa Dangote itapitia kwake tu, mlipaji ni mlaji. Watu hawalijui hilo. Hata hivyo kwa kuwa tumehamasika, basi Dangote alipe tu hizo kodi, ni jambo jema!

Mengine sijui ila kuhusu Umeme nahisi miundombinu ya gesi kule Mtwara haiko katika utayari wa kuingizwa kiwandani kwa sasa!
 
Back
Top Bottom