Wizara ya afya imulikeni hopitali ya KS iliyoko Mbeya

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Wizara ya afya na ustawi wa jamii na/au kamati ya afya mkoa/wilaya ya Mbeya imulikeni hospitali ya Ks iliyoko maeneo ya Mafiati.

Hospitali hii licha ya kutulipa watumishi wake mishahara duni ya hadi Laki moja(100,000/=) kwa mwezi huwa haiwasilishi michango yetu ya kila mwezi kwenye mifuko ya Kijamii(NSSF, PSPF, LAPF). Tume jaribu kuuliza lakini tunapigwa danadana kila mara. Ikitokea ukaonekana unafuatilia sana unafukuzwa kazi kwa mdomo na wala sio kwa barua kama ambavyo inatakiwa.

Watumishi wa hapa tunahudumia wagonjwa wengi sana wa bima na cash kwenye kila shift tunayoingia lakini pamoja na hayo yote hatuthaminiwi. Unafanya kazi hadi unakuja kuondoka au kufukuzwa let's say baada ya miaka mitano au hata mwili lakini kwa muda wote huo hakuna hela ambayo imekuwa ikipelekwa kwenye mifuko tajwa hapo juu licha ya kukatwa. Tuna wasiwasi kuwa huenda hata kodi ya serikali itakuwa inawasilishwa TRA licha ya kukatwa kila mwezi.

Hivyo basi tunaiomba Wizara ya afya
na/au kamati ya Afya mkoa/wilaya ya Mbeya kuimulika hospitali hii na ikiwezekana kufika kujionea hali halisi.

Naomba kuwasilisha.
 
Huyo muhaya ana roho mbaya kweli, tafuta pengine kijana; lkn kwa life la Mbeya unaeza ishi hata kwa 50k
 
Hivi Dr Danny bado yupo? Niliwahi kuona uzi wake hapa watu wanalalamika ana degree moja lakini anafanya majukumu ya daktari bingwa wa mifupa
 
Huyo muhaya ana roho mbaya kweli, tafuta pengine kijana; lkn kwa life la Mbeya unaeza ishi hata kwa 50k
Kumbe ni mhaya!!

Dah kaka tunataabika. Imagine anamlipa mtu Laki moja kwa mwezi halafu mtu huyo anakatwa sijui NSSF na Bima lakini pamoja na hayo hela haifiki inakotakiwa. It is unfair.
 
Back
Top Bottom