Wizara 3 zaungana kuwasaka wazushi wa ajira za Waalimu

Hilo ni tatizo lao na haliwahusu walimu wanaoendelea taabika mtaani. Watoe ajira..
 
Upotoshaji wa namna hiyo una nia ya kuichonganisha Serikali na waajiriwa watarajiwa katika kada ya Ualimu. Police na TCRA chukueni nafasi yenu!
 
Ivi atakae shikwa ni alie itunga na kuipost(the first person who created it)... au hata hawa wenye vihele hele.... maana wengine walisambaza wakijua kuwa ni kweli ile taarifa. .. na ilileta shida sana kabla ya kanusho la wizara..
 
Wangeungana hivyo kusaka watumishi hewa,majangili mbugani,kupambana na wauaji,kuimarisha reli,kutengeneza madawati na mengine yenye tija tungekuwa mbali sana.
 
Watu tunakufa njaa huku,wenyewe wamekazana kumtafuta aliesema ajira hakuna...WAACHE MAIGIZO WATANGAZE AJIRA...WATU TUMESAHAU HATA MAP INAFUNDISHWAJE
 
....google wamemaliza kunitumia "captcha" naonekana nimehama ghafla kutoka Carribean hadi Australia, ISP wangu ndio hanioni kabisa maana hata kifurushi sina na Window hapa inanionyesha "unknown internet connection" wakati nipo hapa Ng'washilalage - Kwimba, Mwanza! Jamani wazungu hawa ni shidaa!
 
sisi chadema tunasema kuwa huyo mtu atafutwe na afikishwe mahakamani na akipipwa fine tutamchangia.
 
Wizara zifanye mambo ya maana, sio kushughulika na mambo madogo madogo kama haya ya mitandaoni.

Madawati ya kutosha watoto kukaa washapata??
Hilo la madawati mbona lishaisha kimkakati au we ulikuwa mtoro? Acha serikali ifanye kazi yake ambayo tumeikabidhi kikatiba, kama unaona so vipi kaweke pingamizi mahakamani ama vipi zungusha mikono hewani
 
Unajua MTU ukiwa na siri baadae ukagundua ile siri imevuja lazma ulipuke
Wizara zifanye mambo ya maana, sio kushughulika na mambo madogo madogo kama haya ya mitandaoni.

Madawati ya kutosha watoto kukaa washapata??
 
Back
Top Bottom