Wito kwa Jukwaa la Wahariri na Wamiliki wa vyombo vya habari nchini

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,550
Wasalaam wapendwa Wanajukwaa.

Napenda kutoa wito kwa Jukwaa la wahariri na wamiliki wote wa vyombo vya habari nchini kupanga siku maalum ya kukutana na kufanya vikao vya dharura kujadili kauli ya Mhe Rais wetu Mama Samia Suluhu ambaye kwa nia njema kabisa na kwa utashi wake wa kutaka watanzania kupata taarifa bila tatizo.

Mhe Rais Samia Suluhu aliagiza vyombo vyote vya habari vilivyofungwa vifunguliwe na wamiliki waelezwe namna ya kufuata sheria. Rais amelisema hili wazi na hadharani dunia nzima unatazama kupitia Runinga, na mitandao ya kijami,Wamejitokeza watanzania wachache waliolewa madaraka na roho zao mbaya zenye ubinafsi na kukana kauli ya Rais hadharani kwa kudai eti aliagiza Online TVs tu kitu ambacho si kweli, kutaja Online TVs mhe Rais wetu alitolea mfano. Hawa watu wanawafanya watanzania wote ni wajinga, tunahitaji watuambie nini maana ya vyombo vya habari.

Ndugu zangu Wamiliki wa vyombo vya habari na jukwaa la wahariri tushughulike na jambo hili mapema ili kama ni kumuona Mhe Rais moja kwa moja tufanye hivyo ili tuweze kupata tafsiri ya kauli yake moja kwa moja kama mhusika.

Watu wachache wasiopenda kuona watanzania wanapata kwa manufa yao binafsi wamefahamika na hawa ndio bimwazo vikubwa kwenye ustawi wa taifa letu.
 
Huna cha kuwafanya wasukuma hata kama huwapendi.

Rais Samia ndiyo kwanza kawaongeza kwa kuwateua kwenye serikali yake.
 
Hebu wacheni kukimbia ukweli msipeleke lawama pasipostahili kwa kujidanganya mfurahishe nafsi zenu kwa hicho kipenzi chenu.

Kama Rais amekubali kushawishiwa na hao basi tatizo ni la Rais sio hao subordinates wake, haiwezekani mtu mwenye madaraka ya juu kabisa afuate ushauri wa watu wa chini yake kama hajauridhia, nani wakumlazimisha kufanya hivyo?

Kubalini ukweli Rais ni dhaifu, hana msimamo, bado anafanya kazi kwa kubahatisha, ndio maana leo anateua huyu kesho anatengua, mara atangaze hivi kesho yake akanushe, huyu mtu asie na msimamo mpaka ashawishiwe na watu wa chini yake hafai kuliongoza hili taifa.
 
Mh Rais hapa kakubali kulazimishwa waziwazi kupindisha maagizo aliyoyatoa awali
 
Back
Top Bottom