EMMANUEL ZACHA
Member
- Sep 6, 2021
- 24
- 111
Siyo ule wimbo tunaoimba huku tumesimama wima mithili ya askari anayelinda benki ya CRDB.
Siyo ule wimbo ulioimbwa kabla ya Timu ya Taifa kupigwa risasi moja ya kichwa na Timu ya Taifa ya Uganda katika michuano ya CHAN pale kwenye uwanja wa Mkapa. Siyo huo !
Huu ni wimbo sugu unaoimbwa na Wanakwaya wenye Digrii za Shida na 'P.H.D' za Njaa ambao sauti zao zimekauka kutokana na kukosa virutubisho vya keki ya Taifa.
Siyo ule wimbo ninaoimba kwa hisia za kizalendo kutoka moyoni na kuapa kuwa nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee. Siyo huo !
Huu ni wimbo unaoimbwa kwenye Redio ya Walala Hoi FM lakini wasikilizaji wakisikia wimbo huu, huzima redio na kwenda kwenye hoteli ya kifahari kunywa maziwa ili kukata sumu na shombo ya sauti walizosikia.
Siyo ule wimbo mtamu wenye vitamini Utu na Protini ya Uafrika wenye beti mbili zilizopangwa kwa sauti nne (4) unaomuomba Mungu kudumisha uhuru na umoja, wake kwa waume na watoto. Siyo huo !
Huu ni wimbo mchungu wenye beti za majonzi na masikitiko wenye sauti tatu (3) mithili ya mafiga.
ZIFUATAZO NI SAUTI TATU (3) MUHIMU ZA WIMBO HUU.
SAUTI YA KWANZA.
Hii ni sauti ya Wanaharakati wenye kiu ya usawa na Walokole wenye njaa ya haki wanaotamani kuona Katiba yetu inapelekwa Hospitali ya Umma (Wananchi) ili kufanyiwa oparesheni ya mabadiliko.
Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa lakini Katiba ni roho ya Taifa. Tusicheze na roho ya Taifa tukapoteza uhai wa haki na maendeleo.
Tunahitaji kurekebisha Sheria kandamizi ili kutibu virusi vya udhalimu na umasikini kabla havijaenea kwa kasi.
ZIFUATAZO NI SHERIA ZINAZOHITAJI KUREKEBISHWA.
1. Ibara ya 74. Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano. Ibara ndogo ya (1) na (2) inahitaji kurekebishwa.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Wajumbe wengine wa Tume ya Uchaguzi wasiteuliwe na Rais.
Kitendo cha Rais kuteua watendaji wakuu wa Tume ya Uchaguzi ni sawa na Simba na Yanga wawe na mechi ya ligi halafu Mohamed Dewji (MO) ndiyo awe refa wa mchezo. Haya ni maajabu ya Dunia! Kwa mazingira ya namna hii unaanzaje kutangaza bosi wako kashindwa?
Hili jambo ni gumu kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
JE, WASIPOTEULIWA NA RAIS, IPI NI NJIA SAHIHI YA KUPATIKANA KWA VIONGOZI WA TUME YA UCHAGUZI ?
Kwa mtazamo wangu, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Wajumbe wengine wa Tume, wangepaswa kuwa Wanasheria ambao wangetakiwa kuandika barua ya maombi ya kazi wakiambatanisha vyeti na wasifu wao (C.V) kwenda kwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika -Tanganyika Law Society (TLS), ambaye yeye pamoja na Baraza la Uongozi la TLS wangepitia barua na wasifu wa waombaji na kisha kupigiwa kura na Baraza la Uongozi, Viongozi wa Mikoa pamoja na Sekretarieti ya Chama hicho.
Hayo ndiyo mawazo yenye ubora wa 'TBS' kuhusu njia sahihi ya kuwapata Viongozi wakuu wa Tume ya Uchaguzi.
2. Sheria nyingine inayohitaji kurekebishwa ni ibara ya 41 kifungu kidogo cha (7).
Sheria hii inakataza matokeo ya Rais kuhojiwa mahakamani. Hii ni sheria kandamizi inayotakiwa kurekebishwa ili kutoa nafasi kwa mtu ambaye hataridhika na matokeo, kupata haki ya kupinga matokeo mahakamani kwa kukata rufaa.
3. Jaji Mkuu asiteuliwe na Rais. Sheria nyingine inayohitaji kurekebishwa ni ibara ya 118 (2) ambayo inampa maamuzi Rais kumteua Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu asiteuliwe na Rais ili kuongeza uhuru wa Mahakama kuanzia kwenye nguzo kuu.
JE, JAJI MKUU ASIPOTEULIWA NA RAIS, IPI NI NJIA SAHIHI YA KUMPATA JAJI MKUU ?
Tume ya Utumishi ya Mahakama ipendekeze majina matatu, halafu ipeleke majina hayo Bungeni ili kupigiwa kura za ndio au hapana kisha Rais ateue jina moja miongoni mwa hayo.
Hiyo ndiyo njia sahihi ya kumpata kiongozi wa Nguzo mama ya Mahakama.
(PICHA) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Hiyo ndiyo sauti ya kwanza ya Wimbo huu.
Tuendelee kuimba wimbo wa Katiba mpaka pale wasikilizaji watakapoupenda wimbo huu na kuuweka kwenye simu zao kama mlio wa kupokea simu.
SAUTI YA PILI.
Hii ni sauti ya Wanakwaya wa Kanisa la Mtakatifu Mama Ntilie, wanaonung'unika bei ya Mafuta ya upako kupanda hivyo kukosa faida kwenye chapati wanazowapikia waumini wao na wengine kufunga biashara kabisa.
Waumini nao wanalalamika kukosa nguvu za ujenzi wa Kanisa kutokana na chapati ndogo wanazopikiwa kutokana na bei ya mafuta ya upako kupanda.
Muumini mmoja jasiri alimwambia Mchungaji wa Kanisa " Baba Mchungaji, tunapikiwa chapati ndogo sana siku hizi kutokana na mafuta ya upako kupanda bei" Mchungaji akasema "hiyo inasababishwa na ubatizo wa waumini wa Ukraine na Urusi.
(PICHA) Mama Ntilie wa Mbagala akipika chapati ndogo kutokana na mafuta ya upako kupanda bei.
Waumini wengine wanaoimba sauti ya pili ni Wanakwaya wa Jumuiya ya Mtakatifu Tanganyika, wanaonung'unika kimoyomoyo kuhusu ongezeko la zaka na sadaka katika kila huduma za Kiinjili na Kiroho zinazotolewa hapo kanisani.
Hiyo ndiyo sauti ya pili. Tuendelee kuimba wimbo huu mpaka pale Wachungaji watakapochukua hatua za makusudi kudhibiti bei ya mafuta ya Upako na Mifumuko mingine ya sadaka kila uchao.
SAUTI YA TATU
(KORASI)
Tusichoke, tusiwaonee aibu Wachungaji. Tupaze sauti bila kuihurumia pumzi.
Vinywa vyetu vigeuke Viwanda vya mabadiliko, vizalishe sauti mfululizo kwa kujali Uzazi wa Mpango. Uzazi wa Mpango ni nini ? Ni kupaza sauti kwa utaratibu bila kuharibu amani ya Kanisa.
Umoja na mshikamano iwe dawa ya kuzibua masikio ya Wachungaji ili wazisikie sauti za waumini wao.
Na hiyo ndiyo bei nafuu ya kununua bidhaa ya haki katika duka la Mzee Jamhuri.
Ahsanteni sana.