Wimbo wa Nikki Mbishi '' I am Sorry JK'' wampeleka kujieleza BASATA

Hivi BASATA kumejaa Wazee waliopitwa na Wakati?

Wimbo wa Nikki Mbishi ni Protest/Appreciation song iliyoelezewa Kwa sanaa ya hali ya juu.

Protest songs zimeimbwa na wasanii wakubwa kina Bob Marley, Bob Dylan, Peter Tosh, Tupac

Lakini pia Nikki Mbishi katumia haki yake ya kikatiba kutoa maoni yake kwamba kammiss JK tatizo liko wapi?.

BASATA wasiue sanaa kwa kujipendekeza, wafanye kazi kwa weledi bila kutaka na wao waonekane kumbe wapo!!!

Au wanataka watu waimbe miziki laini laini isiyo na meseji nzito za kisiasa na hali halisi mtaani?. Ikifikia hali hiyo then BASATA itakuwa ni useless!!
 
jamani jamani....eeeeeh ni kwamba kila mtu anataka kuonyesha sasa hv anafanya kazi ama ni nini?? hii nyimbo mbona ina muda kidogo au wahuska walikua hawajaisikia... hlf mambo mengine mbona ya kawaida sana... itafika mahala itabd kupewa kibali cha kukohoa aisee
Kama utakohoa kwa matusi wacha upewe kibali
 
jamani jamani....eeeeeh ni kwamba kila mtu anataka kuonyesha sasa hv anafanya kazi ama ni nini?? hii nyimbo mbona ina muda kidogo au wahuska walikua hawajaisikia... hlf mambo mengine mbona ya kawaida sana... itafika mahala itabd kupewa kibali cha kukohoa aisee
Ukionekana upo upo unatumbuliwa tu chap. Hakuna namna. Wacha wajibaraguze bwan. Ajira ngumu
 
Kama utani vile Roma akaamua kuimba K,wengi tunatamani atoe zile aina ya ngoma alizokuwa anatoa kipindi cha Jk ila ndo hivyo..
 
Mbona wimbo kaimba ukweli au ukweli hauhitajiki sasa hivi, si tumeona wanafunzi wengine wamekosa mkopo mbona mambo mengine hayahitaj hata toch kwani si maisha magumu unga saiz 1900 hilo nalo linahitaj nini kulijuaa, kwa hiyo wanataka wasanii wote waimbe singel?
 
Dunia ya sasa Kosa kubwa ni Kuongea ukweli. TELLING THE TRUTH IS A NEW CRIME
 
Mbona wimbo kaimba ukweli au ukweli hauhitajiki sasa hivi, si tumeona wanafunzi wengine wamekosa mkopo mbona mambo mengine hayahitaj hata toch kwani si maisha magumu unga saiz 1900 hilo nalo linahitaj nini kulijuaa, kwa hiyo wanataka wasanii wote waimbe singel?
Msema kweli siku zote hupingwa, nafkr wanataka wasanii wote wabane pua
"Njoo usiogope uone Tanzania ya vibanda"
 
BASATA wataua creativity , waache vijana wawe free kuelezea maisha, iwe ni kisiasa, jiuchumi na kijamii!

Hebu chukulia mfano Wimbo wa Sugu enzi zile ukiitwa hali halisi, kuna mstari mle unasema, " ipo siku sisi tutaandamana mpaka ikulu kwa rais, tukamweleze hali halisi", lakini Hakuitwa kuhojiwa hii ni kwa sababu mamlaka za Nyakati hizo zilikuwa na watu wanaojua wanafanya nini.

BASATA ikianza kutumika kama chombo cha kisiasa kucensor kila kitu tutaendelea kuwa na wasanii waimba mapenzi tu wasio na input ya mashairi yoyote ya kuibua fikra!.

Ni aibu sana BASATA kuwa na mentality za kizeezee uliopitwa na wakati.

BASATA waelewe tu kwamba kusifiwa kwa raisi wa Zamani haimaanishi kutukanwa kwa raisi aliyeko madarakani, na yeye akiwatendea wema watu muda wake ukifika atakumbukwa tu kama wenzie!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom